Waziri wa Viwanda na Biashara, Geofrey Mwambe atembelea Maonesho ya Wajasiriamali na kukagua bidhaa

Waziri wa viwanda na biashara Mh Mwambe ametembelea maonesho ya bidhaa za wajasiriamali katika viwanja vya saba saba jijini Dar es Salaam.

Mwambe amekagua bidhaa za wajasiriamali hao na kuwataka waendelee kujikita kwenye ubora na viwango ili waweze kupata masoko ya uhakika.

Maonesho hayo yatafungwa kesho 09/12/2020

Maendeleo hayana vyama!

==========

Mhe Waziri mteule ameeleza kuwa lengo la kutembelea Maonesho ya Tano ya Bidhaa za Viwanda vya Tanzania ni kujifunza, kujionea bidhaa zinazolishwa na viwanda vyetu vya ndani, kujua bidhaa zinazotengenezwa, aina ya bidhaa hizo na kufahamu upatikanaji wa malighafi, kujua muunganiko wa uzalishaji pamoja na masoko.

“Nimepata faraja kuona mwamko mkubwa wa Watanzania kuweza kuzalisha bidhaa za Tanzania ambapo awali bidhaa hizo tulikuwa tunaagiza kutoka nje ya nchi, kupitia Maonesho nimeona dhamira yao na imenipa somo la kuona uhitaji wa uzalishaji mkubwa ili kuweza kusafirisha nje ya nchi”

Ameongeza kwa kusema kuwa nchi yetu imeingia kwenye uchumi wa kati, hivyo wazalishaji wakiwezeshwa kwa kupata kipato kikubwa, wastani wa mapato utaongezeka na kuwa juu hivyo juhudi ya pamoja ndani ya serikali kuelekea mwaka 2025 nchi itaingia kwenye uchumi wa kipato cha kati cha juu utakaopelekea kuboresha maisha ya Watanzania na kutengeneza uchumi wa viwanda ulioimara wenye muunganiko mzuri kati ya wazalishaji wa kilimo, mifugo, uvuvi, viwanda na masoko

Amehitimisha kwa kusema kuwa kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara utatengenezwa mfumo thabiti wa kufanya muunganiko huo kupitia wizara zinazowagusa moja kwa moja ili kutengeza muunganiko wa wazi na matokeo makubwa na chanya.

Ameapishwa lini, wapi na nani?
 
Back
Top Bottom