Wazo: Katiba ya CCM ibadilishwe muundo wa Mwenyekiti wa Chama, bali Mwenyekiti atokane na Marais Wastaafu au Mawaziri Wakuu Wastaafu

mazaga one

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
768
500
Mimi ni Mwana CCM nimejaribu Kuwaza kwa mtazamo wangu na pia kumpunguzia Majukumu ya kichama Rais badala yake yeye awe tu Mjumbe anayeingia moja Kwa Moja kwenye maamuzi ya kichama.

Huu ni mtazamo wangu.Na muundo wake Rais Aliyepo madarakani ndiye ateue Majina ya hao Viongozi Wastaafu au wao wachukue Fomu halafu Wajumbe ndiyo wawapigie kura na Kumpata Mwenyekiti wa CCM Taifa.

Ni mtazamo Wakuu.
 
KingCobra95

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
1,551
2,000
kwA nchi kama hii,hyo ni hatari kubwa Sana,,,siku watawala wakinuniana ,,tutaletewa huo ugomvi sisi tuuamue
 
Kabugula

JF-Expert Member
May 25, 2021
1,716
2,000
Kwa mfumo uliopo ni sahihi Mkit awe nje ya kiti cha urais.

1.Wajumbe hawana Uhuru wakumshauri Mkiti kwakuwa anamakali yote.Dola/Mkiti,yeye ndio kila kitu.
Hivyo Uhuru wakuhoji haupo.

2.Wanachama wanaoongea nje ya vikao ni dhahiri ndani kuna unafiki wakukubali kutokukubaliana.

3.Katiba ya nchi itaheshimika
 
GIUSEPE

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
206
225
Ungeshauri katiba ya chama chako ibadilishwe kwanza,kuwe na demokrasia inayohubiriwa na chama chako,kama jina la chana lilivyo
 
Ezekiel Mbaga

JF-Expert Member
May 28, 2018
9,508
2,000
Kwa mawazo haya mtoa mada wewe sio ccm kama ulivyosema, mwanaccm wa kweli anajua umuhimu wa rais kuwa mwenyekiti wa chama.
 
dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
15,247
2,000
... endelea kuwaza ujinga. Siku yaja hamtakuwa na rais wala wm mstaafu! Zama zaja enyi wapumbavu; jifunzeni kusoma alama za nyakati. Maandishi ukutani ya wazi ewe mfalme juha!
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
23,722
2,000
..Mwalimu Nyerere alipostaafu Uraisi mwaka 1985 aliendelea kuwa Mwenyekiti wa CCM nadhani mpaka mwaka 1990.

..Na alipostaafu uenyekiti wa CCM na kumuachia kijiti Rais Ali Hassan Mwinyi, nakumbuka Mwalimu alimpendekeza Mzee Rashid Mfaume Kawawa kuwa makamu mwenyekiti wa chama.
 
Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
10,466
2,000
Kwa mfumo uliopo ni sahihi Mkit awe nje ya kiti cha urais.

1.Wajumbe hawana Uhuru wakumshauri Mkiti kwakuwa anamakali yote.Dola/Mkiti,yeye ndio kila kitu.
Hivyo Uhuru wakuhoji haupo.

2.Wanachama wanaoongea nje ya vikao ni dhahiri ndani kuna unafiki wakukubali kutokukubaliana.

3.Katiba ya nchi itaheshimika
Safi Sana mkuu
 
Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
10,466
2,000
Ushauri wako Ni mzuri sana. Lkn kwa kuwa unashauri mazwazwa, mambumbumbu yasiyojielewa hautapokelewa katu.

Twaweza walifanya utafiti wakajirridhisha kwamba wanaccm ni hamnazo.
 
Kabugula

JF-Expert Member
May 25, 2021
1,716
2,000
M/kiti taifa aajiriwe na kamati kuu kwa miaka 5/5
Ila atokane miongoni mwa wenyeviti wa mikoa
Awe na elimu
Msikivu nk
Marais/mawaziri wastaafu kupewa uenyekiti big no,kutakuwa na makundi ya mengi ndani ya chama.
Pia Mali za chama na mapato yawe wazi kwa wanachama.
Hela nyingi awamu 5 zimenunua wapinzani ili MTU mmoja aonekane amekubalika
 
Nziiri

JF-Expert Member
Jul 23, 2020
448
500
Mimi ni Mwana CCM nimejaribu Kuwaza kwa mtazamo wangu na pia kumpunguzia Majukumu ya kichama Rais badala yake yeye awe tu Mjumbe anayeingia moja Kwa Moja kwenye maamuzi ya kichama.

Huu ni mtazamo wangu.Na muundo wake Rais Aliyepo madarakani ndiye ateue Majina ya hao Viongozi Wastaafu au wao wachukue Fomu halafu Wajumbe ndiyo wawapigie kura na Kumpata Mwenyekiti wa CCM Taifa.

Ni mtazamo Wakuu.
Hujafikiria kuna siku mnaweza kutokuwa na rais mstaafu?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom