Wazo: CCM ivunjwe na mali zake zitaifishwe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazo: CCM ivunjwe na mali zake zitaifishwe!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Japhari Shabani (RIP), Apr 18, 2011.

 1. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #1
  Apr 18, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Badala ya huu usanii unaoendelea wa CCM kujivua gamba,nafiri kitu ambacho kingefanyika havi sasa ni kuvunjwa chama hiki na mali zake kutaifishwa kama ilivyofanyika Misri.Nasema haya kwa sababu zifuatazo:

  1. CCM kabla ya mfumo wa vyama vingi kilikua chama naweza kusema cha Watanzania wote na kwa namna moja au nyingine watanzania wote walichangia kwa chama hiki kwa hiyali au kwa kulazimishwa. Tulilipa ada michango, kushiriki katika ujenzi wa miradi mbalimbali vikiwemo viwanja,majengo n.k. Baada ya mfumo wa vyama vingi chama tawala kilirithi na kinaendelea kumiliki mali hizi hii haikua nasio halali.

  2. Viongozi wa chama hiki tawala CCM kimekua ukiwakumbatia kuwalinda na kuendeleza UFISADI katika ngazi zote za utawala serekalini. Kuiba na kupora rasiilimali zetu bila huruma na kutuwacha walalahoi katika maisha magumu wakati wao wakijilimbikizia mali na famila zao. Ni hasara kiasi gani taifa letu limezipata kutokana na maamuzi ya chama hiki na serikali yake?

  Baada ya madudu yote haya wanaibuka na kusema "TUMEJIVUA MAGAMBA"Je hii inatosha?Madhala yaliyosababishwa na magamba haya kwa taifa yatalipwa na nani?Ni hatua gani za kisheria zitachukuliwa kwa magamba haya (Asilimia 70) ya uongozi pamoja na mwenyekiti wa chama hiki ni mafisadi au wanalinda ufisadi. Wamekubali kujivua magamba ikiwa na maana ya kua katika chama hiki kulikua na ufisadi na chama kibebe gharama zote zilizotokana na ufisadi.

  KIVUNJWE NA MALI ZITAIFISHWE NA WAHUSIKA WAFIKISHWE MBELE YA VYOMBO VYA SHERIA


  MUNGU IBARIKI TANZANIA.
   
 2. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 5,909
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Thanks!!
   
 3. saragossa

  saragossa JF-Expert Member

  #3
  Apr 18, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 2,130
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Thanks!!! Naona sasa watanzania tunafunguka macho....ila naomba nikusahihishe kidogo. Sio kivunjwe, kiuliwe kabisa tukizike tukisahau na mali zake ziwe urithi wa watanzania, wale tu wenye uchungu na nchi yao!!!
   
 4. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #4
  Apr 18, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,339
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Hiki Chama ndicho kilichotuingiza kwenye umaskini na kuwaruhusu wageni kupora ardhi yetu kwa jina la uwekezaji, nakuunga hoja yako ya kuwa hiki chama kifutwe haraka sana kabla hatujaliazimishwa kufutwa
   
 5. J

  JokaKuu Platinum Member

  #5
  Apr 18, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 11,572
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  ..mali za TANU/CCM baada ya kufutwa kwa mfumo wa vyama vingi, na haswa baada ya kutangazwa kwa azimio la CHAMA KUSHIKA HATAMU, zinapaswa kutaifishwa na serikali.
   
 6. n

  ng'wanamakamya Member

  #6
  Apr 18, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 35
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ni kweli. Watanzania wote tulishiriki kwa CCM kuwa na rasilimali ilizonazo sasa. Bora ziwe mali za serikali ili CCM nao wachangiwe na wanachama wao ili waweze kumiliki mali zao kama vilivyo vyama vingine.
   
 7. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #7
  Apr 18, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,317
  Likes Received: 4,722
  Trophy Points: 280
  ni kweli, tukifanya hivi mapema tutanufaika zaidi kihistoria. Kwa maana tukichelewa sana (maana hili ni lazima litokee) itakuwa kama zile nchi ziliziokuja kupata uhuru wake miaka ya 1980 ambapo zililazimika kusaidiwa na wenzao. Unaona waliowahi kupata uhuru kama Ghana wamepitia tayari baadhi ya 'epoch' za historia na sasa wanaanza angalau kujua mlango wa kutokea kwenye dhiki ulipo.

  Pia hatutakuwa wa kwanza maana Tunisia wamefanya hivyo tayari na Misri wanaendelea na mchakato (wa kufuta chama).


  Tukumbuke "this is the wind of change" kwa hiyo na CCM wenye upeo na mapenzi ya nchi hii watusaidie pia. Utaratibu wa umiliki uko wazi kulingana na report ya Justice Nyarali na kama yanahitajika marekebisho yanaweza kufanyika (lakini sio bunge hili la sasa!!!!)
   
 8. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #8
  Apr 18, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 15,643
  Likes Received: 2,558
  Trophy Points: 280
  Kila siku naliwaza hili sasa watz tuamke! Chama hiki ni cha wezi na kimehusika kwa kila aina ya ufisadi ndani ya tz matharani Kagoda! Kikwete aliingia kupitia ufisadi hivyo urais wake ni batili! Napendekeza wahusika wote wafikishwe AICC au kwa Ocambo baada ya chama kufilisiwa na kufutwa! Kama chama cha mubarak kimefutwa je hiki cha wauwaji na mafisadi?
   
 9. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #9
  Apr 18, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  thanks for the good thread....kwa mfano, kwanini chama kina viwanja vikubwa vya michezo na si idara za michezo na utamaduni??????????wavirudishe tu mapema kwa heshima ili visifilisiwe tukikamata nchi!
   
 10. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #10
  Apr 18, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,317
  Likes Received: 4,722
  Trophy Points: 280
  kuna kitu kibaya zaidi watakifanya endapo haitavunjwa nacho ni kuharibu urith wa taifa kwa kisingizio kuwa ni mari zao. Mfani ni jengo la kihistoria la moshi na hata makao makuu ya vijana ambapo sasa zinajengwa appartments kupitia mradi wa tajiri mmoja badala ya umma wa watz. kikubwa mno ni kuondoa urithi aghali kuliko wote - amani
   
 11. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #11
  Apr 18, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kweli nakubaliana na wewe ni ukweli usiopingika ya kwamba CCM inaelekea ukingoni. Zisipofanyika jitihada za haraka kutaifisha mali za chama hiki kuzirudisha kwa wananchi, chama hiki kikivunjika mali zake watagawana wajanja wachache ambao mbali ya kutunyonya kwa muda mrefu bado watabaki au kutuibia jasho la mwisho la walalahoi viwanja vya michezo, majengo na miradi mbalimbali iliyojengwa kwa jasho la wananchi wote.

  Hii ilitokea Urusi baada ya kusambaratika chama cha kikomunisiti mafisadi walitokomea na mali zote majengo, dhahabu, viwanda, rasilimali, vyombo vya habari na kila kitu walichoweza na kuwaacha walalahoi solemba.

  CCM IMEISHA ANZA KUSAMBARATIKA KATIKA MISUGUANO YA NDANI YA CHAMA CHAO YA WAO KWA WAO ITAPELEKEA KUPOTEA KWA DOCUMENTS MUHIMU AMBAPO BAADAE ITAKUA VIGUMU KUFUATILIA MALI ZIKO WAPI NA NANI KACHUKUA

  HIMAHIMA ILI LIFANYIKE HARAKA MUNGU IBARIKI TANZANIA.
   
 12. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #12
  Nov 5, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 7,496
  Likes Received: 353
  Trophy Points: 180
  kwa mda mrefu sasa tumewaachia ccm wakijitajirisha na mali ambayo ilikuwa ni ya umma wa watanzania.mali hizi ni pamoja na viwanja na majengo ambayo ccm inajidai nayo hivi sasa.
  Naamini chadema ikiingia madarakani 2015 itasimamia urejeshaji wa mali hizi kwa umma wa watanzania.
   
 13. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #13
  Nov 5, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 7,496
  Likes Received: 353
  Trophy Points: 180
  napendekeza tuanze na uwanja wa shekh amri abeid!
   
 14. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #14
  Nov 5, 2012
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,597
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Mmezidi kulia lia! Hebu kueni!
   
 15. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #15
  Nov 5, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,188
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 145
  Ccm ni tanzania na tanzania ni ccm haiwezekaniii bila ya ccm bado sanaaa mlishindwa kuitoa 1995 ndo bac tena imekula kwenu big tyme.
   
 16. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #16
  Nov 5, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,830
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  .itakuwa dream comes true
   
 17. T

  TEMILUGODA JF-Expert Member

  #17
  Nov 5, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  ccm kitakufa tu,aidha kwa natural death,sumu ama kwa fitna.
   
 18. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #18
  Nov 6, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hapa umefunguka vizuri. Kwani kilishasajiliwa? Halafu hakikubadili jina, maana vyama vyote vilivyokuwepo miaka ya 60 havikuruhusiwa kutumia jina. Nasikia CCM haina usajili, ni kweli?
   
 19. D

  Dabudee Senior Member

  #19
  Nov 6, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 155
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kivunjeni chama hiki, Nape atakijenga kwa siku tatu. Alikwishatamka kwa mdomo wake mwenyewe kuwa hata akibaki peke yake chama hakitakufa.
   
 20. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #20
  Dec 12, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 7,496
  Likes Received: 353
  Trophy Points: 180
  hii ni moja ajenda katika uchaguzi wa 2015 kwani haitoshi kunyang'anya ccm madaraka huku tukiwaacha wakitanua na mali za wavuja jasho.
   
Loading...