Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,897
- 13,649
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt Stergomena Lawrence Tax (Mb) tarehe 09 Oktoba 2024 amefanya ziara na kutoa heshima zake katika Kaburi la aliyekuwa Rais wa Awamu ya 3 wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Benjamin Wiliam Mkapa, na kuwasamilia baadhi ya wanafamilia, katika Kijiji cha Lupaso, Wilaya Masasi Mkoa wa Mtwara.
Akiongea katika tukio hilo,Waziri Tax aliyeambatana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala na ujumbe wa mkoa, Waziri Tax, amemzungumzia Hayati Benjamin Mkapa aliyewahi kufanya kazi naye kwa karibu, kama Kiongozi mahiri na mchapakazi wakati wa uhai wake na mfano wa kuigwa.