Waziri wa Sheria na Katiba: Wanaopata ajali za mabasi walipwe fidia

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,682
22,685
Waziri wa Sheria na Katiba, Asha- Rose Migiro amewataka Watanzania kutumia Sheria ya Madhara kudai haki zao baada ya kupata ajali ya basi.

Alisema Watanzania wanaweza kuanzisha shauri la madai katika kipindi cha miaka mitatu tangu wapate ajali hiyo iliyosababishwa na uzembe ili kulipwa fidia.

Sheria hiyo ya madhara ni zaidi ya Sheria ya Bima ambapo wananchi wanaopata ajali katika mabasi wanatakiwa kudai.

Migiro alikuwa anaongezea majibu ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Ame Silima kuhusu stahiki za aliyepata ajali katika basi lililoulizwa na Mbunge wa Kibaha Mjini Silvestry Koka (CCM) katika swali lake la nyongeza.

Naibu Waziri huyo alisema kwamba watu wanaopata ajali wanastahiki zao na ingawa hawafahamu ni lazima wadai fidia hizo kwani magariyanapokosa bima ni kosa la jinai.

Alisema serikali inataka watu wafahamu hivyo ingawa anajua watuwa bima hawaisemi wazi kwa kuhofia kupata hasara.

Akijibu swali la msingi la Mbunge huyo la taratibu zikoje katika ajali na muda unaotakiwa kupita kumaliza tatizo la ajali mahakamani, Naibu Waziri Silima alisema makosa ya Usalama Barabarani ni sawa na makosa mengine ya jinai na huendeshwa kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Mashitaka na sheria inatoa mwongozo wa muda wa siku 60 kukamilisha upelelezi na uendeshaji wa kesi mahakamani.

Aidha alisema kwamba kunapotokeaajali dereva anatakiwa kusimama eneo la tukio na kutoa msaada kamamaisha yake hayamo hatarini au kujisalimisha Polisi.

Chanzo: Habari Leo

Attachments

  • 1432835093544.jpg
    1432835093544.jpg
    9.3 KB · Views: 217
Isiwe kudai lakini ukalipwa elf kumi, cha msingi serikali iweke taratibu za fidia kwa mfano mtu alie katika mguu au mkono fidia yake isipungue milioni Mia moja, na hii itasaidia waajiri pamoja na bima kuwa makini katika kutoa bima, na waajiri kuwapa magari yao ma driver wenye viwango na makini.
 
Waziri wa Sheria na Katiba, Asha- Rose Migiro amewataka Watanzania kutumia Sheria ya Madhara kudai haki zao baada ya kupata ajali ya basi.

Alisema Watanzania wanaweza kuanzisha shauri la madai katika kipindi cha miaka mitatu tangu wapate ajali hiyo iliyosababishwa na uzembe ili kulipwa fidia.

Sheria hiyo ya madhara ni zaidi ya Sheria ya Bima ambapo wananchi wanaopata ajali katika mabasi wanatakiwa kudai.

Migiro alikuwa anaongezea majibu ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Ame Silima kuhusu stahiki za aliyepata ajali katika basi lililoulizwa na Mbunge wa Kibaha Mjini Silvestry Koka (CCM) katika swali lake la nyongeza.

Naibu Waziri huyo alisema kwamba watu wanaopata ajali wanastahiki zao na ingawa hawafahamu ni lazima wadai fidia hizo kwani magariyanapokosa bima ni kosa la jinai.

Alisema serikali inataka watu wafahamu hivyo ingawa anajua watuwa bima hawaisemi wazi kwa kuhofia kupata hasara.

Akijibu swali la msingi la Mbunge huyo la taratibu zikoje katika ajali na muda unaotakiwa kupita kumaliza tatizo la ajali mahakamani, Naibu Waziri Silima alisema makosa ya Usalama Barabarani ni sawa na makosa mengine ya jinai na huendeshwa kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Mashitaka na sheria inatoa mwongozo wa muda wa siku 60 kukamilisha upelelezi na uendeshaji wa kesi mahakamani.

Aidha alisema kwamba kunapotokeaajali dereva anatakiwa kusimama eneo la tukio na kutoa msaada kamamaisha yake hayamo hatarini au kujisalimisha Polisi.

Chanzo: Habari Leo
 
Imechukuwa muda mrefu serikali kusema ukweli kwa tendon la ajali ambalo limemaliza ndugu zetu. Kwa hill ndugu mheshimiwa Rose nakupa hongera kutuweka wazi tutaitumia vizuri sana.
 
Kama ajali zinaendela, na kama madereva bado ni wagumu kuelewa na kuendelea kusababisha ajali kizembe basi hili lipite, naamini litasaidia sana kupunguza ajali, kwa kuwafanya madereva kufuata sheria, na waajiri kuajiri watu makini, ila fidia isiwe ya kukomoa.
 
Tusubirie tuone utekelezaji wake upo vipi...
 
macho yanauma sijasoma post yote,naomba mtu anijulishe je fidia itatoa serikali au mwenye basi
 
Kuna ajali imeua mtu wa nje ya nchi, ndugu zake wapo kwenye mchakato wa kuwashitaki.
 
Back
Top Bottom