Waziri wa Ulinzi Cyprus ajiuzuru - mlipuko wa mabomu kama Go/mboto, Mbagala | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri wa Ulinzi Cyprus ajiuzuru - mlipuko wa mabomu kama Go/mboto, Mbagala

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jul 12, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Waziri wa ulinzi wa Cyprus amejiuzuru kutokana na scandoo ya mabomu kulipuga kutoka ghala la silaha la jeshi na kusababisha hasara kubwa. Taarifa ya habari za kimataifa kutoka CNN, zinasema ni kitu kisichovumilika katika utendaji na uwajibikaji wa kiongozi ha hivyo kulazimika kujiuzuru.

  Serikali ya Tanzania licha ya kutokea zaidi ya mara moja lakini hakuna kujiuzuru na wala kuonywa na viongozi wa juu hasa waziri mhusika Husein Mwingi akitangaza kwamba hana kosa na hajiuzuru. Hii ni aibu sana kwa utendaji wa serikali nchini mwetu. Je serikali inajifunza nini kutoka kwa hawa wenzetu wanavyowajibika>
   
 2. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #2
  Jul 12, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  wa hapa ni mwana wa mfalme aliyepita labda huyo wa "bold" ni mtoto wa mkulima wa mpunga
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  ali

  Ndo maana yake.

  Lakini tukio la awali aliuambia umma wa watanzania kwamba kosa lile halitatokea tena, na lilipotokea tena kilikuwa na kielelezo dhahiri cha uzembe wa hali ya juu na kutowajibika kwake.
   
 4. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #4
  Jul 12, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,613
  Likes Received: 4,719
  Trophy Points: 280
  Huyu wa hapa anaandaliwa mazingira ya kupewa urais, tehe tehe, tehe
   
 5. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #5
  Jul 12, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  na wahapa atajiuzuru 20115 usihofu kwani bado uchunguzi unaendelea, au wewe umesha sikia report ya tume iliyoundwa? kama hujasikia jua kuwa bado tume inaendelea na kazi yake ikikamilika na yeye atajiuzuru
   
 6. M

  Marytina JF-Expert Member

  #6
  Jul 12, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Huyu wa kwetu msimlazimishe kujiuzulu kwani mtaambiwa mnaichukia dini yake
   
 7. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #7
  Jul 12, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Haya ya udini kushikia bango kaka Kikwete na Salma walivyoshikia bango kipindi cha kampeni matokea ndo hayo kulindana, kuhifadhiana, kukirimiana nk
   
 8. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #8
  Jul 12, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Watakwambia Cyprus wana utamaduni tofauti na sisi!! tuna namna tunavyoendesha mambo yetu! Tehe tehe tehe!!
   
 9. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #9
  Jul 12, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kujiuzulu ni ukomavu wa kiongozi, huyu wakwetu hapa hajakomaa na hata hiyo nafasi aliyonayo sio saizi yake kwahiyo asitarajie kuipata ya ukuu wa kaya
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Jul 12, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,688
  Likes Received: 82,553
  Trophy Points: 280
  Mkuu unategemea Serikali ya magamba ijifunze chochote kutoka nchi nyingine? Angalia hii issue ya umeme, nchi nyingine Ngeleja angeshatimuliwa miaka mingi sana lakini bado anapeta. Huyo Hussein Mwinyi naye hali kadhalika. Mkullo mwaka jana katengeneza bajeti ya Serikali kwa miezi 12 kumbe ilikuwa ya miezi 6 tu!! January mwaka huu wakaanza kupitisha kibakuli chao cha kuomba omba kwa Wafadhili. Kwa Serikali ambayo sio taahira hawa wote wangefukuzwa kazi muda mrefu lakini si kwa Serikali ya magamba.
   
 11. Msema hovyo

  Msema hovyo Senior Member

  #11
  Jul 12, 2011
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wamshukuru kwamba wenzetu bado wana viongozi, sisi Tanzania tuna makapi ya viongozi
   
 12. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #12
  Jul 12, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mwajiri wake mkuu aliyempa cheo hicho kwa malipo ya kukirimiwa atakwambia ajipime mwenyewe na aamue kujiuzuru kwa hiari yake
   
 13. Mwazange

  Mwazange JF-Expert Member

  #13
  Jul 12, 2011
  Joined: Nov 16, 2007
  Messages: 1,051
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Da aisee wee unauliza makubwa sana....waziri ajiuzulu kutokana na vile vijibomu, vilivyoua dazeni kadhaa ya watu? Si unakumbuka mkuu wa kambi alisema lakini hakuna mwanajeshi aliyepoteza maisha; hiyo imewatosha kabisa. Lini uliona mwananchi wa kawaida akathaminiwa hapa kwetu?
  Unathubutu kuulizia uwajibikaji wa waziri wa nishati? Muheshimiwa yule yule aliyesinzia pembeni mwa mkuu wa nchi wakati wa mkutano nje nchi? Si mwenyewe alishamuona anasinzia kazini na akaridhika naye? sasa wewe unahoji nini hapo? Tumempa nchi iwe kama banda lake la uani, afanye atakavyo. Kwa hiyo sisi tunyamaze tu, muda wake utakwisha, ataondoka, atakuja mwengine, atafanya yaleyale, hadi hapo tutakapoamka na kuanza kuwawajibisha viongozi. Mpaka hapo kukikucha, ila sasa hivi tuwaache tu wajilie nchi yao hii.
   
Loading...