Wazo kuhusu uhuru wa kamati ya maadili ya uchaguzi

Hey

JF-Expert Member
Apr 26, 2008
1,030
1,116
Baada ya adhabu kutolewa ya Mgombea urais wa CHADEMA kutokuendelea na kampeni, tumeona kinachoonekana kama juhudi za tume ya uchaguzi kujiweka pembeni na maamuzi haya, na badala yake kuonyesha kwamba ni matokeo ya maamuzi huru ya vyama vyenyewe, ikiwemo CHADEMA.

Katika press ya leo, mwenyekiti wa CHADEMA ametufunulia kidogo kuhusu muundo na ufanyaji kazi wa kamati hii, kwa kusema inaundwa na vyama vyenyewe pamoja na mwenyekiti na katibu wa tume, pengine wakiwa na nafasi ya uongozi.

Na pia tumefahamishwa kwamba Kati ya kura zilizopigwa za vyama 15, 13 vimekubaliana na kumwondoa mgombea urais wa CHADEMA kwenye uchaguzi. Nadhani haihitaji akili nyingi ku speculate ni vyama vipi viwili vilivyopingana na maamuzi haya.

Mwenyekiti wa CHADEMA ameripotiwa kusema vyama vilivyounga mkono maamuzi haya vinatumika na chama tawala.

Katika mazingira ambayo demokrasia ya vyama vingi ina changamoto ambazo baadhi wanaweza kuziita existential, katika mazingira ambapo ujengaji wa mfumo wa vyama vingi unalazimu vingine kufa na vingine kuibuka, ingewezekana vyama vilivyoshiriki kwenye mchakato huu vionyeshe vinasimamia upande kwenye maswala ya msingi yanayohusu uendeshwaji wa chaguzi zetu, na mustakabali wa demokrasia ya vyama vingi nchini kwa ujumla wake.

Kwamba ikitokea kesho wananchi wakaiweka NCCR au Chauma kwenye nafasi ya uongozi wa kambi rasmi ya upinzani, wawe wamefanya hivyo kwa kuelewa misimamo ya NCCR au Chauma kuhusu nafasi ya upinzani kwenye siasa zetu.

Binafsi ningependa kujua rationale za vyama 12, ukiachilia chama tawala, kwenye uamuzi uliofikiwa na kamati ya maadili. Pengine kwa kutambua ugumu wa hili tamanio, kuna nafasi nyingine ya kuonyesha uhuru wa kamati hii, na msimamo wa vyama kuhusu uendeshwaji wa chaguzi zetu vis a vis maadili ya wagombea.

Tumeambiwa kuna malalamiko yamepelekwa na CHADEMA kuhusu conduct ya mgombea wa chama tawala kwa tume. Nafasi nzuri ya watanzania kuvipima hivi vyama na kuvisafisha kutoka tuhuma za mwenyekiti wa CHADEMA, ni kuvipa nafasi ya kupigia kura malalamiko haya.

Nadhani ni jukumu la tume kuweka mezani haya malalamiko kwa vyama kuyapigia kura. Ingependeza kujua wanasimama wapi kuhusu ahadi za viongozi wa serikali kwenye kampeni, matumizi ya lugha zisizo rasmi kwenye kampeni kwa mujibu wa sheria, kutofuata ratiba za kampeni, vitisho kwa wapiga kura kunyimwa maendeleo kwa kuchagua wawakilishi kutoka vyama pinzani, conduct ya vyombo vya habari wakati wa uchaguzi, n.k.

Tume haiwezi kujitenga na maamuzi yatokanayo na hii kamati kama haiwapi nafasi kukaa kufanya maamuzi kila inapobidi. Kamati na by extension, vyama, hawawezi kujisafisha na tuhuma za kutumika kama hawata demand ku exercise jukumu lao kwenye kila lalamiko linalotolewa.

Naamini watanzania wata benefit kwa kujua kwa uwazi kwamba, kwa mfano NRA au UPDP walisema wanakubaliana na matumizi ya mali za umma kama TBC, kwa manufaa ya chama kimoja wakati wa uchaguzi.
 
Unafikiri ni kwa nini hawataki kusikia chochote kuhusu suala la Katiba Mpya? Wanayajua madudu na udaifu wao ulipo. CCM ni chama cha hovyo na ambacho kimeshachokwa kitambo tu na Watanzania.

Kwa sasa kinatutawala tu kibabe kupitia Policcm, Necccm, nk.
 
Unachotakiwa kuhoji ni je,Lissu alidanganya? Kama alidanganya, je alitimiza wajibu wake kuomba radhi na kufuta kauli yake? Kama hajafanya hivyo, usipoteze muda kuandika insha ndefu isiyobadili chochote...
 
Unachotakiwa kuhoji ni je,Lissu alidanganya? Kama alidanganya, je alitimiza wajibu wake kuomba radhi na kufuta kauli yake? Kama hajafanya hivyo, usipoteze muda kuandika insha ndefu isiyobadili chochote...
Lissu alidanganya hakudanganya, tutajua kadri muda unavyozidi kwenda hadi siku ya uchaguzi na baada ya uchaguzi.

Lakini kwa mwenendo huu wa mchakato unavyoendeshwa na hii tume, inaonekana yuko sahihi kabisa. Hakuna tume hapa ni kamati kuu ya ccm ndio inaendesha uchaguzi. Nothing more.
 
Back
Top Bottom