Wazo chokozi: Serikali ya CCM inawatesa Watanzania kwa ukweli huu

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,556
29,646
Uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 uligubikwa na sintofahamu kubwa hadi kupelekea mchakato mzima kugubikwa na ukengemaji wa kuwaengua wagombea wa vyama mbadala na kuwapitisha wagombea wa CCM kwa nguvu ya kupita bila kupingwa

Mwaka wa Uchaguzi Mkuu 2020 ndiyo ulikuwa kilele cha janga la kidemokrasia nchini kwa wizi mkubwa wa kura uliotukuka uliofanywa na CCM kwa kushirikiana na dola hivyo kuwapitisha wagombea wa CCM kwa mtutu kupitia sanduku la kura.

Ingawa kura zilipigwa lakini ukweli ni kwamba idadi kubwa ya wapigakura walipiga kura against CCM hivyo endapo NEC ingelikuwa ya wazalendo, tungeshughdia majimbo mengi kutwaliwa na upinzani. Lakini kikubwa ni kuwa hata kura za urais angepatikana mshindi kwa ushindi mwembamba sana

Namba moja anaelewa ukweli huu.
CCM inaujua ukweli huu
Dola inaujua ukweli huu

Je hisia na mawazo kuwa muunganiko wa dola na CCM wameamua kuwatesa Watanzania kwa kuwatwisha kongwa zito la ugumu wa maisha kuanzia nyanja zote za mahitaji ya msingi hadi ya kawaida yanakwepeka?

Upo uwezekano mkubwa raia wanateseka kwa sababu CCM imetambua haipendwi tena hivyo wanabwetteka bila kutafakari njia za kuzuia athari za mikwamo ya kiuchumi. Na inawezekana upandaji wa gharama za maisha na tozo kandamizi ni matokeo ya kuwawajibisha wapigakura walioiadhibu CCM kisaikolojia kwenye sanduku la Kura.

Ni zaidi ya miezi 6 sasa wananchi wanalalamikia wizi kupitia ununuzi wa bando za internet na wahusika wanatoa kauli za vitisho huku wakiharakisha kuweka sheria za kuwaadhibu wanaoisema vibaya serikali.

Demokrasia inakandamizwa huku wanasiasa wa upinzani wakilamba peremende inayoitwa MARIDHIANO baina yao na CCM bila kujali madhila wanayopitia wananchi

Je tuamini kwamba tuna viongozi au wakandamizi?

20220813_002214.jpg
 
View attachment 2403791
WANAOTESEKA NI WAPINZANI WA KWELI AMBAO NI CHADEMA wale wengine Wanakula Keki ya TAIFA
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom