Waziri wa ujenzi Dr.P.Magufuli apiga marufuku matuta kwenye highway | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri wa ujenzi Dr.P.Magufuli apiga marufuku matuta kwenye highway

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TGS D, Jan 4, 2011.

 1. TGS D

  TGS D Senior Member

  #1
  Jan 4, 2011
  Joined: Aug 3, 2010
  Messages: 114
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  waziri wa ujenzi dr.pombe magufuli amepiga marufuku uwekaji wa matuta katika barabara kuu.amesema kwamba katika sheria ameapa kuzitumia hajaona mahali palipoandikwa kwamba wakandarasi waweke matuta kila baada ya umbali fulani.Ameyasema hayo alipokuwa akiongea na wahandisi wa viwanja vya ndege na wakala wa barabara-tanroads.

  source:Taarifa ya habari channel 10.www.chtentv.com
   
 2. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Magufuli ni waziri anayekwenda kwa mantiki. Hafanyi kazi kwa kubahatisha. Namuunga mkono na miguu kwa asilimia mia.
   
 3. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,793
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Mhh itakuaje wakati komakoma mnyamala tuta lilijengwa kwa 40m?si hasara likivunjwa?
   
 4. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #4
  Jan 4, 2011
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Ni usumbufu kwa waendeshaji na wakati mwingine matuta haya yanayowekwa kuokoa maisha ya waenda kwa miguu yamesababisha ajali kwa waendeshaji.

  Lakini Mbona alipokuwa waziri wa wizara hii ktk kipindi cha kwanza hakuliona kama tatizo? Sasa hivi hata barabara ndefu kabisa km. Dar-Mz, zina matuta kama shamba la viazi!
  Wananchi wanaofunga barabara kuomba matuta atawaridhisha namna gani?
   
 5. k

  kayumba JF-Expert Member

  #5
  Jan 4, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35

  Hii inaweza kuwa na mantiki, si vyema kuweka matuta kwa vile tu mtoto amegongwa na wananchi wamezuia barabara na mwishowe mkuu wa wilaya anasema weka tuta hapo!

  Kupunguza ajali ni kutoa elimu kwa watumia wote wa barabara; yaani madreva, waenda kwa miguu, waendesha baskeli n.k.

   
 6. Nyamgluu

  Nyamgluu JF-Expert Member

  #6
  Jan 4, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 3,147
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Ok. Yanakera sana Lakini sheria ni kwa ajili ya watu! Inakueje kwa vijiji/sehem zenye watu wengi si ajali za watu kugongwa zitakua nyingi. Ilula ikiwa haina tuta Taqwa ikishusha down ile hehehehe sipati picha. Mimi ningependekeza yawe ya viwango flani sio kufutwa kabisa.
   
 7. mundo

  mundo JF-Expert Member

  #7
  Jan 4, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 200
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Kama unakumbukumbu nzuri alizuia vile vile.
   
 8. Mbaha

  Mbaha JF-Expert Member

  #8
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 697
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  No... that's not enough!!! Magufuli can do better than that!!!.... Hayo matuta yamewekwa kwa fedha za walipakodi. Hatua gani atachukua kwa waliosababisha hasara hiyo? Kama ameagiza yatolewe basi na awachukulie hatua wote waliohusika kuyaweka!!!
   
 9. lm317

  lm317 JF-Expert Member

  #9
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 452
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Halafu sasa litavunjwa kwa 80m!!!
  Ndio utajua uchitema nshale!
  uchimumunya nshale!
  TULIA UNYOLEWE VIZURI
   
 10. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #10
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 651
  Trophy Points: 280
  mkuu utakuwa umesahau. Hata wakati ule matuta yalikuwa marufuku highway. Na ni kweli hayatakiwi ni usumbufu na kuharibu magari ya watu. Pia inadhalilisha kwani wageni hutuona kama si wastaarabu na hatuna akili. Watu wafundishwe kufuata sheria na faini ziongezwe na pia hao wanaodai matuta kwa kulala barabarani sheria ifuate mkondo wake dhidi yao. Mtu akigongwa kwa uzembe wake au mtoto kwa uzembe wa mzazi then wanakijiji wanalala road kudai matuta. Huo ni umbumbumbu na hasa serikali inaposhindwa kuwaelimisha na kukimbilia kuweka matuta, tena makubwa ya kutisha. Watoe elimu kwa wananchi namna ya kutumia barabara huko mashuleni. Pia madereva waelimhshwe na police wa usalama barabarani kila wapitapo badala ya kupiga mkono na kuomba buku, maji ya kunywa au chai atoe elimu ya alama za barabarani.
   
 11. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #11
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Matuta yanasababishwa na miondo mbinu mibovu hakuna sehemu za kuvuka watu kwanini yasiwekwe madaraja ya kuvukia watu na si kila sehemu ni ya kuvuka .
   
 12. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #12
  Jan 4, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Ni kweli
   
 13. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #13
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 651
  Trophy Points: 280
  kaka faini zikiwa kubwa hawatashuka hapo ilula kwa speed. Kosa moja liwe laki mbili unusu kama ilivyokuwa juzi kwa cheng na si elfu ishirini tena. Pia wananchi wapewe elimu ya kuvuka barabara na tungeweza kupunguza. Kuweka matuta panafanya watu kuwa wazembe na pia madereva kuwa wa..,.. Matuta hayafai. Mafuta yenyewe yako juu plus bumps ni serikali kukomoa wananchi.
   
 14. Capital

  Capital JF-Expert Member

  #14
  Jan 5, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,036
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  matuta ni janga kwa waendeshaji. Katika road zenye matuta nilizowahi kuendesha ni Tinde-Kahama-Ushirombo. Namuunga mkono Dr Pombe
   
 15. Mtumpole

  Mtumpole JF-Expert Member

  #15
  Jan 5, 2011
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,445
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 145
  Kwani komakoma mnyamala(Mwananyamala) nayo ni highway!
   
 16. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #16
  Jan 5, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,520
  Likes Received: 19,943
  Trophy Points: 280
  wajenge madaraja kama la manzese
   
 17. M

  Mitimingi Member

  #17
  Jan 5, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mheshimiwa Magufuli, nilikuwa ninakusubiri ukae nione kama ungelikumbuka hili agizo lako la awali. Uliwahi kutoa tamko hili kuwa matuta kwenye high way hapana. Ninakupongeza sana sana kwa hilo. Ninakuomba ujenzi ni kazi ya kitaaluma na kuna vipimo,,,,,Je inakuwaje TANROADS hapana ngoja niwaite vizuri TANLODS wataalam wanaweka matuta ambayo hayana vipimo? Kila tuta lina size yake...

  Angalizo:

  • Sehemu zote zenye matuta ndipo barabara inpoanza kuharibika kutokana na magari kujikita chini au kusimama hapokwa muda mrefu zaidi kwani yanatembea polepole.

  • Matuta ni chanzo cha foleni
  • Matuta yanawapa vibaka nafasi ya kuvamia magari.
  • Magari madogo yote yanaharibika kwenye matuta.
  Mimi ninafikiri Tanzania tunaongoza kwa kuwa na matuta mengi sana barabarani...Hii mimi binafsi ninahisi ni kwa kuwa nchi yetu ina siasa ya kilimo kwanza na wenzetu wa "TANLODS" wameona ni vyema kupiga matuta ya viazi kwenye barabara za Lami.....Nenda angalia matuta ya Bwawani Mororogo, kibaigwa, karibu na nyumba ya kikwete mikocheni, ..utaweza kupita only if unaendesha KAMAZ....but kama ni TAXI kama ya mheshimiwa Magufulini lazima uache exhaust barabarani.

  Kuhitimisha: Watanzania tuwe na solutions ambazo zinakubalika kimataifa na zinaleta tija. Matatu mhhh tumekosea...
   
 18. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #18
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kwa sisi tulioonja elimu wakati wa mkoloni na kidogo baada yake, tulibahatika kuwa na ugeni wa mara kwa mara shuleni kwetu, ugeni wa police constables, ambao walikuwa wakitufundisha namna ya kutumia barabara, namna ya kuwa raia wema na kazi zao kwa ujumla. Baada ya miaka si mingi ya uongozi wa Nyerere hiyo ikafa kama alivyouwa kila kitu chema hapa kwetu. Nasikia wakati huu wa JMK, Afande Saidi ameianzisha tena hii. It may take another 20 Years to be affective, kwani kubomowa ni rahisi kuliko kujenga.

  Nampongeza Magufuli kwa kuona kero hili la matuta, si tu yanasabisha ajali, yanaharibu barabara, yanaharibu magari, yanafanya magari yatumie mafuta mengi zaidi na hayapunguzi vifo vya ajali za barabarani. Naona Mzee wa ma-statistics kaona hasara za haya matuta.
   
 19. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #19
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,796
  Likes Received: 1,338
  Trophy Points: 280
  Leo hujapata Ganja nini?
  Kuna siku unaamka na akili akili Dar Es Salaam.
   
 20. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #20
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,262
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Matuta ni muhimu yaendelee kuwepo why? Vijijini mpaka mjini watoto wanagongwa sana hata kama kuna vibao vya kuonyesha kuwa kuna shule bado madereva wana overspeed, madereva wengi hawafuati sheria za barabarani. Kuna shule mi niko jirani nayo kwa mwezi mtoto mmoja sometime wawili every month walikuwa wanagongwa, wameweka matuta na hakuna habari ya kugongwa watoto. Ushauri wangu yawepo ila yasiwe makubwa kivile
   
Loading...