Waziri wa Uchukuzi, Mh. Omari, mimi ninakuelewa lakini je? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri wa Uchukuzi, Mh. Omari, mimi ninakuelewa lakini je?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kibunago, Jun 6, 2011.

 1. Kibunago

  Kibunago JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2011
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 288
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Waziri wa Uchukuzi , Mh. Omar, mimi ninamwelewa na nimemkubali.

  Kupitia ITV amesema tuimarishe PPP na sio kutegemea bajeti ikiwa ni pamoja na kukaribisha wawekezaji kwa kuwapa vivutio, kuingia Ubia na pia ubinafsishaji ; tuondoe ukiritimba katika huduma zetu za usafiri na tuongeze ushindani katika usafirisaji ili kuboresha huduma na kupunguza gharama kwa wateja.

  Ni kwa kiwango gani Wanasiasa na Vyama vya Wafanyakazi wanamwelewa na watampa ushirikiano juu ya anachoeleza hususani suala ka kukaribisha Wawekezaji toka nje na kuingia nao mikataba jambo ambalo sasa inabidi ulitetee huku unatokwa jasho baada ya yaliyoonekana mfano katika Mamlaka ya Reli yetu na katika eneo la Nishati & Madini.  Mwisho nimeuona ukweli wake wake alipogusa kwa lugha laini tatizo la uzabuni wa ‘Car tracking system’ ambao tayari umepigiwa kelele na baadhi ya wamiliki wa mabasi.  Nilichokikosa kwake ni kutoongea kwa ushupavu na nguvu zote kukemea wanaochelewesha wateja na mizigo yao bandarini na wadokozi na pia kama Waziri, tone yake juu ya hiyo tracking system isingekuwa kama ya kulalamika bali ya kuagiza utaratibu mpya ulio wazi na unaozingatia kupunguza ajali katika mazingira mbalimbali na wenye wazabuni wengi utumike.  Vinginevyo nimejisikia vizuri sana kuona wasomi kama hawa wanapata nasafi kutumia ujuzi na uzoefu wao walioupata nje na ndani ya nchi katika maendeleo ya nchi yao!
   
 2. Jiwejeusi

  Jiwejeusi JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 755
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Naona unamsaidia kujikosha, maneno yenu hayaleti ndege wala treni na hayawezi kuondoa ukiritimba wa ticts bandar. Lakin endelen tu kubwabwaja kwani ni kawaida yenu, mmeshazoea.
   
 3. MWEEN

  MWEEN JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2011
  Joined: Feb 6, 2010
  Messages: 472
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Hata mimi nilimuelewa ila hakutoa dawa ya kufanikiwa. Sababu ni kuwa serikali iilea uzembe na ufisadi ndani ya mashirika haya kwa manufaa ya wachache. Hivyo hata wakisema hiyo PPP etc etc, mambo ni yale yale ya kula sasa shirika la serikali litalipa baadaye.

  Kwa upande wangu, dawa ni kuwawajibisha wale wote waliohusika kwenye kufilisi mashirika haya kwa kuwafunga na kuwafilisi ili iwe fundisho kwa watakaokabidhiwa wasirudie. Then tunaweza kusema labda kazi itafanyika
   
 4. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #4
  Jun 7, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,815
  Trophy Points: 280
  Mkuu unajua hii dhana ya PPP ni nzuri sana ila inatakiwa itumike sehemu ambazo hazina rushwa na ubnafsi kama hapa Tanzania. Nchi hii imejaa rushwa na ubinafsi hivyo PPP si mahala pake. Tutakuja shituka upande mmoja wa PP ni viongozi wetu ambao walikuwa madarakani wakati wa kuingia mikataba ya PPP. Tunatakiwa tuwe na legal and regulatory framework za jinsi ya kuendesha PPP. Najua sheria imeishapitishwa lakini siju kama stakeholders walishiriki vipi pia elimu kwa umma juu ya PPP haipo. Suala la PPP ni la kwenda nalo taratibu.
   
 5. Bob

  Bob JF-Expert Member

  #5
  Jun 7, 2011
  Joined: Sep 10, 2007
  Messages: 277
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Ni nani anatakiwa kushugulikiwa ukiritimba? Kuweka mzingira mazuri ya uwekezaji?
  Mlalamikiwa anapokuwa mlalamikaji.
  Give me a break!
   
 6. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #6
  Jun 7, 2011
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,692
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 180
  PPP siyo kitu kipya hapa Tz. Sioni tofauti yoyote itakayoletwa na PPP. Imani katika PPP inaweza kuja kama pande mbili katika huo ubia zina nia njema na kuaminika. Kama upande mmoja wa PPP (yaani Public) ni Serikali ya Tanzania nini kitawazuia wale wanousimamia kuutumia kwa manufaa yao binafsi badala ya manufaa ya uma kama wanavyofanya sasa? Je, kampuni hizo za wawekezaji wa nje zinaaminika? Kama hakuna MTz makini wa kuangali maslahi ya taifa unadhani wawekezaji ndio watafanya hivyo? Basi tusingekuwa na matatizo katika sekta ya madini. Suluhisho ni kujenga uwezo wa wakezeji wa ndani. Nina maana ya waTz halisi siyo wale wanaoiba kwetu sasa ili kesho wale vizuri wakiwa Uingereza, Nanada, Australia, US, nk. hasa Wahindi.
   
 7. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #7
  Jun 7, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Sheria na utaratibu upo

  vyombo vya sheria vipo

  acha vifanye kazi zao

  waziri si kazi yake kuviambia vyombo husika kufanya kazi zao

  sasa unaposema aongee kwa ushupavu then iweje? Upuuzi huo kaachiwa Pombe na wenzie wanataka kumanage as if wako kwenye kampeni za siasa

  Nundu piga mzigo achana na hawa watu ambao wako stuck kwenye enzi za Nyerere
   
Loading...