Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,475
- 39,991
1: Sehemu nyingi duniani viongozi wakuu wa vyama ndio huongoza vyama vyao kwenye uchaguzi mkuu walk wakiwa ndio wagombea Dhidi ya aliye madarakani ( incumbent). Zitto ndio kiongozi mkuu wa ACT-Wazalendo..yeye kutokusimama Dhidi ya JPM no kukwepa jukumu lake kuu. Hili no kweli kwa Mbowe na viongozi wengine wa upinzani.
2: Amejipambanua kama mkosoaji asiyekoma wa será, uongozi, mwelekeo na mtindo Wa uongozi Wa Rais Magufuli. Ukosoaji wake hautakuwa na maana kama yeye hatosimama kuonesha utofauti huo. Hawezi kumpa mwingine jukumu hilo.
3: Ana vitambulisho vya upinzani (opposition credentials). Miaka 15 tangu Buzwagi hadi leo hakuna shaka amejiwekea fungu lake na upinzani. Sasa iweje akwepe hitimisho la uamuzi huo.
4:Hawezi kumkwepa Magufuli kwenye uchaguzi huo na bado akabakia kuwa mkosoaji wa kuaminika. Tunaomuunga mkono Rais Magufuli yes #MagufuliTena2020 hatuoni ni nani anaweza kuonesha ushindi wa 2020 kuliko mtu ambaye anaonekana au amejionesha kama mpinzani mkuu. Kama Biden Dhidi ya Trump, Zitto asimkimbie Magufuli na kutafuta njia ya pembeni ya kupambana naye. Kama anaamini hoja zake zina ukweli na zinakubalika basi azipambanishe...Kama Send atagombea Zanzibar, Zitto alipaswa Kugombea Muungano.
5: Kuja kwa Membe ACT WAZALENDO kunapaswa kuwa kwa ajili ya kumuunga mkono Zitto na siyo kinyume chake. Hili nililisema ujio wa Lowassa CHADEMA 2015. Kama Membe amekuwa muumini wa upinzani nina uhakika hatosita kumuunga mkono Zitto.
Nje ya Hili tunashuhudia jinsi upinzani unajua kujiwekea mafuta kikaangoni...kwa mara nyingine
Go Magufuli Go