Waziri wa Viwanda: Hivi ni kweli wakulima tunashindwa kuungana na kuanzisha kiwanda cha nyanya hata cha Milioni 200??

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,300
2,000
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amelaumu uongozi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa kutunza fedha badala ya kuwakopesha wakulima.

Akifungua mkutano wa wadau wa kilimo leo Jumatano Desemba 6,2017, Mwijage amesema benki hiyo ina mabilioni ya fedha lakini kasi ya kuwakopesha wakulima ni ndogo.

“Rais John Magufuli ameuliza wakati nikiwepo ni kwa nini mabilioni ya fedha hayakopeshwi kwa wakulima,” amesema Mwijage.

Amesema Serikali imekuwa ikikopa kwa riba kwa ajili ya kuwekeza katika benki hiyo lakini yenyewe inakaa na fedha.

“Benki imekuwa mtunzaji wa fedha badala ya kuwa mkopeshaji,” amesema Mwijage.

Waziri amesema benki hiyo imekuwa ikisema ina hofu kwamba wakopaji hawawezi kurejesha mikopo.

Amesema hayo baada ya Mwenyekiti wa Baraza la Kilimo Tanzania (ACT), Dk Yusuph Sinare kumwomba Mwijage kufikisha kilio cha wakulima kwa Serikali kutaka benki hiyo iongezewe uwezo wa kukopesha.

Mwijage amesema mpango wa Serikali wa ujenzi wa viwanda utasaidia wakulima kupata masoko ya mazao yao.
Amesema wakulima wanatakiwa kuungana kujenga viwanda vidogo vya kusindika mazao ili kuyaongeza thamani.

“Kiwanda cha kusindika nyanya kinagharimu Sh200 milioni, hivi wakulima tunashindwa kuungana na kuanzisha viwanda vya namna hii,” amehoji Mwijage.

Amewataka kuachana na dhana iliyojengeka kwamba, wakulima kazi yao itaishia katika kilimo tu bali wanaweza pia kujenga viwanda.

Mwijage amezitaka mamlaka za Serikali kuacha kufanya kazi kipolisi bali zielimishe wawekezaji na si kuwatisha.

“Kuna mwekezaji alitishwa na watu wa mazingira kwamba asipofuata sheria ya mazingira atafungwa jela miaka saba.”
Mwenyekiti wa ACT, Dk Sinare amesema wakulima hawawezi kuwa na nguvu kama hawana benki imara.

“Tunaiomba Serikali iiongezee nguvu benki ya wakulima iweze kutoa mikopo kwa wakulima.”

Kuhusu masoko ya mazao, amesema wakati umefika kwa Serikali kuhifadhi chakula cha kutosha na wakulima kuruhusiwa kutafuta masoko ya mazao popote pale duniani.

Mwenyekiti mstaafu wa bodi ya ACT, Salum Shamte amewataka wakulima kutokuwa wazalishaji wa malighafi bali wabadilike na kuyaongeza thamani.
 

Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
10,890
2,000
Ni kweli mahindi ya Zambia yana soko zaidi hata Kenya zaidi ya mahindi yetu....hapo ndio utaelewa sisi hatuna mazao ya ubora unaohitajika hasa kwenye mbegu bora na matunzo bora hadi kuvuna!!!
 

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,597
2,000
Kuna Paragraph ya Kweli serikalini, nimequote hapa chini

"Amewataka kuachana na dhana iliyojengeka kwamba, wakulima kazi yao itaishia katika kilimo tu bali wanaweza pia kujenga viwanda.

Mwijage amezitaka mamlaka za Serikali kuacha kufanya kazi kipolisi bali zielimishe wawekezaji na si kuwatisha"

Ni kweli, wafanyakazi wengi wa Serikali, mamlaka zinawapa kiburi cha kutisha wananchi na wawekezaji, Wapo TRA, wapo NEMC etc

Ni ngumu sana kuwa Polite na kuelimisha mtu, wako wepesi tu kutoa Command
 

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
6,319
2,000
Huyo waziri anadhania kujenga kiwanda ni sawa na kujenga vyoo vya wanafunzi wa shule za kata.

Ujenzi wa kiwanda ni jambo moja, uendeshaji wa kiwanda ni jambo lingine na kuuza bidhaa za kiwanda ni jambo lingine na kupata faida kwa kuanzisha kiwanda ni jambo lingine tofauti kabisa.

Ukiona Wafanyabiashara maarufu wenye viwanda vingi na vikuba kama Mengi, Mo Dewji, Bakhresa, Manji, Dangote nk. hawajakimbilia kuanzisha viwanda vipya mpaka sasa, basi ujue biashara ya viwanda ni pasua kichwa balaa.
 

misasa

JF-Expert Member
Feb 5, 2014
10,730
2,000
Ni kweli, wafanyakazi wengi wa Serikali, mamlaka zinawapa kiburi cha kutisha wananchi na wawekezaji, Wapo TRA, wapo NEMC etc

Ni ngumu sana kuwa Polite na kuelimisha mtu, wako wepesi tu kutoa Command
Afadhari ata TRA ila NEMC ndio hatari kabisa mkuu.
 

dutch2

JF-Expert Member
Sep 20, 2017
1,010
2,000
zile bilioni20 za MO alizopeleka thimba wangemkomalia aziweke uko kwenye viwonder
 

ArchAngel

JF-Expert Member
Oct 11, 2015
4,458
2,000
Mwijage amesema mpango wa Serikali wa ujenzi wa viwanda utasaidia wakulima kupata masoko ya mazao yao.
Amesema wakulima wanatakiwa kuungana kujenga viwanda vidogo vya kusindika mazao ili kuyaongeza thamani.

“Kiwanda cha kusindika nyanya kinagharimu Sh200 milioni, hivi wakulima tunashindwa kuungana na kuanzisha viwanda vya namna hii,” amehoji Mwijage.

Kweli serikali inakosa 200m ya kujenga kiwanda mpaka wakulima wajichangishe?

Halafu kumbe ni mpango wa Serikali wa ujenzi wa viwanda ndio utasaidia wakulima kupata masoko ya mazao yao. Tangu lini mipango ikaleta masoko?


Hii sirikali imekosa maarifa. Siasa siasa tuu hadi kwenye masuala ya msingi.
 

natus

Senior Member
Nov 29, 2017
113
225
Wakulima ndiyo kundi lililo na watu hohehahe ktk yote wadau wa uchumi ktk Nchi hii. Umaskini wao unatokana na sababu nyingi mojawapo ikiwa hawana umoja wanaoweza kuutumia kutetea maslahi yao. Hata asasi kama MVIWATA zinazowapiga 'changa la macho' ati ni sauti ya Wakulima, hamna lolote. Wako pale kwa kuchumia matumbo yao. Wakulima hawawezi kuruhusiwa kuungana kirahisi kihivyo kwani watapata uwezo na nguvu kubwa kwamba hata Serikali watakuwa wanaiweka wao madarakani. Kutakucha! Wakulima wa Tanzania wakiungana na 'wakaachwa' kujenga umoja wao wenye nguvu ni hatari kwa maslahi ya watu au kikundi cha watu ambao wananufaika kiuchumi na kisiasa kutokana na Wakulima. Wengine tuliwahi jaribu kuwaamsha Wakulima kuwa na umoja, Ulisambaratishwa! Sijua, labda tusubiri hadi hapo wasomi wa SUA watakapoamua Kuja vijijini kuwaunga mkono maskini wazazi wao kulima hata kwa jembe la mkono.
 

girlie

Senior Member
Jul 14, 2017
170
250
Mambo zenu naulizia lodge nzuri sinza kwa 20,000 yenye ac,pasafi,kuwe na heater na maji ya kutosha.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom