Wazo: Kutumia njia mbadala kufikisha ujumbe kwa wananchi

Akilindogosana

JF-Expert Member
Jan 12, 2020
2,836
8,612
Leo pametokea figisu kwa wagombea kukatiwa matangazo na vyombo vya habari baada ya kinachosemekana ni maagizo toka "juu".
Sasa wazo la haraka ni kutumia mitandao ya kijamii na kununua vifaa kama video camera na live U solo.

Kisha youtube channel iwe ya mtu anayeendesha awe nje ya nchi. Anawapa wahusika wa Tz credentials na rtmp stream key. Kisha watu wa subscribe na kushare.
Ila nikazidi kuwaza, hivi mitandao na yenyewe ikifanyiwa figisu itakuwaje? Je wangapi wana simu zenye mtandao? Je watu wanaoishi mahali pasipo na mtandao watafikiwaje?

Nikawazaaaaaaaaaaaa nikawazaaaaaaa nikawazaaaaa
Sasa ndio nimekuja na mawazo marahiiisiiii.

1. Inabidi hotuba zirekodiwe kama video na audio kisha. Zisambazwe kwa njia ya flash, bluetooth, memory card au gari litembee na tv watu waone. Hizi video na audio inabidi zipewe watu wa muhimu katika jamii ambao wanaonana na watu wengi, na wahusika wa maeneo ambapo watu wengi wanakutana kama bodaboda, mabanda ya mpira, mabar, watu wanaoweka nyimbo kwenye simu na memorycard, wachajisha simu wa umeme na solar, wafanyabiashara kwenye maduka, vyombo vya usafiri kama daladala, vijiwe vya kahawa na alkasus, vijiwe vya kubeti, magari ya matangazo, wauza sumu ya panya/mende/kunguni/viroboto, vijiwe vya bonanza, saluni,mialoni, maeneo ya kidini, migodini, kwenye minada, masokoni, mitumbani,mashineni, vicoba, waosha kucha, mafundi nguo, waganga wa kienyeji, vibarua wa mashambani, wapasua mbao, wauza mkaa, mafundi viatu, wengine mtawaongeza.

Hii mbinu ni nzuri na rahisi. Maana hata asiye na bando anapata ujumbe, pia hata mwenye simu isiyo na intaneti "fekelo" anapata ujumbe cha msingi simu iwe na bluetooth na memory card.

Hii mbinu rahisi haiwezi kufanyiwa figisu ya maagizo toka juu. Wala hakuna kigogo anayeweza kuizuia bluetooth au memory card kufanya kazi. Hakuna polisi wa kukamata bluetooth wala tcra wa kukamata memory card nchi nzima. Hata Tv zote na radio na mitandao ikigoma bluetooth na memory card itafikisha ujumbe hata mahali pasipo na mtandao au hata radio.

Nashauri kwa kuanzia irekodiwe hotuba ya spana nzito kwa audio na video kuhusu 50m kila kijiji na mtaa. Isiwe ndefu sana isije kujaza memory card na kuchukua muda mrefu kuhamishwa. Ila ifikishe ujumbe na kuomba kura.

Nawasilisha
=======================

Amazon product ASIN B0756H8YFR
51H-xEdWglL._AC_SL1500_.jpg

======UPDATES===========
Siwezi kuendelea kuandika wazo langu naona kama nauza ramani ya vita kwa adui. Huu uzi wangu umeforwadiwa kwenye group fulani ambalo mimi mwenyewe nimo. Wahusika ambao mnataka niendelezee mje PM na vithibitisho ndio nitamalizia humo PM.
 
Amazon product ASIN B0756H8YFRView attachment 1533090

======UPDATES===========
Siwezi kuendelea kuandika wazo langu naona kama nauza ramani ya vita kwa adui. Huu uzi wangu umeforwadiwa kwenye group fulani ambalo mimi mwenyewe nimo. Wahusika ambao mnataka niendelezee mje PM na vithibitisho ndio nitamalizia humo PM.
Ccm wanakoelekea na jamaa lao ni kuzima midomo ya watanganyika, hiyo ni baadhi ya kuzima vitu vyote vya kutoa taarifa.
 
Back
Top Bottom