Waziri wa TAMISEMI, Ummy Mwalimu amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Waziri wa Tamisemi, Ummy Mwalimu amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, Anosta Nyamoga kupisha uchunguzi.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatano Aprili 21, 2021 na kitengo cha mawasiliano serikalini imeeleza kuwa Ummy amechukua hatua hiyo baada ya kupokea malalamiko na tuhuma za ubadhilifu wa fedha za miradi ya maendeleo katika halmashauri hiyo kutoka kwa wananchi, viongozi na vyanzo vingine.

Waziri Ummy amemuagiza katibu mkuu wa Tamisemi, kupeleka timu ya uchunguzi mara moja na kumuelekeza mkuu wa Mkoa wa Kigoma kuhakikisha timu hiyo inapata ushirikiano katika kipindi chote cha utendaji wao ili kumaliza kazi hiyo kwa wakati.

Jana Jumanne Aprili 20, 2021 Ummy alimsimamisha kazi mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Magesa Boniphace kupisha uchunguzi.

Taarifa ya Tamisemi ilieleza kuwa Boniphace alisimamishwa kazi baada ya Ummy kupokea malalamiko na tuhuma za ubadhirifu wa fedha za miradi ya maendeleo katika halmashauri hiyo kutoka kwa wananchi na viongozi mbalimbali akiwemo mbunge wa Sengerema (CCM), Hamisi Tabasamu.
 
Lakini pia hiyo Wizara yake iwe wazi kabisa kutoa maelezo ni vipi ifanye ukarabati wa Nyumba za viongozi mikoani kwa bei za kutisha. Yaani shilingi 555,000,000 kwa ajili ya ukarabati wa nyumba moja tu? Kibaya zaidi fedha iliyotengwa kwa kununulia Madawa kwa sehemu husika haifikii hata asilimia 20 ya huo ukarabati. Jamani hili limekaaje.
 
Hivi Magufuli zile kelele zake kumbe zilikuwa buree kabisa..

Ama kweli wajinga ndo waliwao.
 
Hivi vichwa vyote nchi nzima vinashindwa kutafuta muarobaini wa kudhibiti ufujaji wa fedha za umma kweli?? au yamejaa maigizo watu waonekaane wanafanya kazi kumbe kutumbua si kielelezo cha kazi??
 
Back
Top Bottom