Waziri wa viwanda na biashara alitoa vibali vya kuingiza Mchele. Huo Mchele umeshafika au bado maana hakuna mabadiriko sokoni

Wazolee

JF-Expert Member
Sep 1, 2018
2,699
3,088
Baada ya Mchele tuliolima wenyewe hapa nchini kupanda bila ya sababu za msingi waziri wa viwanda na biashara alisema atatoa vibali vya kuagiza Mchele uje nchini na kupunguza makali ya bei ya bidhaa hiyo. Lakini Cha kushangaza ndio imekuwa kimya na Hadi Sasa haieleweki huo Mchele umeshafika au bado

Au nao pia umedakwa na mafisadi maana kiuhalisia Kwa hapa Dar lazima bei ingeshuka chini maana gharama ya usafiri ingekuwa ni sawa na zero na serikali ingetoa Kodi hivyo bei ya Mchele ingekuwa chini sana.

Lakini pia na huko mikoani bei ingeshuka maana Mchele wao ungeuzwa huko huko kusingekuwa na sababu ya kusafirisha Mchele uje Dar wakati Dar Mchele upo kutoka nje.

Naanza kuamini hu mfumuko wa bei za nafaka ni mpango wa mafisadi na Ili kuwadhibiti mafisadi kiongozi unatakiwa uwe na roho ya chuma kama kipenzi chetu aliyetangulua mbele ya haki.
 
Mchele upo kaka ila hauwezi kushusha bei bei ina shushwa kwa gharama za kiuendeshaji kushuka
Gharama za uendeshaji zipi hizo

Mfanya biashara amepewa kibali amenunua Mchele nje akaupakia katika meli umefika bandarini utatoka bandarini na kusambazwa katika masoko kama vile Tandale , kariakoo,Ilala ,Tandika n k

Kutoka bandarini Hadi katika hayo masoko gharama ya usafiri ni sawa na zero na kama Kuna msamaha wa Kodi ndio kabisa bei itakuwa chini sana

Hizo gharama za uendeshaji unazosema wewe ni zipi?
 
Mchele uliagizwa na MO, unasambazwa na MO kwa bei ya 2000 ila watu wanauchukua wanauchanganya na mwingine wanauza bei ya wa Tz.
Nenda Tegeta, Kawe huo ndio mchezo unaofanyika.

Kiufupi mchele uliokuja ni mchache, hivyo yatakiwa vibali kuagiza mwingine ili bei ishuke

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Mchele uliagizwa na MO, unasambazwa na MO kwa bei ya 2000 ila watu wanauchukua wanauchanganya na mwingine wanauza bei ya wa Tz.
Nenda Tegeta, Kawe huo ndio mchezo unaofanyika.

Kiufupi mchele uliokuja ni mchache, hivyo yatakiwa vibali kuagiza mwingine ili bei ishuke

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Hakuna mfanyabiashara atakayeagiza Mchele Sasa hivi,mavuno ni April hii
 
Hakuna mfanyabiashara atakayeagiza Mchele Sasa hivi,mavuno ni April hii
Kwa lugha nyepesi wafanya biashara wameizidi nguvu serikali

Mchele wa ndani wameupandisha bei na kuagiza Mchele wa nje wamegoma japo walipewa vibali
 
Mwanasiasa hata akiwa baba yako mzazi usikae ukaamini kauli yake yeyote.
Hata akikwambia kumepambazuka toka nje uhakikishe kama kweli kuna jua.

Ukute aliesema keshasau hata kama alisema chochote kuhusu huo mchele.

Tupambane na hali zetu tu.
 
Back
Top Bottom