Wazo: Dodoma ijengwe ziwa la kutengeneza ili watu waburudike na Serikali kuongeza mapato

Akili za mwisho wa mwaka hizi..naona unataka tufanye Kama Dubai..ila nimekusifu angalau umekumbuka kwamba tufanye kazi na tule Bata!
hakuna bata hapa ila kuna kuongeza mapato kupitia utalii wa ndani. inawezekana kuifanya dodoma dubai ya Tanzania
 
Nini kifanyike?
Serikali inaweza kuchimba mfereji mkubwa kama ule wa suez ili kurahisha kupata maji na kuvutwa kutokea bahari ya hindi dar es salaam na huo mfereji ujimbwe mpaka Dodoma na ukifika Dodoma serikali itengeneze bwawa kubwa sana mfano wa ziwa ili maji yaishie hapo. Pia serikali ijimbe mfereji mwingine kutokea Dodoma mpaka kwenye chanzo kingine cha maji ili tusiweze kuweka kusanyiko kubwa la maji kwenye hilo bwawa ama ziwa Dodoma.
Hahahaaa just hahaaa .We mzee wa kuchimba mifereji unanitia mashaka. Mi nakushauri usome kwanza hata ile physics ya form I .eeehee huo mfereji wa dodoma hv umesema mnaupeleka wapi vile? Hahahaaa.
 
Ukiwa ccm hata vile vitu vya kipumbavu kabisa unahisi vinawezekana na utatunisha mishipa kuvitetea. Wee ni mjinga na msomi uchwara.
 
pia inaweza kurahisisha kilimo cha umwagiliaji kama maji hayo yatatibiwa na serikali kuanzisha kilimo kikubwa mno.

Utalimaje kwenye eneo la mapumziko au kipaumbele chako ni nini kati ya kupumzika na kilimo

mawazo yangu tu
 
Nina wazo la kushirikiana nanyi ili kuifanya Dodoma kuwa na muonekane kama ulivyo wa jiji la dar es salaam kwa maana iwe na mandhari nzuri za kuvutia kama beach kwa kuwa na kitu kama mfano wa ziwa ama bahari ya kutengeneza ili watu waburudike na serikali iweze kujipatia mapato kupitia sehemu za kujiburudisha na pia itumike kama njia ya kukuza utalii wetu wa ndani

Nimekaa na kutafakari na kuona kuwa kama serikali itaamua basi wazo hili linaweza kufanikiwa.

Nini kifanyike?
Serikali inaweza kuchimba mfereji mkubwa kama ule wa suez ili kurahisha kupata maji na kuvutwa kutokea bahari ya hindi dar es salaam na huo mfereji ujimbwe mpaka Dodoma na ukifika Dodoma serikali itengeneze bwawa kubwa sana mfano wa ziwa ili maji yaishie hapo. Pia serikali ijimbe mfereji mwingine kutokea Dodoma mpaka kwenye chanzo kingine cha maji ili tusiweze kuweka kusanyiko kubwa la maji kwenye hilo bwawa ama ziwa Dodoma.

Pemnbezoni mwa ziwa hilo kuwekwe beach ambazo zitakuwa zinatumika kuingizia kipato nchi kwa sababu ya utalii wa ndani kuongezeka na pia utalii wa nje utaongezeka.

Kwa kuwa mfereji huo utakuwa ni mkubwa sana kwa hiyo unaweza kupitisha hata meli kubwa sana hivyo kurahisisha usafirishaji wa mizigo na hivyo tanzania kuwa kitovu cha usafirishaji kwa nchi za afrika mashariki na kati na hivyo kuongeza mapato.

Wazo hili limekuja baada ya kuona kuwa Dodoma utakuwa makao makuu ya serikali lakini watu watakosa viburudisho vya msingi kama beach za kuogelea na vitu vingine vya kuweka akili sawa.

Na pia itatumika kama njia ya usalama wa kumkinga rais wetu pale nchi inapotokea machafuko na hakuna uwezekano wa kuondoka kwa njia ya anga ama barabara akiwa Dodoma kwa sababu atasafirishwa kwa kutumia nyambizi ndogo ndani ya maji na akifika dare s salaam atatumia usafiri wa meli kutorokea nchi nyingine.

Hili linawezekana na haijalishi ni muda gani ujenzi utafanyika kwa sababu ili kujenga mfereji wa suez ilichukua takribani miaka 10.

naamini serikali ikipeleka wazo hili kwa wataalamu wote wanaohusika watakuja na majibu mazuri zaidi.

karlo Mwilapwa

Jiwe kasena jana Tanzania itakuwa kama Ulaya. Bila shaka wazo lako atalichukua maana kiakili hamjatofautiana.
 
That's nonsense. Kuna vitu muhimu vinatakiwa vifanywe kuliko hizo anasa. Miaka karibu 60 ya uhuru kilimo chetu bado ni kile kile cha akina Ibrahim na babu yake Nuhu wewe unawaza "Luxury". Very hopeless.
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom