Waziri wa Utalii na Mbunge wa Nzega ni wahaini, wanataka kuleta machafuko na umwagaji damu

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,441
55,017
..Waziri Maige amekaririwa akitoa matamshi ya vitisho kwamba yuko tayari kwa lolote akitetea wachimbaji wadogo wadogo dhidi ya mwekezaji.

..Mbunge wa Nzega, Mh.Kigwangalah naye ameandaa maandamano dhidi ya kampuni ya uchimbaji dhahabu iliyoko jimboni kwake.

..je hawa hawaingii ktk kundi la WAHAINI wanaotaka kuleta umwagaji damu nchini?
 
Kipindupindu said:
Sio mhaini!ni mtetezi wa wanyonge.

Kipindupindu,

..Waziri Maige amesema kwamba yeye atatetea wachimbaji wa wadogo, hataelewa lugha yoyote ile, na yuko tayari kwa lolote!!!

..sasa wewe hapo huoni kwamba huyo anatoa VITISHO kwa serikali? kuitishia serikali iliyochaguliwa na wananchi siyo UHAINI?

...mbunge wa Nzega, mh.Dr.Kingwagallah naye ameandaa maandamano kupinga mgodi wa dhahabu ulioko Nzega.

..sote tunaelewa kwamba migodini kuna mali nyingi, pia migodi hiyo inalindwa na askari wenye silaha nzito. sasa Dr.Kingwangallah haoni kwamba huo ni UCHOCHEZI? je, hana huruma na wananchi ambao wanaweza kumwaga DAMU na kupoteza MAISHA wakisikiliza uchochezi wake.

..KWANINI WABUNGE HAO WASITAFUTE NJIA ZA AMANI ZA KUSHUGHULIKIA MATATIZO HAYO, KULIKO HUU UCHOCHEZI WA KIHAINI?
 
Hata kule Arusha watu walikufa wakitetea haki zao.....waache hao viongozi watetee na washirikiane na wanyonge,hata kama damu itamwagika,ujumbe utakuwa umefika na mabadiliko yatafanyika hata kama si ya kuwanufaisha wao,lakini watoto wao watanufaika na maamuzi magumu ya wazazi wao.Tuache uoga,tutetee haki zetu.....Njia za amani Tanzania zimetumika sana,mara ngapi tumekuwa tunasikia kina Lissu na wengine wakiongelea sheria mbovu za madini? kuna utekelezaji wowote zaidi ya kudanganywa huku madini yakizidi kunufaisha wageni?? Inaruhusiwa kubadilisha approach ya kudai haki kama ile ya mwanzo haikufanya kazi.....!!!
 
..Waziri Maige amekaririwa akitoa matamshi ya vitisho kwamba yuko tayari kwa lolote akitetea wachimbaji wadogo wadogo dhidi ya mwekezaji.

..Mbunge wa Nzega, Mh.Kigwangalah naye ameandaa maandamano dhidi ya kampuni ya uchimbaji dhahabu iliyoko jimboni kwake.

..je hawa hawaingii ktk kundi la WAHAINI wanaotaka kuleta umwagaji damu nchini?
Ni watetezi wa wanyonge na wanasimamia people's power... na wanachofanya ni kusiamamia kiapo chao kama wabunge!!!

nimevitiwa na misimamo yao inayoonyesha kwamba hata kwenye CCM wapo walio na uwakilishi wa kweli kwa wananchi wao
 
Kwa tafsiri za hivi karibuni kutoka ccm wanawezakuitwa wahaini na watu wanaopingana na msimamo wa chama
 
..Waziri Maige amekaririwa akitoa matamshi ya vitisho kwamba yuko tayari kwa lolote akitetea wachimbaji wadogo wadogo dhidi ya mwekezaji.

..Mbunge wa Nzega, Mh.Kigwangalah naye ameandaa maandamano dhidi ya kampuni ya uchimbaji dhahabu iliyoko jimboni kwake.

..je hawa hawaingii ktk kundi la WAHAINI wanaotaka kuleta umwagaji damu nchini?

Hao wanajaribu kudesa kwa Dr Slaa...

...Eti watu wa "chama cha zamani" eti wao wakiongea lolote eti hiyo eti si lugha ya vitisho...

Kigwangalah yeye anaogopa kivuli cha Hussein Bashe. Anajua kuwa wanaCCM wa Nzega walimtaka Bashe, yeye akasaidiwa na familia ya Kikwete kupata ubunge, hivyo ni kama vile anajaribu kutafuta legitimacy. Simlaumu sana, ndiyo "si-hasa" hiyo...
 
Wakifanya ccm ni siasa, wakifanya cdm ni uchochezi na uhaini!
 
Back
Top Bottom