Waziri wa Ujenzi una Wizara kubwa mno, sina hakika kama unaimudu

mmteule

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
5,502
12,827
Waziri wa Ujenzi una wizara kubwa mno, sina hakika kama unaimudu. Enzi hizo wizara hiyo ndiyo ilimtoa Hayati Magufuli mpaka kufikia kujulikana utendajikazi wake kwa Watanzania.

Wizara yako inabeba ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji, usimamizi wa TEMESA, TBA, TAA, TANROADS, magari yote ya serikali nk.

Waziri, tunapigwa kiaina kwenye wizara yako: Barabara nyingi za lami zilizojengwa na Wachina ni machinjio na chanzo cha ajali nyingi. Pita barabara ya Dodoma-Iringa via Mtera. Ni aibu na fedhea kuongea yanayoonekana.

Pita barabara ya Songea-Njombe-Makambako inafikirisha mno. Funga kazi pita barabara ya Mwigumbi-Maswa-Bariadi ambayo Mchina ameamriwa kuirudia upya baada ya kuikosea awali, hakika ni maajabu ya Dunia.

Barabara imekwanguliwa na dozzer then ikarejeshewa lami, kwahiyo zile kucha za doza hazikujazwa vzuri ukipita na gari inakuwa inayumbishwa na ile mikwaruzo ya dozza, ni hatari.

Zile gari ndogo aina ya Wish na Probox zinazopiga deiwaka kwenye hiyo barabara zinakula mzinga kila siku, wakija wazee wa form IV failure kama kawaida wanafunga jalada ajali imetokana na mwendokasi. Kwakweli ile barabara nadhani ni mpango wa kuwapunguza Wasukuma not otherwise, kazi kwako.

Waziri, kuna hivi vivuko vya serikali kwenye mito, maziwa na bahar,i mzee wangu huko ndiko watu wanajipigia kama mali zao binafsi. Nina hakika hata wewe unajua ila hatujui kama uko hapo wizarani kufanikisha malengo yepi.

Waziri kuna hizi taa za Solar mnafunga barabarani, hivi mnauigizia nani? Taa zinawaka wiki 1 zinakufa halafu mnaendelea kila siku kuzifunga for what? Hapa tunapigwa changa la macho hizi taa za Kichina ni maigizo tu.

Waziri, gari za esrikali zina namba zake yaani ST, DFP, SU n.k, lakini nakuhakikishia kwa sasa kuna wimbi kubwa taasisi za umma kusajili kwa namba binafsi hata zile zenye namba rasmi zinapachikwa namba binafsi. Huu ni ukosefu wa usimamizi thabiti, watangulizi wako hasa JPM alifanya vyema eneo hili. SUMA JKT ni mali ya umma gari zake private namba, anza na hao wengine utawajua.

Waziri, gari za serikali zinakuwa na matangazo ya biashara za watu binafsi na ni kosa kisheria. Mali ya umma kuwa na bandiko za aina hiyo hili nalo huoni au mpaka Rais aseme mkalitizame?

Wazir, uko bize sana na barabara tu, najua huko ndiko kwenye 10% nono kiasi kwamba hujui kama unao TEMESA, sasa fika, huko ndiko machinjio ya gari za umma. Diff oil inawekwa kwenye Injini, Injini oil inawekwa kwenye gear box ni aibu ni fedhea ni hasira.😭

Hatuna cha kusema maana sijui wewe ni binamu au kaka au mjomba wa mwenye nchi lkn yakhee hutoshi hapo bwanshee!
 
Back
Top Bottom