Waziri wa Umwagiliaji Isack Kamwelwe, atakiwa kuomba radhi kwa kudanganya

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,738
2,000
FB_IMG_1525709364145.jpg

KutokaBungeni Mbunge wa Monduli, Julius Kalanga (Chadema), amemtaka Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Isack Kamwelwe kuwaomba radhi Watanzania na Bunge kwa kudanganya kuwa fedha za maendeleo zilizotolewa katika bajeti ya mwaka 2017/18 ni asilimia 56 wakati kamati imebaini ni asilimia 22 pekee.

=====

Mbunge wa Monduli (Chadema), Julius Kalanga amemtaka Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe kuwaomba radhi Watanzania na Bunge kwa kudanganya kuwa fedha za maendeleo zilizotolewa katika bajeti ya mwaka 2017/18 ni asilimia 56 ilhali kamati ya bunge imebaini ni asilimia 22 tu.

Akichangia hotuba ya bajeti ya wizara hiyo iliyowasilishwa leo bungeni jijini Dodoma, Kalanga amesema takwimu nyingi za taarifa za hotuba hiyo zinapingana na za Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji.

Amesema waziri huyo ameonesha fedha za miradi ya maendeleo ya maji zimetolewa kwa asilimia 56 ili kulishawishi Bunge lipitishe bajeti hiyo ilihali wilaya nyingi ikiwamo Monduli hazijatengewa bajeti za mradi wowote mwaka huu.

“Waziri anasema ni asilimia 56 wakati kamati inasema 22, tunataka kujua nani ni mkweli? Amehoji Kalanga.

Akiwasilisha bajeti ya Mhandisi Kamwele katika bajeti ya mwaka 2017/18 hadi kufikia Machi mwaka huu wizara ilipokea fedha za maendeleo Sh bilioni 347.5 sawa na asilimia 56.

Chanzo: Mtanzania
 

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
7,064
2,000
Huyu Waziri kwa kujikomba kwa mkulu ni hatari! Alisababisha aliyekuwa Waziri wa Maji bw. Lwenge kutumbuliwa!
 

herzegovina

JF-Expert Member
Oct 28, 2015
3,121
2,000
Wote wanaiga

Kumbuka

"Nilipoingia madarakani sukari ilikuwa inauzwa SH. 5000/="
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom