snochet
JF-Expert Member
- Mar 31, 2011
- 1,407
- 1,110
Kikwazo kikubwa kinachoathiri biashara ya Daladala leo ni njia na usimamizi wa haya magari. Hii inajumuisha wasimamizi yaani TRA & trafiki, Bima etc.
Biashara ya Daladala imekuwa moja ya uwekezaji hatari zaidi hadi sasa kutokana na wamiliki kushindwa kushika mambo yote,tena ukizingatia wengi wamechukua mikopo na wana shughuli zingine mbali na usimamizi wa daladala.
Nimeona biashara hii kwenye nchi jirani ambapo wanaziita SACCO sijui uhusiano wake na Saccos lakini huwa wanasimamia magari ya watu..Kampuni hii inahusika na usimamizi kamili wa magari na kusimamia ufuatiliaji na tarehe na mileage ya service ya kawaida(oil, mafuta, tairi etc).
Kwa mtu mwenye muda,uwezo anaweza kubeba wazo hili na kulifanyia kazi.
Mtu huyu atakuwa na authority ya kuajiri madereva/deywaka, kupokea hesabu ya siku,pamoja na kuwasilisha hesabu kwa mmiliki ambapo msimamizi atatakiwa kupata 20% ya hesabu yote na mmiliki kupata 80% in a weekly/monthly basis.
Hili wazo linaweza kufanyika kwenye bodaboda/bajaj na vyombo vingine vya usafiri pia.
Sijajua bado kama hapa Tanzania kuna kampuni inafanya hii biashara naomba mnijuze kama ipo na terms zao zikoje watu wajikomboe na ajira zipatikane.