Wazito PPF wachota ‘vijisenti’

Status
Not open for further replies.

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,792
287,994
Wazito PPF wachota 'vijisenti'

Mwandishi Wetu Mei 7, 2008
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo


Walipwa kama wastaafu, kisha warudi kazini

WAKURUGENZI kadhaa wa Mfuko wa Pesheni ya Mashirika ya Umma (PPF), wamejilipa mamilioni ya fedha, ikiwa ni mafao yao ya kustaafu kazi, lakini imebainika kuwa wanaendelea na nyadhifa zao licha ya kujilipa.

Habari ambazo Raia Mwema imezipata wiki hii zinasema kuwa mafao ya wakurugenzi hao yanafikia kati ya Sh. milioni 130 na 220 kwa kila mmoja, kiwango ambacho kinafikia jumla ya Sh. bilioni 1.2, kilichotolewa na PPF kwa 'wastaafu' hao.

Raia Mwema imearifiwa kuwa malipo hayo yamefanyika kwa kufuata utaratibu uitwao Group Endowment Scheme, ambao unahusu mafao ya wafanyakazi yanayopaswa kutolewa kwa mtumishi anapostaafu kazi katika PPF.

Kwa mujibu wa habari hizo, chini ya mpango wa Group Endowment Scheme, wafanyakazi hukubaliana na mwajiri kabla ya kuanza kazi, ambapo shirika linakuwa linachangia kiasi fulani cha fedha kama akiba ya mfanyakazi, ambayo hupewa mara anapostaafu.

"Mnakubaliana wewe mfanyakazi na mwajiri. Ni kama mkataba wa aina fulani. Shirika linatoa fungu, linakuchangia…Unapoondoka kazini wakati unastaafu, unapewa fedha zako ili zikusaidie kwenye maisha yako mengine.

"Ukipewa fedha chini ya utaratibu wa Group Endowment Scheme, hatutarajii kuona mhusika anabaki kazini. Kama kuna watu wanafanya hivyo, basi wanauhujumu utaratibu huu," alisema Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa PPF, Naftali Nsemwa, ambaye aliombwa na Raia Mwema kutoa ufafanuzi wa jinsi mpango huo unavyofanya kazi.

Lakini Raia Mwema imeambiwa kwamba katika jambo ambalo linashangaza, wakurugenzi hao sita wa PPF wamejilipa mafao hayo ya Sh. bilioni 1.2, kwa maana ya kustaafu, lakini hadi jana Jumanne walikuwa wakiendelea na kazi, wakiwa tayari wameweka mafao yao vibindoni.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Badru Msangi, alipoulizwa kuhusu suala hilo, alikiri kuwapo kwa utaratibu wa Group Endowment Scheme, lakini akakataa kuzungumza zaidi kwa maelezo kuwa yeye si msemaji wa PPF, bali Mkurugenzi Mkuu mwenyewe, William Erio ambaye yuko safarini Afrika Kusini.

Hata baada ya kumsihi azungumze, Msangi alisema: "Msubiri Msemaji wa Shirika, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu. Atakuwepo ofisini wiki ijayo. Unapotaka sisi ndio tuzungumze, hututakii mema, unataka tufukuzwe kazi."

Mwenyekiti wa Bodi ya PPF, Gray Mgonja hakupatikana jana kuzungumzia suala hilo, na hata pale Raia Mwema ilipojaribu kuwasiliana naye, simu yake ilikuwa ikiita mfululizo na baadaye ikafungwa.

Raia Mwema ina majina ya wakurugenzi hao lakini kwa kuwa haikufanikiwa kuzungumza nao kuoata maelezo ya upande wao kwa sasa hawatatajwa.

Habari zaidi zilizopatikana zinasema kulipana huko kumehojiwa na mmoja wa wajumbe wa Bodi ya PPF, Monica Mbega akitaka kujua ni nani aliyeyaidhinisha.

Mbega alihoji suala hilo katika mkutano wa Jumamosi iliyopita wa timu ya ukaguzi ya Bodi ya PPF ambayo yeye ndiye Mwenyekiti wake. Yeye na Erio, na baadhi ya wakurugenzi ambao ni wajumbe wa timu hiyo, wako safarini Afrika Kusini.

Mikataba ya Group Endowment Scheme katika PPF imekuwa ikifanyika kila baada ya miaka mitatu, na mwenye kufaidika na mpango huo anapaswa kuwa awe anastaafu na kuondoka kabisa katika ajira ya PPF.
 
Naomba kuuliza huyu William Erio au Eriyo (lazima kuna tofauti) Si ndio Ndugu au anauhusiano na William Benjamin Mkapa au Mama Anna Mkapa?

Siye aliyewekwa kindugu hapo? au nimekosea?
 
Halafu huyo Gray Mgonja ana undugu wowote na yule Gray Mgonja wa

a. IPTL
b. Richmond
c. Rada
d. Tangold
e. Airbus


????
 
Simply put, Ndugu Gray Mgonja yumo kwenye Bodi zoote serikalini na kwenye makampuni binafsi (ofcourse sio zote ila nyingi). Sielewi GODFATHER wake ni nani hasa, ila ana connections kubwa!
 
Halafu huyo Gray Mgonja ana undugu wowote na yule Gray Mgonja wa

a. IPTL
b. Richmond
c. Rada
d. Tangold
e. Airbus


????

Yule yule mwenyekiti wa bodi ya PPF, Mjumbe wa Bodi ya BOT(EPA)
Sisi tunaochangia hilo shirika kweli tunaumia jamaa wanajinufaisha ile mbaya wana miradi mingi ya kifisadi ujenzi wa nyumba holela kiseke mwanza na maghorofa lukuki yasiyowasaidia wanachama huku tunaambiwa hadi tutimize miaka 55 ndio tuanze kupata Pensheni (waliondoa ule utaratibu ukitimiza miaka kumi unakuwa eligible kupata pensheni ufisadi mtupu wachangia wanapiga miayo tu
 
nani asiyejua taabu wanazozipata wastaafu wa nchii hii katika kufuatilia mafao yao??? kwa nini watu wote basi wasihudumiwe haraka haraka kama hawa wanavyojichotea.

Halafu afadhali hivyo vijisenti vingekuwa vya kufaa ni vijisenti haswa.
 
Yaani nimeshakuwa sugu kiasi ninaposoma habari kama hizi hivi sasa huwa sishtuki kabisa!
 
Ha ha haaa.. M.M.M acha uchokozi, si unajua mambo ya "Waarabu wa Pemba........."!!!!
Duh, kaaz kweli kweli wallahi nchi yetu Tanzania..... Eee Mola tusaidie!!
 
Huyu Mgonja balaa naona anaubia na urais wa JK yaani ananuka cent tu kila sector yeye haoni aibu duh balaa wanachukua chao mapemaaaaa nchi inabaki mikono mitupu na huyu William Erio si yule yule ndugu na ANBEN?? Hawa jamaa balaa sijui referee wao nani haswa yaani dili zinawanyokeaaa.
 
Ukitaka Habari Zaidi Ya Gray Mgonja Nenda Pale Eu Umoja Wa Nchi Za Ulaya Upande Wa Accounts Na Finance Ndio Wanamjua Sana Ndio Wengi Hula Nae Pale
 
Vijisenti vyaigawa PPF

Waandishi Wetu Mei 7, 2008
Raia Mwema

KUNA utata wa dhahiri katika Mfuko wa Pensheni ya Mashirika ya Umma (PPF), uliogubikwa na maamuzi ya kutatanisha, ikiwa ni pamoja na mafao ya wakurugenzi sita ‘waliostaafu' kutokuwamo kwenye bajeti ya shirika kwa mwaka huu.

Kumekuwa pia na kauli za kupingana, baadhi zikitaka waajiriwa wanaostaafu chini ya utaratibu wa Group Endowment Scheme, wapewe mafao mara ajira zao zinapokoma, na nyingine zikitaka mafao hayo yatolewe hata kama mfanyakazi anaendelea na ajira.

Taarifa zinasema kwamba lengo kuu la utaratibu wa Group Endowment Scheme lilikuwa ni kutoa zawadi kwa ustaafu na si kama mafao ya wafanyakazi kwa kuzingatia mikataba ya ajira, kwa kuwa utaratibu huo si sehemu ya marupurupu ya mwisho wa kila mkataba.

"Utaratibu wa Group Endowment Scheme ufanyike mwisho wa ajira ili kuhakikisha kuwa wafanyakazi wazuri na wazoefu wanaheshimu kanuni na taratibu muda wote wa ajira, ili kuhakikisha hawafutwi kazi kabla ya kufikia kikomo cha ajira.

"Utaratibu wa Group Endowment si wa kisheria bali ni tuzo maalum ya kustaafu kazi...haitakiwi kulipwa wakati huu kwa wafanyakazi watajwa, ambao wataendelea na ajira katika Mfuko (PPF). Ni utaratibu unaodhibiti nidhamu kwa wafanyakazi ili waepuke kufukuzwa. Kuwalipa wakati huu itakuwa ni kumomonyoa kusudio lake la awali," unasema waraka mmoja ambao Raia Mwema imefanikiwa kuuona.

Lakini taarifa ya PPF kwa umma, inasema kwamba wakurugenzi sita wa PPF walilipwa mafao ya Group Endowment, na kwamba malipo yalifanyika kufuatia kumalizika kwa mikataba yao ya ajira, ambayo ilimalizika Machi 31, mwaka huu, kwa wakurugenzi watano na Aprili 30, mwaka huu, kwa mkurugenzi mmoja.

"Ifahamike zaidi kuwa kufuatia kumalizika kwa ajira hizo, wakurugenzi hao waliomba kazi tena na Bodi (ya PPF) ikaridhia waajiriwe upya kuanzia tarehe 01.04.2008 kwa wakurugenzi watano na 01.05.2008 kwa mkurugenzi mmoja," inasema taarifa hiyo lakini bila kueleza hata hivyo kwamba mmoja wa wakurugenzi hao amelipwa kabla ya siku yake ya mwisho kazini kufika.

Pamoja na utata wote huo, bado Raia Mwema imedokezwa kuwa malipo yaliyofanyika, ambayo yanafikia Sh. bilioni 1.2, hayakufanywa kwa kuzingatia maamuzi yaliyofanywa kwenye bajeti ya PPF ya mwaka huu wa fedha, jambo ambalo linatia shaka kwenye mfumo wa maamuzi wa shirika hilo la umma.

Bajeti iliyopitishwa kwa mwaka 2008 huu wa fedha, ambayo imo kwenye kifungu namba 3.1.19 cha Group Endowment Expenses ni Sh. 1,730,187,000, lakini ukapitishwa uamuzi kwamba hakuna fedha itakayolipwa mwaka huu labda kama mfanyakazi atakua anacha kabisa ajira katika Mfuko.

Kwamba kiwango hicho hakitafaa kutolewa kwa mwaka huu, na badala yake kinapaswa kufanywa wakati mwajiriwa anapoacha kazi katika PPF.

Mgongano wa taarifa za ndani ya PPF baina ya mabosi wa shirika ni kielelezo kingine kwamba kuna mchezo mbaya unaofanyika, ikiwa ni pamoja na kujinufaisha kwa kisingizio cha "kwa mujibu wa mikataba, kanuni za utumishi za Mfuko na idhini ya Bodi ya Wadhamini."

Wakurugenzi hao sita, ambao wamelipwa mafao na kuendelea tena na kazi, walisaini mikataba ya miaka mitano ya kufanya kazi katika shirika hilo.

Mafao ya wakurugenzi hao yanafikia kati ya Sh. milioni 130 na 220 kwa kila mmoja, kiwango ambacho kinafikia jumla ya Sh. bilioni 1.2, kilichotolewa na PPF kwa ‘wastaafu' hao.

Chini ya mpango wa Group Endowment Scheme, wafanyakazi hukubaliana na mwajiri kabla ya kuanza kazi, ambapo shirika linakuwa linachangia kiasi fulani cha fedha kama akiba ya mfanyakazi, ambayo hupewa mara anapostaafu.

Raia Mwema ina majina ya wakurugenzi hao lakini kwa kuwa haikufanikiwa kuzungumza nao kupata maelezo ya upande wao kwa sasa hawatatajwa.
 
Tobaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!! Twafaaaaaaaaaaaaaaaaaa

JK mbona ana kazi ??????????
 
as long as JK alikubali pesa za ufisadi kwenye kampeni yake, zitamuandama mpaka mwisho. na kila atachofanya kitaenda kombo
 
Raia mwema hayo kama ni kweli ni vema ukawahoji hao wakulugenzi ili majina yao na sisi wananchi tuweze kuyapatabmajina yao ambao wanakula fedha za walala hoi
 
Haya habari nzuri anazozitaka JK si hizi sasa? kama kweli alikuwa anataka habari nzuri ndio hizo sasa kapewa aendeleze kasumba yake ya kukaa kimya kama kawaida yake??

Inakuwaje jamani, Kwanza ajira Tanzania ni chache, mijitu mingine inangangania kukaa tu hapo bila kujali kuwa umri wao umepita na wanatakiwa kuachia ngazi wachukue watu wengine

Pili hii serikali kuongozwa kwa mazoea, ndio mwanzo wa matatizo yote haya, sasa watu wanajua kuwa PPf ni yao na wanaweza kutunga sheria wakafanya watakavyo na kuzipindisha

Haya bwana, Hii ndio Tanzania na sisi ndivyo tulivyo
 
PPF ni moja ya mifuko ya mafao ya uzeeni ambayo imelalamikiwa sana juu ya malipo duni kwa wanachama wao ikilinganishwa na mifuko mingine.

Habari tuliyonyaka inaonyesha kwamba wajumbe wa Bodi iliyomaliza muda wake kipindi kilichopita ilipitisha na kujilipa milioni 200 kwa kila mjumbe. Hiyo ikiwa eti ni shukrani kwa kazi nzuri waliyofanya.

Nimepiga mahesabu yangu kwa idadi ya wajumbe wa bodi ambao walikuwepo, ambao ni wanane mbali na staff wengine wa pembeni:
1. Gray Mgonja
2. Prof Bertha Koda
3. Monica Mbega
4. Elvis Musiba
5. Ramadhan Khijah
6. Dr Kassim Kapalata
7. William Erio
8. Samwel Lwakatare

inaonyesha zaidi ya bilioni iliondoka.

Je, hii ni halali? Wanacahama wa PPF wengine huishia milioni 20 baada ya kuchangia hata kwa miaka 25. hawa wajumbe wanajilipa milioni 200 kila mtu kwa kukaa ktk vikao vya bodi kipindi kisichofikia hata miaka 5!! Na tena nasikia hao hao tena wamependekezwa kurudi ndani ya Bodi.

Heb
 
Status
Not open for further replies.
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom