Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi (Zanzibar) afanya mazungumzo na uongozi wa Posta Zanzibar

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
WAZIRI WA UJENZI, MAWASILIANO NA UCHUKUZI (ZANZIBAR) AFANYA MAZUNGUMZO NA UONGOZI WA POSTA ZANZIBAR

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Rahma Kassim Ali(Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Meneja Mkaazi wa Shirika la Posta Tanzania (Zanzibar) Ndg. Ahmad Mohamed Rashid katika ofisi za Waziri huyo, Kisauni Zanzibar

Katika mazungumzo hayo, Mhe. Rahma Kassim Ali amesisitiza uwepo wa ushirikiano baina ya Posta na Taasisi zingine mjini humo ili kuongeza kasi ya utendaji yenye kuleta tija kwa Taifa

Kwa upande wake, Meneja Mkaazi Zanzibar ametumia nafasi hiyo kueleza maeneo ambayo Shirika la Posta Tanzania lingependa kuongezewa nguvu hasa katika nyanja za usafirishaji.

Akijibu maombi hayo, Mhe. Rahma Kassim Ali ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Shirika la Posta na ameona iko haja ya kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Afya Zanzibar kwa lengo la kuona uwezekano wa kulifanya Shirika la Posta kuwa mchukuzi mkuu wa sampuli za maabara kwa upande wa Zanzibar.

Meneja Mkaazi amemshukuru Mheshimiwa Rahma kwa kukubali kutenga muda kumkaribisha na kuwa tayari kumsikiliza.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano,
Shirika la Posta Tanzania,
03 Novemba, 2021.

Screenshot_20211104-091354.jpg
 
Back
Top Bottom