Waziri wa Viwanda na Biashara, Geofrey Mwambe atembelea Maonesho ya Wajasiriamali na kukagua bidhaa

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,512
141,239
Waziri wa viwanda na biashara Mhe. Mwambe ametembelea maonesho ya bidhaa za wajasiriamali katika viwanja vya saba saba jijini Dar es Salaam.

Mwambe amekagua bidhaa za wajasiriamali hao na kuwataka waendelee kujikita kwenye ubora na viwango ili waweze kupata masoko ya uhakika.

Maonesho hayo yatafungwa kesho 09/12/2020

Maendeleo hayana vyama!

==========

Mhe Waziri mteule ameeleza kuwa lengo la kutembelea Maonesho ya Tano ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania ni kujifunza, kujionea bidhaa zinazolishwa na viwanda vyetu vya ndani, kujua bidhaa zinazotengenezwa, aina ya bidhaa hizo na kufahamu upatikanaji wa malighafi, kujua muunganiko wa uzalishaji pamoja na masoko.

“Nimepata faraja kuona mwamko mkubwa wa Watanzania kuweza kuzalisha bidhaa za Tanzania ambapo awali bidhaa hizo tulikuwa tunaagiza kutoka nje ya nchi, kupitia Maonesho nimeona dhamira yao na imenipa somo la kuona uhitaji wa uzalishaji mkubwa ili kuweza kusafirisha nje ya nchi”

Ameongeza kwa kusema kuwa nchi yetu imeingia kwenye uchumi wa kati, hivyo wazalishaji wakiwezeshwa kwa kupata kipato kikubwa, wastani wa mapato utaongezeka na kuwa juu hivyo juhudi ya pamoja ndani ya serikali kuelekea mwaka 2025 nchi itaingia kwenye uchumi wa kipato cha kati cha juu utakaopelekea kuboresha maisha ya Watanzania na kutengeneza uchumi wa viwanda ulioimara wenye muunganiko mzuri kati ya wazalishaji wa kilimo, mifugo, uvuvi, viwanda na masoko

Amehitimisha kwa kusema kuwa kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara utatengenezwa mfumo thabiti wa kufanya muunganiko huo kupitia wizara zinazowagusa moja kwa moja ili kutengeza muunganiko wa wazi na matokeo makubwa na chanya.

1.JPG
2.JPG
3.JPG
4.JPG
 
Ametembelea TIC na Brela? Wafanyabiashara wengi kariakoo tunakwamba sana kupata huduma Brela kwasababu ya mitandao yao ya online. Huko TIC ukienda ni balaa kuomba misamaha ya uwekezaji ni shida tupu.

Yule Ceo wa TIC na wa Brela ni vema wakaondolewa mapema sana maana ni kama hawana wanalolikua kuhusu uwekezaji. Vigezo gani vilitumika kiwateua hawa.
 
Amekusikia bwashee.

Huyu waziri alikuwa CEO wa TIC juzikati kabla hajagombea ubunge, amekuelewa!
 
Hahahaaaa! Maalimu Seif na Zitto Kabwe wanakunywa juisi Ikulu muda huu wewe endelea kubrush viatu hapo Useri!
Usipende kuitaja taja useri sana aisee. Nitakupeleka mamtukuna nikufikishe tengu nikakufanyie kitu kahe.
 
Ametembelea TIC na Brela? Wafanyabiashara wengi kariakoo tunakwamba sana kupata huduma Brela kwasababu ya mitandao yao ya online. Huko TIC ukienda ni balaa kuomba misamaha ya uwekezaji ni shida tupu.

Yule Ceo wa TIC na wa Brela ni vema wakaondolewa mapema sana maana ni kama hawana wanalolikua kuhusu uwekezaji. Vigezo gani vilitumika kiwateua hawa.
Huyu waziri mwenyewe alikua hapo TIC kama boss mkuu.
 
haya tutajie waziri wa viwanda😂😂.. any way uko sahihi sababu mh G Mwambe ni waziri mteule wa viwanda🤔

Wizara haina Waziri toka Mkuu wa nchi aapishwe, na hakuna mbunge aliyekula kiapo kuwa Waziri.

Hata angekula kiapo, bado mwambe asingekuwa Waziri kwa sababu hajaapa kuwa Mbunge, hivyo mwambe siyo mbunge kwa sababu hajaapa kuwa Mbunge, na siyo Waziri kwa sababu siyo mbunge na hajaapa kuwa Mbunge.

Mwambe ni mbunge mteule, na Waziri mteule ila siyo Mbunge Wala Waziri
 
Back
Top Bottom