Waziri wa Uchukuzi afanya ziara kushtukiza kukagua 'Flow meters'

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,575
Prof. Mbarawa afanya ziara kushtukiza KOJ Kurasini.

1101.jpg

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiongea na baadhi ya wafanyakazi wa TPA eneo la kupakulia mafuta yanayoingia nchini (KOJ) Kurasini jana jiji Dar es salaam. Wa kwanza kulia Mhandisi anayefanya kazi eneo la KOJ Jabiri Muyones.

267.jpg

Kapteni Abdulla Mwingamno (kulia) akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kushoto) baadhi ya vifaa vya kituo cha kupakulia mafuta yanayoingia nchini (KOJ) Kurasini jana jiji Dar es salaam.

346.jpg

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akiongozana na Mhandisi anayefanya kazi eneo la KOJ Jabiri Muyones alipotembelea TPA eneo la kupakulia mafuta yanayoingia nchini (KOJ) Kurasini jiji Dar es salaam.

442.jpg

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akikagua baadhi vipuri eneo la kupakulia mafuta yanayoingia nchini (KOJ) Kurasini jiji Dar es salaam.

536.jpg

Eneo la kupakulia mafuta yanayoingia nchini (KOJ) Kurasini jiji Dar es salaam.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amemuagiza Kaimu Meneja Msaidizi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Nelson Mlali kufanya uhakiki wa kampuni zinazotoa huduma mbalimbali bandarini ili kuboresha utendaji kazi na kuepuka mgongano wa maslahi binafsi minongoni wa watumishi wa bandari.

Profesa Mbarawa alitoa kauli hiyo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza jana jioni(29/03/2016) kwenye ofisi za Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) eneo la kupakulia mafuta yanayoingia nchini (KOJ) Kurasini.

“Mtafanyaje kazi na mtu ambaye ni mfanyakazi na huku kampuni yake inatoa huduma bandarini, hamuoni kutakuwa na mgongano wa kimaslahi binafsi,” alihoji Profesa Mbarawa.

Aidha, Prof. Mbarawa amemtaka Kaimu Meneja Msaidizi Mlali azingatie umiliki wa makampuni kulingana na taarifa za Wakala wa Usajili wa Biashara na Kampuni nchini (BRELA) katika zoezi la kuhakiki kampuni hizo.

Akiwa eneo la (KOJ) Kurasini, Prof. Mbarawa amewataka wafanyakazi wa TPA wabadilike na kufanya kazi kwa juhudi na maarifa badala ya kufanya kazi kwa mazoea ili kuboresha kuongeza ufanisi na kuliongezea taifa mapato kwa manufaa ya wananchi

Prof. Mbarawa amewaagiza pia Mamlaka ya Bandari wanaponunua vipuri na vifaa mbalimbali vinavyohitajika bandarini hapo wazingatie vipimo sahihi kulingana na vifaa vinavyohitajika kuendeshea mitambo mbalimbali ili kulipunguzia taifa gharama zisizohitajika.

Chanzo: Muhidin Issa Michuzi
 
Naona, Mbarawa anajitahidi kuyatumbua! Aongeze kasi kidogo wizara yake kubwa sana! ajiwekee lengo la kutumbua jipu1 kwa siku, yanaweza kwisha baada ya mwaka
 
“Mtafanyaje kazi na mtu ambaye ni mfanyakazi na huku kampuni yake inatoa huduma bandarini, hamuoni kutakuwa na mgongano wa kimaslahi binafsi,” alihoji Profesa Mbarawa.
naona mnajaribu kudivert hoja ya m.c.c kwa flash news kama hizi!hivi huu wimbo wa utumbuaji majipu bado una hit sokoni?
 
naona mnajaribu kudivert hoja ya m.c.c kwa flash news kama hizi!hivi huu wimbo wa utumbuaji majipu bado una hit sokoni?
Wenzako wapo kwenye mada ya kupunguzwa mishahara vigogo wanaopata shs.milioni 40 kwa mwezi, wewe bado upo MCC! Issue ya MCC ilishaisha hiyo na wenzako wanasonga mbele kufanyakazi kwa bidii ili nchi yetu ijitegemee.
 
oho,kumbe,halafu wakisha wapunguzia hao ma c.e.o,watawaongezea kina nani?naona mnakomalia watumishi wa umma tu!
 
oho,kumbe,halafu wakisha wapunguzia hao ma c.e.o,watawaongezea kina nani?naona mnakomalia watumishi wa umma tu!
Subiri kaka! Rais wako anaipeleka Tanzania kwenye "service" ya nguvu ili baadaye tusidharauliwe tena na vimisaada vyenye masharti uchwara. Tumpe muda JPM kwani hajatimiza hata miezi sita katika uongozi wake.
 
na ule wa msaada wa japani wa 100 billioni,hauwatii aibu?
 
Wao walitoa masharti gani kama yalikuwepo, nikumbushe!
kupewa vitalu vya kuwinda wanyama katika mbuga zetu,na hii ikaonekana ina tija zaidi kwa serikali ya jpjm kuliko yale ya m.c.c ya kurudia uchaguzi zenji kui revamp sheria ya mtando!
 
kupewa vitalu vya kuwinda wanyama katika mbuga zetu,na hii ikaonekana ina tija zaidi kwa serikali ya jpjm kuliko yale ya m.c.c ya kurudia uchaguzi zenji kui revamp sheria ya mtando!
Ungeweka ushahidi wa maneno yako angalau ningekuamini kidogo! Kwamfano, hivyo vitalu vipo wapi na ni mwaka gani wamepewa etc!
 
“Mtafanyaje kazi na mtu ambaye ni mfanyakazi na huku kampuni yake inatoa huduma bandarini, hamuoni kutakuwa na mgongano wa kimaslahi binafsi,” alihoji Profesa Mbarawa.
wafanyakazi wa aina hiyo yafaa kuachishwa kazi mara moja na kuchunguzwa namna walivyoweza kupata kandarasi kama utaratibu ulifuatwa. haitakiwi kupepesa macho kuhusu jambo hili kama hatutaki kufanya utani kwenye mambo ya corporate governance.
 
naona mnajaribu kudivert hoja ya m.c.c kwa flash news kama hizi!hivi huu wimbo wa utumbuaji majipu bado una hit sokoni?
MCC wala si hoja si chochote! Kabla ya MCC nchi yetu ilikuwa haiendi? Acheni kujikomba kwa Wamarekani haisaidii. Angalieni Libya na nchi zingine zimeishia wapi?
 
Back
Top Bottom