Wazo deni la taifa yaani (debt ceiling) liwekwe kwenye katiba

maskin

Member
Oct 27, 2010
78
27
Jamani nahisi kuna umuhimu wa kuweka deni la taifa kwenye katiba kwa twaweza kutumia GDP kupiga hesabu ni kiasi gani kiwa cha mwisho kukopa kutokana nauwezo wetu kama nchi ,kuwe na exemption tu kama kukiwa na vita au national disaster bila hivyo next generation watapelekwa utumwani kulipia madeni yetu ,hilo ni wazo tu jamani tujadili kama ni possible
 
Hivi bajeti ya Tanzania kwa USD ni kiasi gani?

Kati ya hiyo ni % ngapi zinatoka kwa nchi wahisani?

Kati ya hiyo ni % ngapi ni budget support?

Je serikali ya China wanachangia kiasi gani kwenye hilo fungu la pesa toka nchi wahisani?

Je serikali sasa hivi inadaiwa kiasi gani na nchi za nje (external bilateral debt)

Nchi ipi inaongoa kwa kuipatia tanzania grant au loan (in terms of USD)

Je so far serikali imetoa sovereign guarantee kwa miradi mingapi tukipata data za miaka 2 iliyopita tutaelewa) na tukipata data in terms of USD itakuwa boara zaidi

Na katika hiyo sovereign guarantee wamepewa nchi au mabenki yepi (mliokuwa mnafuatilia ya akiana shose sinare na kitilya nadhani mnaelewa naelekea wapi)

Je tunayo debt limit ya kuendelea kukopa? na kama ipi hiyo limit inawekwa na nani?

Je kutokana na hii miradi mingi ya infrastructure na energy ambayo mheshimiwa magufuli anataka ifanyike kuna uwezekano kweli wa kupata sovereign guarantee kama tumefikia debt limit?

Je hiyo SG inatolewa kwa miradi ipi?

Na imeathiri vipi bajeti yetu ya 2016/2017?

Ikiwezekana naomba mumlete Zitto aje kutusaidia maana kuna mambo naona hayajawekwa wazi kwenye tovuti ya wizara ya fedha
 
Serikali yetu kwanza haina nia ya kulipa madeni..hata kwwnye bajeti deni ka Taifa halijaguswa.
 
Jamani nahisi kuna umuhimu wa kuweka deni la taifa kwenye katiba kwa twaweza kutumia GDP kupiga hesabu ni kiasi gani kiwa cha mwisho kukopa kutokana nauwezo wetu kama nchi ,kuwe na exemption tu kama kukiwa na vita au national disaster bila hivyo next generation watapelekwa utumwani kulipia madeni yetu ,hilo ni wazo tu jamani tujadili kama ni possible

Hakuna sababu ya jambo hili kwasababu deni la taifa halilipiki. Kama ukufuatilia huko nyuma ilikuwa wazi kuwa hatutafanikiwa kulipa hayo madeni hata siku moja. Vile vile siyo kila deni huwa linalipwa. Madeni mengine yanabaki madeni milele.
 
Deni. Na Leo tumepewa trilioni16, na bado tunataka madaraja na barabara. Tril16 Ni Reli, afadhali itajilipa
 
Back
Top Bottom