Waziri: Watanzania wanalishwa tope

Bujibuji Simba Nyanaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
62,545
2,000
BAADA ya wachinjaji wa mifugo katika machinjio ya Vingunguti, Dar es Salaam kugoma kwa siku moja, Serikali imekiri hali ya machinjio hayo hairidhishi na kutoa mwezi mmoja kwa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kufanya maboresho mbalimbali.

Miongoni mwa maboresho hayo ni pamoja na kununuliwa kwa nondo 10 za kutundikia ngombe wakati wa kuchuna, kuzibua mashimo ya vyoo, kujenga eneo la kushushia mifugo hiyo, kununua jenereta mpya pamoja na kujenga eneo la kukatia nyama.

Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Dk. David Mathayo alitoa maagizo ya kukamilishwa kwa mahitaji hayo jana Dar es Salaam mara baada ya kufanya ziara katika machinjio hayo kwa lengo la kufahamu sababu za wachinjaji hao kugoma Ijumaa iliyopita.

Waziri Mathayo alishangaa kuona machinjio hayo yanakusanya fedha nyingi kwa mwezi, ambazo ni Sh milioni 24 lakini manispaa hiyo imeshindwa kuweka mazingira safi huku ikijua kuwa nyama inayotoka eneo hilo inatumiwa na idadi kubwa ya wananchi.

Aliitaka manispaa kuangalia athari za kufunga machinjio hayo na kuhoji , fedha zitokanazo na machinjio zinatumika kufanya nini, kwa kuwa hali ni mbaya.

“Magogo yanayotumika kukatia nyama nayo ni ya zamani na hapa mwananchi analishwa tope, mkishindwa kukamilisha taratibu zinazotakiwa machinjio yafungwe,” alisema Dk. Mathayo.

Kuhusu nondo za kutundikia ng’ombe, alisema hadi wiki ijayo ziwe zimenunuliwa nyingine, kuzibua matundu ya vyoo na kukarabati zaidi na kujenga eneo la kushushia ngombe na kukatia nyama vikamilike mwanzoni mwa Januari mwaka 2011.

Awali akisoma taarifa yake, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Gabriel Fuime alisema machinjio hayo yana uwezo wa kuchinja ngombe 250 hadi 300, mbuzi na kondoo 250 hadi 300 na Manispaa inakusanya wastani wa Sh milioni 24 kwa mwezi kutokana na ada ya Sh 2,500 kwa ngombe na Sh 650 kwa mbuzi na kondoo.

Alisema, hatua zilizochukuliwa baada ya mgomo ni kuzoa mbolea iliyolundikana katika eneo hilo kwa ajili ya kuimarisha usafi, kununua jenereta mpya, kukarabati la zamani na kurekebisha mfumo wa umeme kwa ajili ya kuongeza mwanga.

Hata hivyo alisema, leo atakutana na wafanyabiashara wote wa mifugo katika eneo hilo, ili kuwasikiliza na kupata maoni mbalimbali yenye lengo la kuboresha eneo hilo.Chanzo:- Habari Leo
 

Gama

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
12,531
2,000
Serikali itueleze mradi wa machinjio wa kiltex pale gongolamboto uliishia wapi.
 

Dick

JF-Expert Member
Feb 10, 2010
477
0
Kama serikali inashangaa, nani atende? Kama wameshindwa kazi wajiuzulu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom