kibogo
JF-Expert Member
- Apr 1, 2012
- 9,739
- 4,734
Wana JF wenzangu.
nachukua fulsa hii kuandika juu ya hili suala la sukari ambalo kwa sasa hali imekuwa mbaya zaidi kuliko walivyojinadi hawa viongozi wetu wa awamu hii ya tano.
Ikumbukwe kwa huku nilipo wakati Kikwete anaondoka mfuko wa Kg. 25 ulikuwa unauzwa Tshs. 44,000/= hadi 44,500/=, alipoingia Magufuli hapo Oktoba ilipanda na kufikia Tshs. 46,000/= na hapo tukasikia tamko la Rais kuwa ni marufuku kuagiza sukari kutoka nje ya nchi na sababu hasa ikiwa ni kuwa kuingiza huku kwa Sukari kunaua viwanda vya ndani. Kuanzia hapo sukari ikawa ni tatizo ndipo alipoteua baraza la Mawaziri na Mh. Mwijage kukabidhiwa Wizara na alikuja na mbwembwe nyingi kwa kukemea eti kuna wafanya biashara wanahujumu kwa kuficha sukari ili ipotee na kufanya bei iwe juu na ndipo ikajitokeza kampuni ya kiwanda cha Kagera Sugar na kujinadi mbele ya Waziri huku TV mbali mbali zikionyesha tukio hilo kuwa wao wameishazalisha Sukari ya kutosha na hakutakuwa na upungufu wa Sukari hapa nchini kwani wamejipanga kisawasawa kuzalisha sukari kwa wingi.
Ninayaandika haya kwa masikitiko makubwa kwani sasa hivi Sukari mfuko wa Kg. 25 unauzwa kati ya Tsh. 51,000/= hadi 52,000/= na sukari hiyo ni ile ya hicho kiwanda cha Kagera Sugar iliyojinadi kuwa itazalisha na kusambaza sukari nchini.
Sasa kwa mbwembwe zile huyu Waziri ni vema akajipima juu ya kauli zake kwani ni wazi tumeshuhudia maneno meeengi ambayo ni wazi yalikuwa kumfurahisha aliyemteua huku kiuhalisia ameshindwa kutekeleza yale aliyokuwa akiyaongea.