Waziri Wassira: Sina tuhuma za ufisadi

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,577
6,582
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wassira amesema yeye ni mwanafunzi safi wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na kamwe hawezi kujiingiza kwenye vitendo viovu ukiwamo ufisadi.

Waziri Wassira, ambaye hivi karibuni aliibuka na ushindi wa kura 2,135 kwenye kundi la wajumbe 10 wa NEC, alisema matokeo hayo yanaonyesha wazi namna alivyopata darasa zuri kutoka kwa Mwalimu Nyerere.

Akihutubia wananchi wakati wa mikutano ya hadhara kwa nyakati tofauti, baada ya kupokelewa na wana CCM wilayani Bunda, Waziri Wassira alitamba katika uchaguzi huo hakununua mjumbe hata mmoja.

Wassira ambaye pia ni mbunge wa Bunda, alisema kamwe hata kama angekuwa na fedha asingeweza kufanya hivyo, kwani mafundisho ya Mwalimu Nyerere yanambana.

Alisema kiongozi yeyote, anayechaguliwa kwa kununua wananchi, hawezi kuwatumikia ipasavyo na wala hawezi kuwajibika kwao.

“Mwalimu Nyerere alisema, ukipata uongozi kwa rushwa hauwezi kuwatumikia wale waliokuchagua kwa sababu uliwanunua...ukitoa rushwa ili uchaguliwe hiyo ni sawa na biashara, maana wamekuuzia kura na wewe umenunua sasa ukishapata biashara imeisha.

“Sasa mimi siwezi kufanya hivyo kutokana na mafundisho haya, mimi ni mwanafunzi mzuri wa Nyerere, kamwe siwezi kufanya hivyo hamjawahi kusikia natajwa kwenye kashfa za ufisadi.

“Mwalimu Nyerere, hakupenda tabia ya rushwa hata kidogo, alipenda viongozi tuwatumikie wananchi wanaotuchagua na Mwalimu Nyerere aliwahi kunifundisha na kuniuliza unapenda watu au fedha, alisema ukipenda fedha hauwezi kutumikia watu ipasavyo,” alisema Wassira.

Kuhusu uchaguzi wa NEC, alisema umekijenga chama chao na kutoa misingi ambayo inaweza kusaidia kutatua matatizo ya wananchi.

Alisema ushindi huo, ni dalili ya wazi ya kuwamaliza wapinzani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kuingia Ikulu.

Alisema kazi kubwa inayofanywa na CCM, ni kujenga umoja, kama kauli mbiu yao inavyosema umoja ni ushindi.

Aliwataka viongozi wa chama hicho, kutembelea wanachama wao kuanzia ngazi ya chini na kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili, badala ya kukaa ofisini.

“Wananchi tuleteeni kero zenu pale ofisini kwetu, ili uongozi uzifuatilie na kuchukua hatua madhubuti kwa ajili ya kutafutia ufumbuzi,” alisema.

Alisema Serikali, haitasita kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi wanaokiuka maadili ya kazi zao, ikiwa ni pamoja na kuomba rushwa.


Chanzo: Gazeti la Mtanzania | Novemba 28, 2012 | Mwandhishi - Ahmed Makongo, Bunda
 
Si nilisikia kuwa huyu bwana anapora WAKE za wenzie? Ufuska ndo UFISADI per se
 
Sijasikia tuhuma za ufisadi kwa Wasira ila rushwa aliyotumia katika uchaguzi wa NEC ndio unaomtia hasira JK na Mangula.

Inakadiriwa kwamba Wasira alitumia sh 700M kuhonga wajumbe wamchague. Hili limemchafua Wasira ndani ya chama.
 
sijasikia tuhuma za ufisadi kwa wasira ila rushwa aliyotumia katika uchaguzi wa nec ndio unaomtia hasira jk na mangula.

Inakadiriwa kwamba wasira alitumia sh 700m kuhonga wajumbe wamchague. Hili limemchafua wasira ndani ya chama.

...kwa taarifa yako wewe sio mwana CCM, mkutano mkuu safari hii tofauti na chaguzi za jumuiya haukuwa na pesa ndio maana kashinda kwa merits...

Hizo milioni mia saba ulizibeba wewe siku ya jumapili...jk alipiga goli ya kisigino jumamosi wajumbe wakafika jumapili uchaguzi, nafasi ya kuhonga haikuwepo ila uchaguzi ulikuwa uwe jumanne...wasira alishinda fair & square
 
Sijasikia tuhuma za ufisadi kwa Wasira ila rushwa aliyotumia katika uchaguzi wa NEC ndio unaomtia hasira JK na Mangula.

Inakadiriwa kwamba Wasira alitumia sh 700M kuhonga wajumbe wamchague. Hili limemchafua Wasira ndani ya chama.

Misaada kutoka world bank kwa ajili ya huduma za jamii ktk jimbo lake zimepotelea mikononi mwake.
Amepaka rangi jengo la hospital kwa zaidi ya million 200.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
...kwa taarifa yako wewe sio mwana CCM, mkutano mkuu safari hii tofauti na chaguzi za jumuiya haukuwa na pesa ndio maana kashinda kwa merits...

Hizo milioni mia saba ulizibeba wewe siku ya jumapili...jk alipiga goli ya kisigino jumamosi wajumbe wakafika jumapili uchaguzi, nafasi ya kuhonga haikuwepo ila uchaguzi ulikuwa uwe jumanne...wasira alishinda fair & square
Sipati faida kusema uongo kama nisivyopata faida kubishana na yeyote JF. Post yako inajaribu bila mafanikio kushawishi kwamba rushwa uchaguzi NEC zilikuwa zinagawiwa wakati wa uchaguzi. Haikuwa hivyo, wajumbe walishapewa mshiko wao well before ya wiki ya uchaguzi. Wasira ni mgombea pekee aliyeongea na kila mjumbe ana kwa ana.

Kama shule yako upande wa hesabu na group psychology inakutosha ingekuwa rahisi kwako kusoma takwimu za kura waliopata wagombea na kugundua kwamba something was serious wrong kwa kura alizopata Wasira dhidi ya wapinzani wake.

Mgawanyo wa kura unaonyesha dhahiri kwamba wapiga kura walikubaliana kwa Wasira lakini waka deviate vibaya mno kwa wagombea wengine. Group psychology aisemi hivyo na hiyo ni kiashiria tosha cha uchunguzi wa rushwa. Wajumbe aliwahonga Wasira wanafunguka na safu mpya ya CCM inafahamu. Kama hard drive yako inatunza kumbukumbu za threads za JF utakuja kukumbuka maneno yangu kwamba rushwa hii ndio itakayomuangamiza Wasira.

Uwingi wa kura za NEC usikupumbaze hata siku moja maana kila mjumbe anajuwa mwenyewe jinsi alivyopata hizo kura. Utashangaa kwamba waliopata kura chache na au kushindwa uchaguzi wameshindwa kwa heshima mno kuliko walioshinda kwa fedheha maana walishindana na nguvu za rushwa.

Nilikuwapo Dodoma wiki mbili kabla ya uchaguzi na wito wangu kwa CCM ni kutokuhadaika na uwingi au matokeo ya chaguzi. Ni wagombea tu ndio wanaweza kutueleza namna kura walivyozipata na hivyo possibility ya kura zao kuakisi ubora wao ni highly questionable.

Position ya Wasira aliyonayo sasa serikalini inatosha kuchunguza endapo kura alizopata had anything to do with it na endapo mgombea kama Le Mutuz alikuwa anagombea na Wasira from the same line.
 
Stephen Wasira

From Wikipedia, the free encyclopedia


Stephen Masato Wasira (born 1945) is a Tanzanian politician.
Wasira served as Deputy Minister of Agriculture in the first phase Government under President Julius Nyerere and also served as the Deputy Minister for Local Government and later as the Minister of Agriculture and Livestock Development under second phase President Ali Hassan Mwinyi.

He was appointed as Minister of Water on January 4, 2006, when Jakaya Kikwete, who had been elected President, named his new cabinet. He was then moved to the position of Minister for Agriculture, Food Security and Cooperatives on October 15, 2006, and on February 12, 2008 he was named Minister in the Prime Minister's Office for Regional Administration and Local Government. On November 24, 2010, Mr. Wasira was names Minister of State President's Office in charge of Social relations and Coordination in the newly formed cabinet after October 2010 elections

Education



Positions .


  • Member of Parliament - Mwibara Constituency 1970 - 1975
  • Deputy Minister of Agriculture 1972 - 1975
  • Regional Commissioner Mara Region 1975 - 1982
  • Minister Counselor at the Embassy of Tanzania, Washington, DC, USA - 1982 - 1985
  • Member of Parliament - Bunda Constituency 1985 - 1990
  • Deputy Minister for Local Government 1987 - 1989
  • Minister of Agriculture and Livestock Development 1989 - 1990
  • Regional Commissioner Coastal Region 1990 - 1991
  • Member of Parliament - Bunda Constituency 1995 - 1996
  • Member of Parliament - Bunda Constituency 2005–Present
  • Minister for Water - January 2006 - October 2006
  • Minister of Agriculture, Food Security and Cooperatives - October 2006 - February 2008
  • Minister in the Prime Minister's Office for Regional Administration and Local Government - February 2008 - May 2008
  • Minister of Agriculture, Food Security and Cooperatives May 2008–2010
  • Minister of State President's Office in charge of Social relations and Government Planning Coordination November 2010 – Present


CV YAKE INAONYESHA NI EXPERIENCED NA HIVI YUPO TODAY (KAPATIA KITU FULANI), ELIMU YAKE NA CONVICTIONS ZINAONEKANA TANZANIA LEO SABABU THERE IS A CRY FOR GOOD LEADERSHIP VIJANA WAZEE KUNA OMBWE WE NEED MABADILIKO NA UADILIFU..SIJASIKIA KASHFA YA UKWELI ZAIDI YA POROJO AU WIZI WA TAIRI MIAKA ILE " I THINK ILI ZUSHWA NA MAHASIMU WAKE CDM"..

NYERERE LOVED WASIRA AKAMPA NAFASI, KATIKA VIONGOZI VILAZA WA SASA HUYU KIDOGO BADO ANAONEKANA ANAIPENDA NCHI, NAAMINI AKISEMA YEYE SIO FISADI SINA SABABU YA KUAMINI OTHERWISE UNTIL PROVEN OTHERWISE.
 
Misaada kutoka world bank kwa ajili ya huduma za jamii ktk jimbo lake zimepotelea mikononi mwake.
Amepaka rangi jengo la hospital kwa zaidi ya million 200.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Duh! Hii nilikuwa sijaipata, nitaifanyia kazi nipate ukweli wake maana hapa JF lazima ujiongeze.
 
sipati faida kusema uongo kama nisivyopata faida kubishana na yeyote jf. Post yako inajaribu bila mafanikio kushawishi kwamba rushwa uchaguzi nec zilikuwa zinagawiwa wakati wa uchaguzi. Haikuwa hivyo, wajumbe walishapewa mshiko wao well before ya wiki ya uchaguzi. Wasira ni mgombea pekee aliyeongea na kila mjumbe ana kwa ana.

Kama shule yako upande wa hesabu na group psychology inakutosha ingekuwa rahisi kwako kusoma takwimu za kura waliopata wagombea na kugundua kwamba something was serious wrong kwa kura alizopata wasira dhidi ya wapinzani wake.

Mgawanyo wa kura unaonyesha dhahiri kwamba wapiga kura walikubaliana kwa wasira lakini waka deviate vibaya mno kwa wagombea wengine. Group psychology aisemi hivyo na hiyo ni kiashiria tosha cha uchunguzi wa rushwa. Wajumbe aliwahonga wasira wanafunguka na safu mpya ya ccm inafahamu. Kama hard drive yako inatunza kumbukumbu za threads za jf utakuja kukumbuka maneno yangu kwamba rushwa hii ndio itakayomuangamiza wasira.

Uwingi wa kura za nec usikupumbaze hata siku moja maana kila mjumbe anajuwa mwenyewe jinsi alivyopata hizo kura. Utashangaa kwamba waliopata kura chache na au kushindwa uchaguzi wameshindwa kwa heshima mno kuliko walioshinda kwa fedheha maana walishindana na nguvu za rushwa.

Nilikuwapo dodoma wiki mbili kabla ya uchaguzi na wito wangu kwa ccm nikuto kuhadaika na uwingi au matokeo ya chaguzi. Ni wagombea tu ndio wanaweza kutueleza namna kura walivyozipata na hivyo possibility ya kura zao kuakisi ubora wao ni highly questionable. Position ya wasira aliyonayo sasa serikalini inatosha kuchunguza endapo kura alizopata had anything to do with it na endapo mgombea kama le mutuz alikuwa anagombea na wasira from the same line.

mimi ni mjumbe wa huo mkutano mkuu na nilipiga hizo kura siku ya jumapili..tulifika jumamosi, ratiba ilikuwa jumanne ndio tupige kura...swala la walipewa hizo mil 700 umelitunga na ni la uongo hadi utuletee ushahidi...kwamba hakukuwa na rushwa kabisa sio hoja ila ilikuwa minimized na ratiba

pili, la wasira kuzungumza na wananchama ni siasa sababu hakuna siasa bila kuzungumza..ila kila mjumbe ana kwa ana kwa mtu ambaye hafahimiki sio wasira..mpende usimpende ila kufahamika anafahamika na karibu kila mwana ccm...chaguzi zote yuko nao, igunga, arumeru na kujibu hoja za wapinzani.

Mwisho, makundi karibu yote wasira anazungumza nao...ndio maana kundi la membe, lowassa, sijui nani walimpa kura, hata zanzibar alifanya vizuri...wakati kura zinahesabiwa namba ya wasira 31 ilikuwa katika kila........hata wewe umesema kawazidi wengine ushindi wake ni umoja na walimkubali
 
Asidanganye watu, huyu ni bingwa wa rushwa. Kuna wakati aligombea ubunge akishindana na Warioba. Alishinda lakini ushindi wake ukatenguliwa kwa sababu ilionekana alishinda kwa rushwa! Hatujasahau!!
 
Ufisadi wa Wassira kama walivyo mawaziri wengi ni kuzitafuna TAASISI zilizo chini ya wizara wanazoziongoza. Ufisadi huu unafanyika kwa siri kubwa na ndio umewatajirisha akina Lowasa pia. Wanatafuna mamilioni kila mwaka. Sasa hivi TASAF iko chini ya wizara ya Wassira. Ulizieni mamilioni anayotafuna huko. Ufisadi huu haupigiwi kelele sana lakini upo na ni mkubwa zaidi hata ya EPA kwa mwaka.

Ndio maana zipo wizara ambazo kila waziri angetamani kuziongoza ikiwemo TAMISEMI, MAJI, NISHATI na MADINI, UJENZI, MAWASILIANO na UCHUKUZI,... Wizara hizi zina taasisi nyingi za UMMA. Kila Mkurugenzi Mkuu kwenye taasisi anapeleka mamilioni kwa mawaziri wetu hawa.

Wassira alikuwa hoi sana kabla hajateuliwa kuwa waziri mwaka 2006. Asema ahueni yake ya sasa kaitoa wapi kwa mishahara hii ya KITANZANIA.
 
asidanganye watu, huyu ni bingwa wa rushwa. Kuna wakati aligombea ubunge akishindana na warioba. Alishinda lakini ushindi wake ukatenguliwa kwa sababu ilionekana alishinda kwa rushwa! Hatujasahau!!
Basi hata ushindi wa Godbless Lema umetenguliwa sababu alishinda kwa rushwa pia?kwenu iringa, kama utakumbuka alikuwa NCCR...ukweli ukiwa kichomi upinzani Jimbo linatenguliwa kwa ki memo..
 
Mwandishi ameshalipwa kalamba chake. Habari imeshatoka jamaa anajigamba yeye ni safi. Moja ya kasoro kubwa ya uandishi Tanzania ni kukosa weledi wa kuandika habari zenye ushahidi wa kina katika pande mbili za sarafu. Waandishi wamegawanyika katika makundi. Wale wa maslahi -wanaojipendekeza wapate ulaji, wale ambao wanadakia fulani kasema nini wanaandika,wale ambao wamebaki katika misingi ya uandishi ambao ni wachache sana.
 
Wana Jf
Leo nilikua Wizara ya Kilimo na Chakula Idara ya Uhasibu katika mambo ya ambayo nimesikitika ni uzembe na Ufisadi wa waziri huyu akiwa katika serekali ya Awamu ya Nne .

Wazira wasira akiwa waziri Mwaka jana mwezi 4 alitakiwa kwenda mwanza kufungua kikao cha BODI ya Pamba jamaa akakatiwa Tiketi ya Ndege Precision jamaa akalala akapitiliza matokeo yake wizara ikabidi Imkodishie Ndege ndogo wizara ikaamua kumkodishia Single engine small flight akagoma wizara ilikua ilipe Dola 8000 kwa safari hiyo kwa aina hiyo ya Ndege.

Waziri akalazimisha akodishiwe Ndege ndogo yenye Engine mbili kwa Gharama ya Dola 13,000 hii ni fedha za walipa Kodi pia Waiting Charge na Gharama za kurudi. Ambazo kwa ujumla wizara ililipa Jumla ya Dola 19,870.

Tukio la Pili ni Ufisadi wa Ununuzi wa Gari ya wizara. Mwaka Jana (2010) mwezi Juni alinunuliwa Gari VX V8 ambayo ilikuwa haina Friji ndani kwa Gharama ya Milioni 250 akalikataa akataka zuri zaidi lenye madoido akataka la Thamani ya milioni 350 likaletwa mwezi September ambalo alilitumia kwa miezi 2 kabla ya uchaguzi.

Tukio la Tatu ni Kuibeba Kampuni inayoitwa SIMON GROUP kampuni hii ilipewa Miradi yote ya Kusambaza na Kuchukua Vyakula kutoka SGR za serekali bila kutangaza Tenda, Miradi hii Mwaka Jana Peke yake walipewa Miradi Ifuatayo. SONGEA 23.5bn, Iringa 19.2bn, Rukwa 39.5bn lakini pia ikumbukwe kampuni hii ndio iliyopewa kinyemela UDA kwa bei ya KUTUPA, kampuni hii ndio iliyonunua NYUMBA ya Familia ya MARIALE kwa 1bn masaki kampuni hii ilipewa Mradi mkubwa wa kuingiza Matrekta ambayo halmashauri zimelazimishwa kununua Matreka ya aina ya POWER TILER ambayo hayana uwezo wa kufanya kazi na mengi yamekwama. TUJIULIZE SIMON GROUP NANI YUPO NYUMA YA HII KAMPUNI?

Wana JF nimeleta uchafuu huu tuujadili na tuangalie huy wasira ambae anafanya kazi kwa karibu na MKULU.
 
Naona jamaa ameshaanza kuuota urais 2015.Kweli nimeamini 2015 patachimbika upande wa kushoto ,upande wa kulia na hata katikati pia patakuwa hapatoshi!
 
Wassira amepata kura nyingi za ujumbe wa NEC kwa kuitukana sana CHADEMA na VIONGOZI wake majukwaani. Vivyo hivyo Mwigulu naye kapata kura nyingi kwa sababu ya kuishambulia CHADEMA Bungeni. Wawili hawa wanapaswa kuishukuru CHADEMA kwa ushindi wao huo.
Namwona na WJM naye kawaiga humu JF. Naye anatukana Dr Slaa kama vile hana umri wa kumzaa.
 
wana jf
leo nilikua wizara ya kilimo na chakula idara ya uhasibu katika mambo ya ambayo nimesikitika ni uzembe na ufisadi wa waziri huyu akiwa katika serekali ya awamu ya nne .

wazira wasira akiwa waziri mwaka jana mwezi 4 alitakiwa kwenda mwanza kufungua kikao cha bodi ya pamba jamaa akakatiwa tiketi ya ndege precision jamaa akalala akapitiliza matokeo yake wizara ikabidi imkodishie ndege ndogo wizara ikaamua kumkodishia single engine small flight akagoma wizara ilikua ilipe dola 8000 kwa safari hiyo kwa aina hiyo ya ndege.

waziri akalazimisha akodishiwe ndege ndogo yenye engine mbili kwa gharama ya dola 13,000 hii ni fedha za walipa kodi pia waiting charge na gharama za kurudi. Ambazo kwa ujumla wizara ililipa jumla ya dola 19,870.

Tukio la pili ni ufisadi wa ununuzi wa gari ya wizara. Mwaka jana (2010) mwezi juni alinunuliwa gari vx v8 ambayo ilikuwa haina friji ndani kwa gharama ya milioni 250 akalikataa akataka zuri zaidi lenye madoido akataka la thamani ya milioni 350 likaletwa mwezi september ambalo alilitumia kwa miezi 2 kabla ya uchaguzi.

Tukio la tatu ni kuibeba kampuni inayoitwa simon group kampuni hii ilipewa miradi yote ya kusambaza na kuchukua vyakula kutoka sgr za serekali bila kutangaza tenda, miradi hii mwaka jana peke yake walipewa miradi ifuatayo. Songea 23.5bn, iringa 19.2bn, rukwa 39.5bn lakini pia ikumbukwe kampuni hii ndio iliyopewa kinyemela uda kwa bei ya kutupa, kampuni hii ndio iliyonunua nyumba ya familia ya mariale kwa 1bn masaki kampuni hii ilipewa mradi mkubwa wa kuingiza matrekta ambayo halmashauri zimelazimishwa kununua matreka ya aina ya power tiler ambayo hayana uwezo wa kufanya kazi na mengi yamekwama. Tujiulize simon group nani yupo nyuma ya hii kampuni?

Wana jf nimeleta uchafuu huu tuujadili na tuangalie huy wasira ambae anafanya kazi kwa karibu na mkulu.

Fact checker has detect ukanjanja with this reporting..1st, its try to level allegations of misuse of funds with ridiculing Wasira as someone who sleeps all the time "jamaa akalala akapitiliza akaachwa na ndege....it maybe comical but it doesnt apprear credible.

Simon group of companies is run by Mr. Robert kisena, the same company that bought UDA and is doing many businesses transportation, cotton ginning...unless you haven't participated in TZ tender process my friend, there is a Procurement Management Unit (PMU) and a Tender board, as minister you dont give out tenders that easily ...unless you honestly believe he is a shareholder of Simon group, which is highly unlikely the company has been around for years. Did it perform?

Rumors is not News, eti VX Haina friji na madoido...Guys are just disrespectful, i know we're tired but this post is simply ridiculous to be taken serious as him missing a flight..Come across as if its not news worth
 
Kama hana tuhuma za ufisadi sasa anataka nini?
Anataka URAIS. Hili amelisema mara kadhaa kwa watu wake wa karibu. Na kura za juzi mkutano mkuu wa CCM ndio zimemtia kiwewe kabisa. Anajiona kwa sasa ndie bora kabisa CCM. Alikuwa hamtaji Mwalimu tangu alipoangushwa na Warioba mahakamani kwenye ile kesi ya uchaguzi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom