Waziri wa Ujenzi tunaomba ufuatilie barabara ya Morogoro kuanzia Kimara hadi Kibaha

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,120
7,702
Kwanza kabisa tunamshukuru sana Hayati JPM kwa kufanya maamuzi magumu ya kujenga barabara ya njia 6/8 kuanzia Kimara hadi Kibaha, hakika barabara hii sio tu kwamba imeondoa foleni ktk maeneo hayo lkn pia imeboresha muonekano wa Jiji la DSM, kila anayepita juu ya "mkeka" huu hakika anamkubali na kumrehemu JPM japo kimya kimya!.

Tatizo na changamoto nilizo ziona ktk Barabara hii ni ufinyu wa vituo vya daladala, na maeneo mengine hayana mahali vituo vidogo vya daladala kupaki kwa yale yanayo ishia kwa mfano Kibamba/kituo cha polisi kiluvya gogoni, maeneo hayo ilipaswa ijengwe stendi ndogo ya daladala ili kuruhusu mabasi kupaki.

kwa sasa wananchi wanao fuata huduma za polisi kiluvya gogoni wanalazimika kusha kibamba na kisha kutembea kwa miguu umbali wa km.1 na nusu hadi kituo cha polisi.

Tunashauri kituo cha daladala kijengwe maeneo hayo.

Pili tunashauri kwa hadhi ya barabara hii ziwekwe taa za barabarani.

Kwa mara nyingine nampa hongera prof. Mbarwa kwa kuteuliwa kuwa waziri wa ujenzi.
Kazi iendelee.
 
Mh Mbalawa, katika watu wanaotaabika hapa Morogoro ni wakazi wa Kilombero na Ifakara wanaotumia barabara Kidatu -Ifakara. Hii barabara ni ya kipande kifupi mnoooooo. Lakini mizaha zaha imekuwa mingi

Imeanza kufanyiwa maigizo ya kuwekwa lami tangu wakati wa Hayati Magufuli. Na tangu wakati huo watu wanapiga mark time tuuu.

Miaka inaenda, miaka inaisha , wala hakuna development ya maana inayoonekana katika ile scheme. Ni kama vile wahusika wa ile tenda wanajifanyia kazi kwa namna wanayoyataka.

Je, ni lini wizara yako itakuwa serious na kuhakikisha hii barabara inakamilika haraka iwezekanavyo, wananchi wa Kilombero wamechoka kula vumbi. Ebu muwaelewe.
 
Heee! Jamani! Hayo matatizo yoooote yalikuwa yanamsubiri Mheshimiwa?
Mwacheni atulie kwanza, apange program yake.
Miradi yooote hiyo iko kwenye mafaili.
Mtamchanganya!!
 
Heee! Jamani! Hayo matatizo yoooote yalikuwa yanamsubiri Mheshimiwa?
Mwacheni atulie kwanza, apange program yake.
Miradi yooote hiyo iko kwenye mafaili.
Mtamchanganya!!
Hizo projects zote zilianza tangu Mbalawa alipokuwa Waziri kabla hajapigwa chini na Makufuli
 
Hizo projects zote zilianza tangu Mbalawa alipokuwa Waziri kabla hajapigwa chini na Makufuli
Sawa. Tuseme wewe ni baba umetoka kazini, hata ndani hujaingia. Unazungukwa na watoto, huyu anasema hili, hajamaliza mwingine kadakia hili, hajamaliza mkewe nae , we!! baba watoto nilisahau kukuambia kuwa unga umekwisha!! Ungefanya mini?
 
Sawa. Tuseme wewe ni baba umetoka kazini, hata ndani hujaingia. Unazungukwa na watoto, huyu anasema hili, hajamaliza mwingine kadakia hili, hajamaliza mkewe nae , we!! baba watoto nilisahau kukuambia kuwa unga umekwisha!! Ungefanya mini?
Natuliza akili,kisha naanza kufikiria nianze kutatua tatizo lipi na lipi nilikaimishe kwa wasaidizi wangu
 
Back
Top Bottom