Wazo Huru: Serikali isiuze nyumba za Dar hata ikihamia Dodoma

S.N.Jilala

JF-Expert Member
Jan 26, 2012
540
507
Wazo Huru.

Rais Magufuli amesisitiza majengo ya Serikali yatapigwa mnada Serikali itakapohamia rasmi mkoani Dodoma. Amesema kuwa Dar es Salaam itabaki kuwa mji wa kibiashara, majengo makubwa ya serikali yatageuzwa kuwa hoteli kwa ajili ya wafanyabiashara watakaokuja Dar Es Salaam.
Siku zote najua majengo yale ambayo wizara zipo yapo chini ya Shirika la Nyumba Tanzania (National Housing Corporation).

Lakini niende moja kwa moja kwenye hoja, yawe chini ya Shirika la Nyumba Tanzania au la, kuyapiga mnada majengo yale Mimi naona si sahihi kabisa. Wakati wa Mkapa tuliumizwa sana maana majengo mengi yaliuzwa kwa bei za chini na kusema kweli Mimi si Mchumi lakini wananchi mpaka leo wanasema tulifanya makosa makubwa. Na baadhi ya viongozi nao walisisitiza kuwa tulifanya makosa sana. Je, kwa nini majengo yale yasiwe chini ya National Housing Corporation na kama mtu anataka kuwekeza Hotel au Biashara yoyote apangishiwe?. Ni Mimi naona ni faida kubwa sana itapatikana serikalini kuliko kuuza Jengo. Kwa mfano, umeuza jengo kwa 2 au 5 Bilioni nina uhakika ndani ya miaka kadhaa faida hiyo itakuwa imerudi na watafanya biashara yao maisha pamoja na majengo kuwa yao. Ni afadhari kupata faida kidogokidogo lakini mkawa na umiliki wa muda wote.

Kama serikali itashikilia msimamo, ni vyema ikafanya jitihada kubwa za kutadhimini FAIDA na HASARA za kuuza majengo yaliyojengwa kwa kodi za wananchi. Hata kama watayauza watadhimini kwa kina ni nini wanaenda kukifanya wakishapata hizo hela. Je, kujenga nyumba Dodoma kwa ajili ya Wizara?. Kama ni hivyo, serikali ni vyema ikatenga bajeti kila mwaka ikawa inahamia Dodoma taratibu taratibu kama ambavyo imeanza, Mwisho wa siku, kizazi kinachokuja kitatushangaa kwa maamuzi haya kama wakati huu tunavyoshangaa yalivyouza nyumba za serikali kwa bei ambayo inasadikiwa kuwa faida ilikuwa ndogo.

Kama wamefanya uchambuzi wa kutosha na wakaona kuuza Majengo ya serikali kutapatikana faida kwenye serikali yetu basi wafanye kwa mustakabali wa Taifa letu.

image.jpg



.
 
Back
Top Bottom