Waziri wa ujerumani aliyechakachua phd ajiuzulu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri wa ujerumani aliyechakachua phd ajiuzulu

Discussion in 'International Forum' started by Faru Kabula, Feb 6, 2013.

  1. Faru Kabula

    Faru Kabula JF-Expert Member

    #1
    Feb 6, 2013
    Joined: Mar 26, 2009
    Messages: 10,642
    Likes Received: 2,876
    Trophy Points: 280
    [​IMG]
    Waziri wa elimu wa Ujerumani, Annette Schavan, amevuliwa cheo chake cha Daktari wa Falsafa, baada ya kugundulika kuwepo na wizi wa mawazo ya mtu.

    Chuo Kikuu cha Düsseldorf kilichoko mashariki wa Ujerumani, kimesema jana jioni kuwa Schavan hakuonyesha vyanzo ipasavyo katika shahada yake ya juu ya mwaka 1980, ambayo ilichunguza uundwaji wa dhamira na kwamba kwa makusudi alichukuwa mawazo na kuyaonyesha kama ya kwake.

    Madai kuwa Schavan aliiba mawazo ya sehemu ya shahada yake ya juu, yalianza mwaka uliyopita, wakati madai yasiyo na jina yalipochapishwa kwenye mtandao wa intaneti.

    Schavan siyo mwanasiasa wa kwanza maarufu nchini Ujerumani kudaiwa kuiba mawazo mwaka 2011, aliyekuwa waziri wa ulinzi Karl-Theodor zu Guttenberg alivuliwa shahada yake ya juu na kulaazimishwa kujiuzulu.

    Chanzo: Deutsche Welle
     
  2. Mkoroshokigoli

    Mkoroshokigoli JF-Expert Member

    #2
    Feb 6, 2013
    Joined: Dec 20, 2012
    Messages: 14,419
    Likes Received: 2,519
    Trophy Points: 280
    Waziri wa elimu wa Ujerumani Annete Schavan amevuliwa PhD yake kwa kosa la kuiba mawazo ya mtu na kujifanya ni ya kwake,sosi:taarifa ya habari ya redio Kheir

    a-16544422.jpg
     
  3. mansakankanmusa

    mansakankanmusa JF-Expert Member

    #3
    Feb 6, 2013
    Joined: Sep 30, 2010
    Messages: 4,091
    Likes Received: 603
    Trophy Points: 280
  4. Babu Lao

    Babu Lao JF-Expert Member

    #4
    Feb 6, 2013
    Joined: Nov 2, 2010
    Messages: 2,056
    Likes Received: 9
    Trophy Points: 135
    Mulugo vipi????
     
  5. Mamndenyi

    Mamndenyi JF-Expert Member

    #5
    Feb 6, 2013
    Joined: Apr 11, 2011
    Messages: 29,103
    Likes Received: 6,567
    Trophy Points: 280
    bongo inajulikana kama copy and paste na watu kibao wanatumia huu mtindo na wanapata maganda yao.
     
  6. Iron Lady

    Iron Lady JF-Expert Member

    #6
    Feb 6, 2013
    Joined: Mar 4, 2008
    Messages: 4,077
    Likes Received: 133
    Trophy Points: 160
    wenzetu wapo makini katika vitu kama hivi.
    hapa kwetu wanafanya kubebana tu tukiamua kuwa kama hawa wengi tu watavuliwa vyeti vyao
     
  7. kabanga

    kabanga JF-Expert Member

    #7
    Feb 6, 2013
    Joined: Dec 12, 2011
    Messages: 29,805
    Likes Received: 3,702
    Trophy Points: 280
    one nineteen sixty one....
     
  8. Kennedy

    Kennedy JF-Expert Member

    #8
    Feb 6, 2013
    Joined: Dec 28, 2011
    Messages: 11,329
    Likes Received: 2,980
    Trophy Points: 280
    Wako smart unadhani mpaka sasa Hamim(Mulugo) km ni Ujerumani asingekuwa Waziri.
     
  9. Jagarld

    Jagarld JF-Expert Member

    #9
    Feb 6, 2013
    Joined: Apr 7, 2011
    Messages: 1,536
    Likes Received: 227
    Trophy Points: 160
    mbona huja acknowledge mkuu kwa mhusika nawe tutakunyang'anya sababu kila mmoja anajua haya maneno mazuri yalitamkwa na Mlugo!
     
  10. Gefu

    Gefu JF-Expert Member

    #10
    Feb 7, 2013
    Joined: Nov 30, 2010
    Messages: 6,962
    Likes Received: 257
    Trophy Points: 180
    Chuo kikuu cha Heinrich-Heine cha Dusseldorf kimempokonya waziri wa elimu na sayansi Anette Schavan wa chama cha CDU,shahada yake ya uzamili aliyoipata miaka 33 kwa makosa ya udangayifu

    Baada ya miezi kadhaa ya uchunguzi kupitia vituo tofauti, wanachama15 wa baraza la kitivo cha falsafa walikutana kwa saa kadhaa jana na kukubaliana kwa wingi mkubwa bibi Anette Schavan,mwenye umri wa miaka 57 amefanya udanganyifu alipoandika tasnifu yake,aliyoipa jina "Mtu na Moyo."Schavan amefanya makusudi kutumia vifungu vya maneno na fikra ambazo kusema kweli si zake" amesema mkuu wa kitivo cha falsafa cha chuo kikuu cha Heinrich Heine mjini Düsseldorf,Bruno Bleckmann.

    Waziri huyo wa elimu na sayansi wa serikali kuu ya Ujerumani daima amekuwa akisema pengine amefanya makosa ya kijuu juu,lakini hajafanya uhadaa wala udanganyifu.
    Bibi Anette Schavan ambae hivi sasa yuko ziarani nchini Afrika kusini anajikuta hivi sasa mikono mitupu-shahada zake zote alizopata chuo kikuu zimekuwa batil baada ya kupokonywa shahada hiyo ya uzamili.

    Source: DW
     
  11. Bornvilla

    Bornvilla JF-Expert Member

    #11
    Feb 7, 2013
    Joined: Feb 17, 2011
    Messages: 925
    Likes Received: 20
    Trophy Points: 35
    Bongo mbona asilimia kubwa ni mzbingwa wa copy n paste? Tukisema research za hata wanaojiita magreat thinkers humu JF utakuta ni full plagerism. Mawaziri wengi tu na wasomi kibao wana copy. Nenda vyuo vikuu ukaone jamaa wanavyocopy toka intrenet. Yaani kwa Bongo ni bora mtu katoka na degree tu na ndio maana hakuna ubunifu mwisho taifa limekuwa la vilaza. Tunakoenda itakuwa balaa zaidi.
     
  12. charger

    charger JF-Expert Member

    #12
    Feb 7, 2013
    Joined: Nov 21, 2010
    Messages: 2,327
    Likes Received: 64
    Trophy Points: 145
    Aisee!
     
  13. UJANJAUJANJA

    UJANJAUJANJA JF-Expert Member

    #13
    Feb 7, 2013
    Joined: Oct 14, 2012
    Messages: 215
    Likes Received: 13
    Trophy Points: 35
    Possible in Germany but not in Tanzania
     
  14. N

    Ngekewa JF-Expert Member

    #14
    Feb 7, 2013
    Joined: Jul 8, 2008
    Messages: 7,730
    Likes Received: 23
    Trophy Points: 135
    Huyu ni wa Chama gani CCM au CHADEMA?
     
  15. nyabhingi

    nyabhingi JF-Expert Member

    #15
    Feb 7, 2013
    Joined: Oct 12, 2010
    Messages: 10,898
    Likes Received: 5,360
    Trophy Points: 280
    Mbona story ya zamani sana hii
     
  16. kbosho

    kbosho JF-Expert Member

    #16
    Feb 7, 2013
    Joined: Jun 4, 2012
    Messages: 12,505
    Likes Received: 3,314
    Trophy Points: 280
    wap mchmb, maanga na.......
     
  17. Gefu

    Gefu JF-Expert Member

    #17
    Feb 7, 2013
    Joined: Nov 30, 2010
    Messages: 6,962
    Likes Received: 257
    Trophy Points: 180
    ..au ndo hao wanao hujumu hoja binafsi za upinzani kwa hofu ya madudu ya wizara ya Elimu ?
     
  18. Gefu

    Gefu JF-Expert Member

    #18
    Feb 7, 2013
    Joined: Nov 30, 2010
    Messages: 6,962
    Likes Received: 257
    Trophy Points: 180
    kwangu mpya, si unajua mambo ya ving'amuzi mkuu !
     
  19. Gefu

    Gefu JF-Expert Member

    #19
    Feb 7, 2013
    Joined: Nov 30, 2010
    Messages: 6,962
    Likes Received: 257
    Trophy Points: 180
    ..ndo halihalisi mkuu ! wakati vyuo vyetu vinagawa phd hata kwa wafuga kuku !
     
  20. Gefu

    Gefu JF-Expert Member

    #20
    Feb 7, 2013
    Joined: Nov 30, 2010
    Messages: 6,962
    Likes Received: 257
    Trophy Points: 180
    ...lukuvii,nagu...
     
Loading...