Waziri wa TAMISEMI, George Simbachawene amteua Mhadhiri wa UDOM, Profesa Mwamfupe kuwa Diwani

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Waziri wa TAMISEMI, George Simbachawene amteua Mhadhiri wa UDOM, Profesa Mwamfupe kuwa Diwani katika Manispaa ya Dodoma.

Mytake;

Hii inatumika kama pale tu Madiwani hawana kiwango fulani cha Elimu.. Nafikiri wazee wa ndio mnabidi mjiongeze

=======

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), George Simbachawene amemteua Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Profesa Davis Mwamfupe kuwa diwani katika Manispaa ya Dodoma.

Juzi Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi alimtaja Profesa Mwamfupe pamoja na wenzake wawili Roze Nitwa (CCM) na Vicent Tibalindwa (CHADEMA) kuwa waliteuliwa na Waziri kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo.

Kunambi alisema Simbachawene aliteua majina sita kwa vyama vya CHADEMA na CCM ndipo wakayapigia kura likiwamo jina la Mwamfupe aliyetokea CCM.

“Waziri alitumia sheria namba 288 (24) (2d) ya Serikali za mitaa na kanuni za uteuzi za mwaka 2010 sura ya 4 (1) na 5 (1) vinavyompa mamlaka ya kufanya hivyo bila kuulizwa na humteua mtu ambaye ni mkazi wa eneo husika,” alisema Kunambi.

Manispaa ya Dodoma haina Meya baada ya Jaffary Mwanyemba kuondolewa na madiwani Machi mwaka huu kwa madai ya matumizi mabaya ya madaraka.

Hata hivyo, Mkurugenzi huyo alikana madai ya kumwandaa msomi huo wa uchumi katika nafasi ya Umeya ingawa alisema kila mtu mwenye sifa za kuwa diwani ana haki ya kugombea nafasi ya uongozi ikiwamo meya.

Mkurugenzi huyo aliwaondoa hofu waliokuwa wamejenga nyumba zao katika maeneo ambayo hayajapimwa kabla ya kuvunjwa kwa CDA akisema hawatasumbuliwa badala yake watarasimishwa huku akitoa tahadhari kwa wavamizi wa maeneo na viwanja kuwa lazima watavunjiwa.

Naibu Meya wa Manispaa ya Dodoma, Jumanne Ngede alisema baraza la madiwani halina shaka na uteuzi huo na kwamba watapewa ushirikiano katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ikiwamo mchakato wa makao makuu.

Alisema mpango uliopo katika manispaa hiyo ni kujipanga kuwa na ugeni mkubwa ambao umeingia mkoani hapo ikiwemo maofisa wa serikali.

Mmoja wa madiwani ambaye hakupenda kutajwa jina lake alisema mpango wa uteuzi wa msomi huyo unaweza kuwagawa madiwani kwani kuna kila dalili za kuandaliwa kushika kiti hicho huku wengine wakitaka apewe nafasi katika kamati ya uchumi na fedha tu ili akaonyeshe uzoefu wake huko.


Chanzo: Mpekuzi
 
Waziri wa TAMISEMI, George Simbachawene amteua Mhadhiri wa UDOM, Profesa Mwamfupe kuwa Diwani katika Manispaa ya Dodoma-

Mytake

Hii inatumika kama pale tu Madiwani hawana kiwango fulani cha Elimu.. Nafikiri wazee wa Ndio Mnabidi Mjiongeze
Mbona sielewi
 
From being a university professor to councilman..??
Damn sorry ..hizi ni dalili za siku moja PhD holder kuja
kuteuliwa kuwa balozi wa nyumba kumi.

ndo maana kina flani wanasema kuwa kile ni chuo cha....
maana maprof wa UDSM wanateuliwa nafasi za maana
kama kudili na makinikia, etc wa UDOM kuwa madiwani...daaa
inatia uchungu ridandasi.
 
From being a university professor to councilman..??
Damn sorry ..hizi ni dalili za siku moja PhD holder kuja
kuteuliwa kuwa balozi wa nyumba kumi.

ndo maana kina flani wanasema kuwa kile ni chuo cha....
maana maprof wa UDSM wanateuliwa nafasi za maana
kama kudili na makinikia, etc wa UDOM kuwa madiwani...daaa
inatia uchungu ridandasi.
Kwani ni Mara ya kwanza professor kuwa diwani?
 
Mjue kuwa Dodoma haina mstahiki meya kwa sasa na ni jiji tarajiwa linalokua kwa kazi.Hivyo ni lazima kuwa na meya msomi ili kumudu changamoto za Makao makuu ya nchi.
 
Diwani aliyekuwepo kaenda wapo?. Makao makuu inaanza kuheshimika....km amekubali hongera yake na ya manispaa pia!!
 
From being a university professor to councilman..??
Damn sorry ..hizi ni dalili za siku moja PhD holder kuja
kuteuliwa kuwa balozi wa nyumba kumi.

ndo maana kina flani wanasema kuwa kile ni chuo cha....
maana maprof wa UDSM wanateuliwa nafasi za maana
kama kudili na makinikia, etc wa UDOM kuwa madiwani...daaa
inatia uchungu ridandasi.

Kuna tatizo gani Professor akiwa balozi wa nyumba kumi?
 
Hivi Professor wa Chuo cha Umma/Serikali si Mtumishi wa Umma? Maana sijui kama sheria inamruhusu mtumishi wa umm
a. Karibu kwenye uchambuzi kwa wale political analysists
tradeoff lecturer for councilor
 
Mwalimu wangu huyu guru wa Human Geography leo anaenda kuwa Diwani?!!! Hongera zake. Nakukumbuka sana kwa umahiri wako miaka ile pale Mlimani.
 
Ngoja ni-digest kwanza....

Lakini dah, tuacheni masihara jamani... hii serikali kwa teuzi tu, alhamdulillah, "inatujali" sana wananchi!!

Kumbe serikali zilizopita zilikuwa zinatubania tu bhana... kumbe kuna hadi madiwani wa kuteuliwa!!

Halafu ngoja... huyo diwani anaweza kuteuliwa kuwa meya? But why not? Ikiwa mbunge wa kuteuliwa anaweza kuwa waziri why not diwani wa kuteuliwa asiwe meya!!!

Lile sakata la madiwani wa manispaa ya Dodoma kumkataa meya liliishia wapi?
 
Waziri wa TAMISEMI, George Simbachawene amteua Mhadhiri wa UDOM, Profesa Mwamfupe kuwa Diwani katika Manispaa ya Dodoma-

Mytake;

Hii inatumika kama pale tu Madiwani hawana kiwango fulani cha Elimu.. Nafikiri wazee wa ndio mnabidi mjiongeze
Evidence please!
 
Back
Top Bottom