Wazo Huru: CCM na Serikali yako mnakwama wapi?

Rasterman

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
33,905
44,011
Asalam aleykum wapendwa wana siasa na wajenzi wa uchumi wa nchi yetu Tanzania. Hongereni kwa Waislam tunaoendelea na ibada yetu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani huku tukikabiliwa na janga kubwa la Mlipuko wa Covid-19. In sha allah mwenyezi Mungu atatufanyie wepesi katika hili.

Hoja yangu ni fupi tu lakini tuifikiri kwa pamoja. Nashindwa kuelewa namna serikali inavyopambana dhidi ya ugonjwa huu wa corona. Corona iko dunia nzima hivyo hakuna namna ya kulia lia na kutaka huruma bila kuchukua hatua madhubuti. Ni dhahiri corona inakuja na madhara makubwa kwa binadamu ikiwemo vifo Maradhi na na mdororo wa uchumi. Wajibu wa serikali ya ccm ni kukabiliana na madhara hayo yasiyokwepeka.

Cha kushangaza CCM na serikali yake inataka madhara haya yabebwe na wananchi na sio nchi.

Mambo yanapokuwa mazuri wapenzi na wanufaika wa mfumo wa kichoyo wa CCM na serikami hutamba na kusema kwa majivuno hivi.

1. Sisi ndio wenye nchi na hakuna mtu wa kuleta fyokofyoko.

2. Sisi ndio wenye serikali tunaweza kumfanya mtu kitu chochote na tunaweza ku-organize resources zetu tukakupata mahali popote na tukakufanya chochote.

2. Sisi ndio wenye madaraka bajeti zetu hatuwezi kuwapangia miradi ya maendeleo majimbo ya wapinzani (as if wao sio wananchi).

4. Serikali yetu inakusanya mapato kwa kiasi cha kuvuka malengo kila mwezi.

5. Tuna hifadhi ya pesa BoT na tunaweza kulisha na kutunza nchi miezi 6 mbele.

6. Kupora watuhumiwa pesa zao wakiwa mahabusu (yaani kudai Ransom) ili waachiwe kwenye kesi zao za kuunga unga na kubambikiza.

8. Kutelekeza wananchi wanapopatwa na majanga na kuambiwa maneno ya kebehi ya kubeza kuwa wametaka wenyewe. Waliambiwa wahame mabondeni wakakaidi.

9. Serikali ya CCM kutekeleza kwa haraka mikakati na miradi ya kupoteza na kutapanya fedha za umma mathalani kwa kununua wabunge. Tume ya uchaguzi kutoyumba kifedha hata siku moja inapotokea jimbo liko wazi kwa mbunge kuunga mkono juhudi. Fedha hupatikana haraka sana na mipango yao hukamilika 100%. Pamoja na kunua wabunge wa upinzani kwa fedha nyingi na ahadi kedekede.

10. Rushwa, ufisadi kukithiri ndani ya serikali hii ya awamu ya tano kwa wale tu" the annointed" hawaguswi wala kuhojiwa as long as they pose no threat to the top figure.

11. Serikali inatoza kodi almost kwa kila mwananchi hadi wamachinga wanachangia elfu 20 kwa mwaka. Wafanyakazi na wakulima wanakatwa kodi kwa mishahara yao. Na kila manunuzi wanayofanya kodi inalipwa. Hizi ni fedha nyingi mno. Ni wakati sasa zisaidie wananchi.

CCM na serikali yenu mnakwama wapi?

Mkiwa na sifa zote hapo juu mkijigamba kuwa mnaweza na kuwa serikali ni yenu na anayeleta fyokofyoo mnamnyosha. Saaa inakuwaje Janga la Covid-19 mnatafuta huruma yetu, eti tuchangie fedha za kupambana na corona? Mmetuacha na hali.mbaya kiuchumi. Ajira hakuna na zilizopo kidichu tutoe pesa kutoka wapi.

Leo mnatafuta huruma na kuungwa mkono kwetu sisi tunaoitwa wasaliti?

Hatuchangi hata sentano.

Covid-19 ingekuwa inachagua ingeanza na nyie. Shukuruni sana kwakuwa haina mwenyewe. Kwa hili CCM na serikali bebeni mzigo mnaweza. Msitafute huruma wakati wa majanga. Mkiwa na starehe tunaona mkila bata huko maulaya Marekani na kwingineko. Na hili nalo ni la kwenu.

CCM na serikali yenu mnakwama wapi?
 
Serikali haina hela ndio maana hawataki mambo ya lockdown ili ikusanye kodi.jiwe kauliyake kila akionekana anasema pigeni kazi ili kodi ikusanywe bila ya hivyo basi anaangukia pua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwenye fedha hajifichi,ungeona mipango na utekelezaji.Wangenunua hats vifaa vya uchunguzi,kinga kwa watoa huduma za afya na tiba zikiwemo ventilators walau kila Kituo cha Afya.

Hawana fedha maana vipaumbele vyao wanavifahamu wenyewe.Wananchi wanabaki watazamaji-COVID ndiyo imewaumbua.
Labda pesa ipo ila vipaumbele vya viongozi na raia vimetofautiana.
 
Mwenye fedha hajifichi,ungeona mipango na utekelezaji.Wangenunua hats vifaa vya uchunguzi,kinga kwa watoa huduma za afya na tiba zikiwemo ventilators walau kila Kituo cha Afya.

Hawana fedha maana vipaumbele vyao wanavifahamu wenyewe.Wananchi wanabaki watazamaji-COVID ndiyo imewaumbua.
Wamekwama kichizi yaani hawana pakushika . Kwa mabeberu wameshanyea wanapolala hawawezi kwenda.
 
Asalam aleykum wapendwa wana siasa na wajenzi wa uchumi wa nchi yetu Tanzania. Hongereni kwa Waislam tunaoendelea na ibada yetu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani huku tukikabiliwa na janga kubwa la Mlipuko wa Covid-19. In sha allah mwenyezi Mungu atatufanyie wepesi katika hili.

Hoja yangu ni fupi tu lakini tuifikiri kwa pamoja. Nashindwa kuelewa namna serikali inavyopambana dhidi ya ugonjwa huu wa corona. Corona iko dunia nzima hivyo hakuna namna ya kulia lia na kutaka huruma bila kuchukua hatua madhubuti. Ni dhahiri corona inakuja na madhara makubwa kwa binadamu ikiwemo vifo Maradhi na na mdororo wa uchumi. Wajibu wa serikali ya ccm ni kukabiliana na madhara hayo yasiyokwepeka.

Cha kushangaza CCM na serikali yake inataka madhara haya yabebwe na wananchi na sio nchi.

Mambo yanapokuwa mazuri wapenzi na wanufaika wa mfumo wa kichoyo wa CCM na serikami hutamba na kusema kwa majivuno hivi.

1. Sisi ndio wenye nchi na hakuna mtu wa kuleta fyokofyoko.

2. Sisi ndio wenye serikali tunaweza kumfanya mtu kitu chochote na tunaweza ku-organize resources zetu tukakupata mahali popote na tukakufanya chochote.

2. Sisi ndio wenye madaraka bajeti zetu hatuwezi kuwapangia miradi ya maendeleo majimbo ya wapinzani (as if wao sio wananchi).

4. Serikali yetu inakusanya mapato kwa kiasi cha kuvuka malengo kila mwezi.

5. Tuna hifadhi ya pesa BoT na tunaweza kulisha na kutunza nchi miezi 6 mbele.

6. Kupora watuhumiwa pesa zao wakiwa mahabusu (yaani kudai Ransom) ili waachiwe kwenye kesi zao za kuunga unga na kubambikiza.

8. Kutelekeza wananchi wanapopatwa na majanga na kuambiwa maneno ya kebehi ya kubeza kuwa wametaka wenyewe. Waliambiwa wahame mabondeni wakakaidi.

9. Serikali ya CCM kutekeleza kwa haraka mikakati na miradi ya kupoteza na kutapanya fedha za umma mathalani kwa kununua wabunge. Tume ya uchaguzi kutoyumba kifedha hata siku moja inapotokea jimbo liko wazi kwa mbunge kuunga mkono juhudi. Fedha hupatikana haraka sana na mipango yao hukamilika 100%. Pamoja na kunua wabunge wa upinzani kwa fedha nyingi na ahadi kedekede.

10. Rushwa, ufisadi kukithiri ndani ya serikali hii ya awamu ya tano kwa wale tu" the annointed" hawaguswi wala kuhojiwa as long as they pose no threat to the top figure.

11. Serikali inatoza kodi almost kwa kila mwananchi hadi wamachinga wanachangia elfu 20 kwa mwaka. Wafanyakazi na wakulima wanakatwa kodi kwa mishahara yao. Na kila manunuzi wanayofanya kodi inalipwa. Hizi ni fedha nyingi mno. Ni wakati sasa zisaidie wananchi.

CCM na serikali yenu mnakwama wapi?

Mkiwa na sifa zote hapo juu mkijigamba kuwa mnaweza na kuwa serikali ni yenu na anayeleta fyokofyoo mnamnyosha. Saaa inakuwaje Janga la Covid-19 mnatafuta huruma yetu, eti tuchangie fedha za kupambana na corona? Mmetuacha na hali.mbaya kiuchumi. Ajira hakuna na zilizopo kidichu tutoe pesa kutoka wapi.

Leo mnatafuta huruma na kuungwa mkono kwetu sisi tunaoitwa wasaliti?

Hatuchangi hata sentano.

Covid-19 ingekuwa inachagua ingeanza na nyie. Shukuruni sana kwakuwa haina mwenyewe. Kwa hili CCM na serikali bebeni mzigo mnaweza. Msitafute huruma wakati wa majanga. Mkiwa na starehe tunaona mkila bata huko maulaya Marekani na kwingineko. Na hili nalo ni la kwenu.

CCM na serikali yenu mnakwama wapi?
Tukifanya makosa kuirudisha serikali hii madarakani tutajuta mno kwa awamu ya pili.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom