Waziri wa Sheria UK kubadili sheria ya uhamiaji kufanikisha kuwaondoa wahalifu wa kigeni. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri wa Sheria UK kubadili sheria ya uhamiaji kufanikisha kuwaondoa wahalifu wa kigeni.

Discussion in 'International Forum' started by Richard, Nov 21, 2011.

 1. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #1
  Nov 21, 2011
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,274
  Trophy Points: 280
  Waziri wa sheria wa UK bwana Ken Clarke anamalizia mipango ya kubadilisha sheria ya uhamiaji ili kuondoa sehemu zote ambazo zinazingatia sheria ya haki za binadamu ambapo majaji wataweza kuruka sehemu hizo ili kuwarudisha nchini kwao wale wahalifu wote wa kigeni ambao watakuwa wamefungwa jela za UK kwa zaidi ya mwaka mmoja.

  Katika miezi ya hivi karibuni kumekuwa na kelele zinazoelekezwa kwenye sheria ya haki za binadamu ambayo inaitwa kwa kiingereza Human Right Act, ambayo katika sehemu yake ya nane inatoa nafasi kwa raia anaeishi katika moja ya nchi za Ulaya kupata kinga dhidi ya hatua yoyote ya kumrudisha raia huyo katika nchi anayotoka ambayo ipo nje ya bara la Ulaya. Hiyo ni kwa sababu raia huyo kama atakuwa ana familia basi hataweza kurudishwa kwao kwa kuwa yeye ana familia ambayo inamtegemea.

  Bwana Ken Clarke ambae ni mbunge wa chama kinachotawala cha Concervative kwa pamoja na kile cha Liberal tayari amekwishazungumza na mawaziri wenzie wa sheria wa nchi za Ulaya na kukubaliana jambo la msingi kwamba linapokuwa suala muhimu la msingi katika kesi yoyote hasa zile ambazo mtuhumiwa analeta hofu kwa wananchi kama vile ughaidi na ujambazi wa kutumia silaha, madawa ya kulevya, basi ni lazima sheria hiyo irukwe na raia huyo arudishwe kwao.

  Lakini tayari raia wa kigeni ambao wana kesi za uhalifu nchini humo wameanza kutafuta masuluhisho mbalimbali ya kuhakikisha wanaendelea kuishi nchini humo kwa kukwepa kurudishwa makwao na mojawapo ni kuanza familia au kutafuta watoto waliozaliwa kutokana na mahusiano kati ya raia hao na raia wenyeji wa UK ambao ni waingereza.

  Chama cha Concervative kiliahidi kwenye kampeni yake za uchaguzi kwamba kingepunguza namba ya raia wa kigeni ambao huja nchini humo kutoka laki moja hadi chini ya elfu kumi tu kufikia mwishoni mwa mwaka 2011. Lakini ahadi hiyo imekuwa ikikumbana na vikwazo mbali mbali vikiwemo uhaba wa maofisa wa idara yake ya uhamiaji (UK Border Force) kwenye viwanja vya ndege na kwenye vituo vya mipaka kama pale Calais kusini mwa London.

  Vikwazo vingine ni kama vile kukosekana kwa takwimu sahihi ambazo ni za raia ambao ama waliingia kama wanafunzi au watalii nchini humo idadi ambayo inasemekana ni kubwa kama ilivyokuwa ikifikiriwa hapo mwanzo na ni idadi ambayo ilisababishwa na sera za chama Labour ambacho kilikuwa madarakani kwa miaka kumi.

  Pia suala la raia ambao wanaishi nchini humo kinyume cha sheria ambao idadi yao inakisiwa kuwa ni zaidi ya laki mbili na nusu. Idadi hii pia inachangiwa na na upotevu wa takwimu sahihi kwani maofisa ambao walipaswa kushughulikia makabrasha ya raia hawa waliamua kuyatupia kwenye hifadhi maalum ya kumbukumbu au Archive ambayo iliwekwa kama siri.

  Kama nchi zingine kubwa za Ulaya na Marekani nchi ya UK imekumbwa na matatizo ya kiuchumi kama mfumoko wa bei ambapo bei za mafuta na vyakula zimepanda.

  Pia raia wake wenye umri chini ya miaka 24 hawana ajira na hawana uhakika wa maisha ya baadae na hali hiyo imefanya kuwepo kampeni maalum za kuwasaidia watoto hao kutafuta kazi za kujiajiri na kulazimishwa kwenda kazini.

  Hata hivyo raia wa kigeni nchini humo ndio wamekuwa wakienda makazini na kujishughulisha kwenye maeneo mbalimbali kama vile mahoteli, migahawa, kwenye maduka makubwa, hospitalini, mabohari na kwingine. Raia kutoka iliyokuwa Ulaya Mashariki, Afrika na na nchi kama Spain, Portugal na Greece wamekuwa wakitembea kifua mbele kwa kujidamka mapema kwenye saa kumi na moja na nusu usubuhi kuwahi kazini huku vijana wa kiingereza wakiwa wamelala usingizi wa pono.

  Nipe mawazo yako je wewe upo unaishi Ulaya hasa UK na je unaonaje maisha ya sasa ukifananisha na miaka tuseme kumi iliopita?
   
Loading...