Uchaguzi 2020 Wazo Jadidi: Sababu 5 za kwanini Zitto alipaswa Kugombea dhidi ya Magufuli - Sipendi akwepe hili

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,988
1: Sehemu nyingi duniani viongozi wakuu wa vyama ndio huongoza vyama vyao kwenye uchaguzi mkuu walk wakiwa ndio wagombea Dhidi ya aliye madarakani ( incumbent). Zitto ndio kiongozi mkuu wa ACT-Wazalendo..yeye kutokusimama Dhidi ya JPM no kukwepa jukumu lake kuu. Hili no kweli kwa Mbowe na viongozi wengine wa upinzani.

2: Amejipambanua kama mkosoaji asiyekoma wa será, uongozi, mwelekeo na mtindo Wa uongozi Wa Rais Magufuli. Ukosoaji wake hautakuwa na maana kama yeye hatosimama kuonesha utofauti huo. Hawezi kumpa mwingine jukumu hilo.

3: Ana vitambulisho vya upinzani (opposition credentials). Miaka 15 tangu Buzwagi hadi leo hakuna shaka amejiwekea fungu lake na upinzani. Sasa iweje akwepe hitimisho la uamuzi huo.

4:Hawezi kumkwepa Magufuli kwenye uchaguzi huo na bado akabakia kuwa mkosoaji wa kuaminika. Tunaomuunga mkono Rais Magufuli yes #MagufuliTena2020 hatuoni ni nani anaweza kuonesha ushindi wa 2020 kuliko mtu ambaye anaonekana au amejionesha kama mpinzani mkuu. Kama Biden Dhidi ya Trump, Zitto asimkimbie Magufuli na kutafuta njia ya pembeni ya kupambana naye. Kama anaamini hoja zake zina ukweli na zinakubalika basi azipambanishe...Kama Send atagombea Zanzibar, Zitto alipaswa Kugombea Muungano.

5: Kuja kwa Membe ACT WAZALENDO kunapaswa kuwa kwa ajili ya kumuunga mkono Zitto na siyo kinyume chake. Hili nililisema ujio wa Lowassa CHADEMA 2015. Kama Membe amekuwa muumini wa upinzani nina uhakika hatosita kumuunga mkono Zitto.

Nje ya Hili tunashuhudia jinsi upinzani unajua kujiwekea mafuta kikaangoni...kwa mara nyingine

Go Magufuli Go
 
ZZK namkubali sana ingawa ndio wale wale ....basi sawa mnatuchezea akili zetu big time ...BM ni..version ya EL
 
Wewe unataka Magufuli ashinde sasa utatoa ushauri gani mzuri kwa upinzani wa kumfanya Magufuli ashindwe.

Aendelea kumpigia kampeni Yesu wa Lugola achana na upinzani.
 
Mwanakujiji...
Zitto si mjinga anazijua siasa za Tanzania vizuri sana.

Kweli Zitto hodari sana tena kupita kiasi lakini Membe ana sifa ya zaida ambayo Zitto anaijua hawezi kuipata hata akidhikiri uchi.

Mwanakijiji anajua Membe ni mseminari wa Kikatoliki anaenda kupambana na Mkatoliki wa kawaida Magufuli aliyefukuzwa seminary. Anajua huu mchezo ni mgumu sana mwaka huu kuliko ile ya 2015.
 
Usimlazimishe. Kila mtu ana strength zake na sio mtu akiwa kiongozi wa Chama basi ni haki yake kugombea kila kitu. Yeye kama anaona kuna watu wanafaa zaidi kugombea urais basi hana budi awaachie wafanye hivyo.

Mwenyekiti wa Democratic Party ni Tom Perez lakini mbona hagombei urais? Mwenyekiti wa Republican Party ni Ronna McDaniel lakini mbona hagombei urais?

Uamuzi wa nani asimame kugombea urais ni wa wanachama wa ACT Wazalendo, sio wa Zitto peke yake. Uamuzi huo sio wa kwako au wangu.

Wewe ungewekeza kwenye kumpigia debe mgombea wa chama chako. Mbona mlikuwa mnampigia debe Slaa awe mgombea urais na sio Mbowe kama kweli mnadhani kiongozi wa chama kuwa ni lazima agombee urais?

Kujifanya kuwa ati unatafuta mshindani ambae anaweza kutoa ushindani mzito kwa mgombea wako ni hypocrisy of the highest order.

Amandla...
 
Wewe mzee unazidi kuzeeka vibaya hakika fainali ni uzeeni....
Kumbuka nyuma ya membe kuna kikwete na mkapa
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Zitto lengo lake sio kushika dola,lengo lake ni kupiga "ruzuku".
Zitto ni "mpango na mkakati" wa kuua upinzani huku yeye akineemeka.
 
Naafikiana nawe ingawa naona umeshindwa kuangalia vitu viwili vikubwa,uwezekano wa kutoa challenge kubwa na umri wa ZZK.
Kwa hali ya sasa ZZK hawezi kutoa challenge kubwa kwa JPM lakini 2025 ataweza kuwa tishio kwani CCM itakuwa inatoa mtu mpya na kwa umri wa ZZK ni heri aweke akiba kwa ajili 2025.Kwa sasa JPM nahitaji mtu anayeweza kumwambia ukweli bila kumuogopa na naona ni Membe na Tundu Lissu tu!!
 
Mtu hagombei ilimradi anagombea

Mtu anagombea pale anapokuwa amejiandaa kisaikolojia kuwa anagombea, na pia awe amejipima kukubalika kwenye jamii.

Mtu hugombei ili ukawe msindikizaji!

Zitto ana potential ya kugombea urais lakini siyo katika uchaguzi huu
 
Ukiingia kwa mswahili atakuambia "karibu' ukikaa muda ukasikia anasema tena karibu ujue anakuambia ondoka! Watanzani ni waswahili ndio yaweza kuwa hapana na hapana ikawa ndio.
 
Zitto lengo lake sio kushika dola,lengo lake ni kupiga "ruzuku".
Zitto ni "mpango na mkakati" wa kuua upinzani huku yeye akineemeka.
Tusijidanganye kwa wakati huu eti kwamba upinzani watashinda kura ya urais... labda kutokee miujiza!
Kwa tume ipi? Katiba ipi? Vyombo dola gani? Upinzani wakifaulu kupata zaidi ya asilimia 45-50 ya wabunge Bunge litabadilika na huu utakuwa mwanzo mwema kuelekea kuondosha utawala wa chama kikongwe kilichochoka. Vinginevyo tudanganyane tu.
 
Back
Top Bottom