Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Isack Kamwelwe azikaribisha nchi wanachama wa SADC kutumia bandari ya Dar es Salaam

mkiluvya

JF-Expert Member
May 23, 2019
802
725
1568704939544.png

1568705012886.png

1568705053170.png

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe amezikaribisha Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini Mwa Afrika (SADC) kutumia bandari ya Dar es Salaam mara baada ya ukarabati wake hasa gati namba sufuri kuanza kupokea mizigo.

Akizungmza Jijini Dar es Salaam alipotembelea kuona meli kubwa ya Mizigo ya Magari ya kampuni ya Meli ya Mv Grand Duke iliyotua bandarini hapo jana, Waziri Kamwelwe alifurahishwa kuona meli hiyo kubwa nyenye urefu wa mita 200 na uwezo wa kubeba magari 6,000 ambapo imetua ikiwa na magari 1,347 imedhihirisha uwezo wa bandari hiyo kwamba iko tayari kupokea mizigo mikubwa.

“Tuko hapa kuwahabarisha Watanzania, na Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC), kwamba ukarabati wa Bandari ya Dar es Salaam unaenda vizuri ikiwa ni pamoja na kukamilika kwa gati namba moja, mbili na hili gati namba sifuri liko mwishoni na limeanza kupokea meli kubwa za Mizigo kama mnavyoona hapo, hiyo ni meli ya mizigo ya magari yenye uwezo mkubwa sana”, Waziri Kamwelwe.

Malengo ya Serikali ni kufanya ukarabati wamagati nane ambapo mpaka sasa gati

namba moja na gati namba mbili yako kwenye matumizi mara baada ya kukamilika

na sasa meli zinaendelea kutoa huduma kama kawaida, gati namba sifuri ambalo ni maalum kwa meli za mizigo ya magari linaendelea na ukarabati lakini asilimia

kubwa liko vizuri.

Waziri Kamwelwe alisema kuwa mara baada ya gati hilo kukamilika Tanzania
itakuwa na uwezo mkubwa wa kupokea mizigo ya magari laki 6 kwa mwaka, lakini
pia bandari hiyo inabeba tani milioni 17 kwa mwaka huku malengo ya Serikali ikiwa ni kufikia tani milioni 25 ifikapo mwaka 2021.

“Malengo yetu ni kufikia tani milioni 25 kwa mwaka tofauti na tani za sasa milioni

17, kwa hiyo Nchi Wanachama wa SADC, bandari hii sasa inafanya kazi vizuri, kwa

hiyo majirani zetu kutoka SADC, DRC, Malawi, Zambia na nchi zingine za ukanda

huu wa Kusini mwa Afrika wanakaribishwa sana kutumia bandari ya Dar es Salaam” Alisisitiza Waziri Kamwelwe.

Waziri Kamwelwe alisema Serikali itaendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na wafanyabiashara kutoka Nchi Wananchama wa SADC ili maeneo ambayo yana changamoto ziweze kutatuliwa haraka.
“Serikali imewekeza fedha nyingi katika ukarabati huo, kwa hiyo itahakikisha kuwa inaipa bandari hii mizigo ya kutosha na hasa kutoka kwa Nchi Wanachama wa SADC, ili kuwawezesha kupata huduma rahisi za usafirishaji” alisema Kamwelwe.

kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari, Mhandisi Deusdedit Kakoko, alisema kuwa gati jipya namba sufuri limeanza kufanya kazi kwa kupokea meli kubwa ya Mv Grand Duke ambayo imetua jana na mzigo wa magari 1347.

“ Hili gati ni Jipya ni kati ya magati nane ambayo yanajengwa, lenyewe limejengwa kwa zege kama mnavyoona, lina uwezo wa kubeba magari 10,000 kwa wakati mmoja kutoka uwezo wa kubeba magari 2,500 ambao tulikuwa nao hapo mwanzo, lakini pia lina urefu wa mita 320 kwa hiyo ni gati kubwa na hii meli ina urafu wa mita 200 kwa hiyo kuna mita 120 zimebakia kwenye gati hili”, Alisema Mhandisi Kakoko.

Gati hilo ambalo ni la kisasa Zaidi litakuwa na taa ambazo zitawezesha kufanyika kazi usiku na mchana hapo bandarini, na makabidhiano ya gati hilo yatafanyika kesho ambapo Mkandarasi ataikabidhi Mamlaka ya Bandari (TPA).

Aidha, Mhandisi Kakoko alisema kuwa meli ya Abiria ziwa nyasa imeingia kwenye majaribio ya mwezi mmoja ambapo mwezi ujao inatarajiwa kukabidhiwa kwa Mamlaka hiyo ili kuanza kuhudumia wananchi wa maeneo hayo.
 
Serikali iwekeze kidogo kwenye vichwa vya traffic police na wakuda wengine wanaosumbua hao wafanyabiashara kutoka SADC.
Mmewasumbua Sana kwa Mambo ya hovyo km asipakie hata radio kutoka Dar akija na nduguze kuosha macho wasipande hiyo gari.
View attachment 1209586
View attachment 1209591
View attachment 1209592

Back
Top Bottom