Waziri wa zamani wa Mawasiliano wa Afghanistan anauza Piza nchini Ujerumani

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Maisha yana namna nyingi za kutufundisha kushikilia tulichokuwa nacho kwa wakati huo.

Baada ya Kundi la Wanamgambo wa Taliban kuchukua utawala wa Afghanistan, aliyekuwa Waziri wa Mawasiliano wa taifa hilo, Syed Ahmed Shah Sadat ameonekana akitembeza Piza nchini Ujerumani.

Gazeti la nchini Ujerumani, Leipziger Volkszeitung, limeripoti kuwa Sadat sasa anafanya kazi katika kampuni ya chakula kama kijana anayewafikishia Piza wateja majumbani kwa kutumia baiskeli katika mji wa Leipzig.

Sadat, Mhitimu mwenye Shahada mbili za Uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Oxford, moja ya Uhandisi na nyingine ya Mawasiliano, alikuwa Waziri wa Mawasiliano chini ya serikali ya Ashraf Ghani hadi mwaka 2018 alipojiuzulu nafasi yake kutokana na kutofautiana na Ghani. Miaka miwili baadaye, Sadat alihamia nchini Ujerumani lakini kutokana na sababu za kiuchumi, mtaalamu huyo wa mawasiliano amelazimika kutembeza Piza kwa kutumia baiskeli ili mkono uende kinywani.

“Kwa sasa, ninaishi maisha ya kawaida kabisa. Ninahisi nina amani nchini Ujerumani. Ninaishi kwa furaha na familia yangu hapa Leipzig. Ninakusanya fedha na kusoma kozi ya Kijerumani ili niongeze elimu,” Sadat alinukuliwa.

Amesema amejaribu kutafuta kazi nyingi lakini kwa bahati mbaya hakupata kazi nyingine zaidi ya hiyo, na ana ndoto ya kufanya kazi katika kampuni ya teknolojia ya mawasiliano nchini Ujerumani.

Sadat ana uzoefu wa zaidi ya miaka 23 katika sekta ya mawasiliano, akiwa amefanya kazi na zaidi ya makampuni 20 katika zaidi ya nchi 13 ikiwamo Saudi Arabia.

Chanzo: Independent

1629983695239.png
 
“Kwa sasa, ninaishi maisha ya kawaida kabisa. Ninahisi nina amani nchini Ujerumani. Ninaishi kwa furaha na familia yangu hapa Leipzig. Ninakusanya fedha na kusoma kozi ya Kijerumani ili niongeze elimu,” Sadat alinukuliwa.

..jambo la msingi..
-"ana amani"
-"anaishi kwa furaha na familia yake"
-"anasave kujiendeleza kielimu"
Yatosha kusema mengine ni ziada tu..

]
 
Back
Top Bottom