Informer
JF-Expert Member
- Jul 29, 2006
- 1,582
- 6,627
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wassira amesema yeye ni mwanafunzi safi wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na kamwe hawezi kujiingiza kwenye vitendo viovu ukiwamo ufisadi.
Waziri Wassira, ambaye hivi karibuni aliibuka na ushindi wa kura 2,135 kwenye kundi la wajumbe 10 wa NEC, alisema matokeo hayo yanaonyesha wazi namna alivyopata darasa zuri kutoka kwa Mwalimu Nyerere.
Akihutubia wananchi wakati wa mikutano ya hadhara kwa nyakati tofauti, baada ya kupokelewa na wana CCM wilayani Bunda, Waziri Wassira alitamba katika uchaguzi huo hakununua mjumbe hata mmoja.
Wassira ambaye pia ni mbunge wa Bunda, alisema kamwe hata kama angekuwa na fedha asingeweza kufanya hivyo, kwani mafundisho ya Mwalimu Nyerere yanambana.
Alisema kiongozi yeyote, anayechaguliwa kwa kununua wananchi, hawezi kuwatumikia ipasavyo na wala hawezi kuwajibika kwao.
Mwalimu Nyerere alisema, ukipata uongozi kwa rushwa hauwezi kuwatumikia wale waliokuchagua kwa sababu uliwanunua...ukitoa rushwa ili uchaguliwe hiyo ni sawa na biashara, maana wamekuuzia kura na wewe umenunua sasa ukishapata biashara imeisha.
Sasa mimi siwezi kufanya hivyo kutokana na mafundisho haya, mimi ni mwanafunzi mzuri wa Nyerere, kamwe siwezi kufanya hivyo hamjawahi kusikia natajwa kwenye kashfa za ufisadi.
Mwalimu Nyerere, hakupenda tabia ya rushwa hata kidogo, alipenda viongozi tuwatumikie wananchi wanaotuchagua na Mwalimu Nyerere aliwahi kunifundisha na kuniuliza unapenda watu au fedha, alisema ukipenda fedha hauwezi kutumikia watu ipasavyo, alisema Wassira.
Kuhusu uchaguzi wa NEC, alisema umekijenga chama chao na kutoa misingi ambayo inaweza kusaidia kutatua matatizo ya wananchi.
Alisema ushindi huo, ni dalili ya wazi ya kuwamaliza wapinzani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kuingia Ikulu.
Alisema kazi kubwa inayofanywa na CCM, ni kujenga umoja, kama kauli mbiu yao inavyosema umoja ni ushindi.
Aliwataka viongozi wa chama hicho, kutembelea wanachama wao kuanzia ngazi ya chini na kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili, badala ya kukaa ofisini.
Wananchi tuleteeni kero zenu pale ofisini kwetu, ili uongozi uzifuatilie na kuchukua hatua madhubuti kwa ajili ya kutafutia ufumbuzi, alisema.
Alisema Serikali, haitasita kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi wanaokiuka maadili ya kazi zao, ikiwa ni pamoja na kuomba rushwa.
Chanzo: Gazeti la Mtanzania | Novemba 28, 2012 | Mwandhishi - Ahmed Makongo, Bunda