Wazo: Dodoma ijengwe ziwa la kutengeneza ili watu waburudike na Serikali kuongeza mapato

FPT

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
1,201
1,839
Nina wazo la kushirikiana nanyi ili kuifanya Dodoma kuwa na muonekane kama ulivyo wa jiji la dar es salaam kwa maana iwe na mandhari nzuri za kuvutia kama beach kwa kuwa na kitu kama mfano wa ziwa ama bahari ya kutengeneza ili watu waburudike na serikali iweze kujipatia mapato kupitia sehemu za kujiburudisha na pia itumike kama njia ya kukuza utalii wetu wa ndani

Nimekaa na kutafakari na kuona kuwa kama serikali itaamua basi wazo hili linaweza kufanikiwa.

Nini kifanyike?
Serikali inaweza kuchimba mfereji mkubwa kama ule wa suez ili kurahisha kupata maji na kuvutwa kutokea bahari ya hindi dar es salaam na huo mfereji ujimbwe mpaka Dodoma na ukifika Dodoma serikali itengeneze bwawa kubwa sana mfano wa ziwa ili maji yaishie hapo. Pia serikali ijimbe mfereji mwingine kutokea Dodoma mpaka kwenye chanzo kingine cha maji ili tusiweze kuweka kusanyiko kubwa la maji kwenye hilo bwawa ama ziwa Dodoma.

Pemnbezoni mwa ziwa hilo kuwekwe beach ambazo zitakuwa zinatumika kuingizia kipato nchi kwa sababu ya utalii wa ndani kuongezeka na pia utalii wa nje utaongezeka.

Kwa kuwa mfereji huo utakuwa ni mkubwa sana kwa hiyo unaweza kupitisha hata meli kubwa sana hivyo kurahisisha usafirishaji wa mizigo na hivyo tanzania kuwa kitovu cha usafirishaji kwa nchi za afrika mashariki na kati na hivyo kuongeza mapato.

Wazo hili limekuja baada ya kuona kuwa Dodoma utakuwa makao makuu ya serikali lakini watu watakosa viburudisho vya msingi kama beach za kuogelea na vitu vingine vya kuweka akili sawa.

Na pia itatumika kama njia ya usalama wa kumkinga rais wetu pale nchi inapotokea machafuko na hakuna uwezekano wa kuondoka kwa njia ya anga ama barabara akiwa Dodoma kwa sababu atasafirishwa kwa kutumia nyambizi ndogo ndani ya maji na akifika dare s salaam atatumia usafiri wa meli kutorokea nchi nyingine.

Hili linawezekana na haijalishi ni muda gani ujenzi utafanyika kwa sababu ili kujenga mfereji wa suez ilichukua takribani miaka 10.

naamini serikali ikipeleka wazo hili kwa wataalamu wote wanaohusika watakuja na majibu mazuri zaidi.

karlo Mwilapwa
 
kama hatuna pesa sasa hivi , ni heri likatengwa eneo mapema , liwe kama km 20 urefu na upana km20 ama km za mraba 400
 
pia inaweza kurahisisha kilimo cha umwagiliaji kama maji hayo yatatibiwa na serikali kuanzisha kilimo kikubwa mno.

mawazo yangu tu
 
Kujenga mfereji kama Suez ni hela ndefu,ila idea ya artificial lake itakuwa simple maji yakivutwa kwa bomba kubwa kutoka udzungwa hadi Dodoma halafu kunakuwa na exit pipe ambayo itaelekeza hayo maji kwenye irrigation schemes.
This can't the whole year.
 
mkuu maji ya bahari ni muhimu , wengine wanasema yanaondoa nuksi. tusiwanyime wagogo pia haja ya kuondoa nuksi na mikosi
Mradi wa kutoa maji ya bahari pwani hadi Dodoma ili watu waogelee, du, dunia nzima itatucheka. Hapo ndio kila mtu ataju tunaongozwa na vichaa, sio utani. Na ni baada ya international airport Chato?
 
mkuu maji ya bahari ni muhimu , wengine wanasema yanaondoa nuksi. tusiwanyime wagogo pia haja ya kuondoa nuksi na mikosi
Wagogo wanakula VIWAVI,nasikia vinasaidia sana kuondoa Mikosi mkuu.
 
Dodoma maji ya shida?? Mbona wanasema maji ni mengi sana chini ndo haitatokea kuwe na Jengo la grorofa zaidi ya 20
Labda miundombinu ya visima vyakuvuta maji ndo shida
 
Back
Top Bottom