TANZIA Waziri wa zamani, Dkt. Pius Yasebasi Ng'wandu afariki dunia

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
5,661
15,026
Mbunge wa zamani wa jimbo la Maswa pia aliwahi kuwa Waziri, Dkt Pius Ng'wandu amefariki dunia.

Amefariki Usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Somanda mjini Bariadi.

Alikimbizwa jana katika Hospitali hiyo baada ya kupata matatizo ya presha.

Mungu amlaze Mahali pema Peponi.

Dr. Pius Yasebasi Ng’wandu aliwahi kuwa balozi wa Japan Tokyo 1990 hadi 1993

Waziri wa Sayansi na Teknologia mwaka 2000 hadi 2008

Ng’wandu aliwahi kuwa Mbunge wa Maswa, pia Waziri wa Ardhi, Maji, Nyumba na Maendeleo ya Mji kuanzia mwaka 1985 hadi 1987, na alikuwa Waziri wa Maji 1987 hadi 1990, nafasi ambayo aliishika tena mwaka 1996 hadi 1999.

Dr_Pius_Y_Ngwandu_360_453shar-50brig-20_c1_c_t.jpg

Balozi Pius Yasebasi Ng'wandu enzi za uhai wake
 
Back
Top Bottom