Waziri wa Ujenzi, Isack Kamwelwe: Ukarabati wa Bombardier utagharimu Bilioni 6 na siyo bilioni 13.9.

Mgambilwa ni mntu

JF-Expert Member
May 30, 2017
2,869
3,188
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Isack Kamwelwe, ametoa ufafanuzi kuwa, matengenezo ya Ndege mbili za Bombardier zinazotarajiwa kupelekwa nchini Canada, yatagharimu Bilioni 6 na siyo 13.9 zilizoripotiwa kwenye vyombo vya habari.

Waziri alisema kuwa, kuna uwezekano mkubwa aliyeandika taarifa hiyo alimnukuu kimakosa ama yeye ndiye aliyetamka kiwango hicho kimakosa. Hivyo gharama ni bilioni 6 kwa ndege mbili, sawa na bilioni 3 kwa kila ndege.

IMG_0634.JPG
IMG_0635.JPG
 
Hongera mh kwa kazi nzr na iliyotukuka, zimekuja juzi juzi tu hvyo sio mbaya tukatumia hayo mabilion kuzikarabati ili zizidi kufanya kazi zaidi kwa manufaa ya umma. Hakika awamu ya tano imeamua na imethubutu, na ndio mana nasema hongereni saaaana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mpeni taharifa huku dumila maji yamejaa na kusababisha kukatika kwa mawasiliano ya barabara ya dom - moro,
asishadadie bombadia yeye sio waziriwa bombadia
 
Mbona hii kitu waziri alisema mwenyewe? Na inakuwaje vyombo vya habari vyooooote nchini ikiwemo mitandao ya kijamii vimnukuu vibaya? Waache kutufanya mazwazwa. Bora wazipack kuliko kutuletea double standards daily. Hiyo Bilioni tatu si mafuta ya kwenda na kurudi na per diem za hao marubani na vibaraka wengine? Mwambie Kamwele sisi sio Wachunga ng'ombe. Aendelee kutafuta mizigo ya kubebwa na dream liner.
 
watatuletea risiti !
maana hata HOSTEL ZA UDOM tuliambiwa ni milioni 500 pekee kwa kila ghorofa..
tofauti na taarifa ya kamati ya bunge iliyoenda kuhakiki..
ila asipate tabu angesema tu ni offer hatutolipa kitu..
unaficha moto wa petrol...
kkkkkk !

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzungu mjanja sana....anakuuzia ndege mpya zenye mapungufu kiufundi ili baada ya muda urudi kwa ajili ya matengenezo akupige tena hela, hii kwa lugha ya kigeni inaitwa passive income

Ni km alivyofanya kwenye kompyuta anatengeneza makusudi virus ili atuuzie antivirus.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ulitegemea Msukuma anaeogopa english amzidi ujanja mzungu?
 
Ni ukarabati ni service.. Hebu tuwekeni sawa.. Maana Bavicha wanadai ni ukarabati kwamba ndege ni mbovu tumepigwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa ni maintenance ya kawaida, je matrilioni na mabilioni yote hayo yanalipika? tunaweza kurudisha mtaji na kupata faida na kufaidi matunda? au ndio mkenge tumeingizwa kwa ushamba wa Magu?
 
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Isack Kamwelwe, ametoa ufafanuzi kuwa, matengenezo ya Ndege mbili za Bombardier zinazotarajiwa kupelekwa nchini Canada, yatagharimu Bilioni 6 na siyo 13.9 zilizoripotiwa kwenye vyombo vya habari.

Waziri alisema kuwa, kuna uwezekano mkubwa aliyeandika taarifa hiyo alimnukuu kimakosa ama yeye ndiye aliyetamka kiwango hicho kimakosa. Hivyo gharama ni bilioni 6 kwa ndege mbili, sawa na bilioni 3 kwa kila ndege.

View attachment 995860View attachment 995861
They do not keep their words ''public figure ought to keep their words''
 
Back
Top Bottom