Waziri wa sheria akiri kasoro katika katika kesi za madai;KUNA HAJA YA KUENDELEA NAE? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri wa sheria akiri kasoro katika katika kesi za madai;KUNA HAJA YA KUENDELEA NAE?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Pdidy, Jun 4, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jun 4, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,772
  Trophy Points: 280
  Waziri wa sheria akiri kasoro katika katika kesi za madai

  Na Exuper Kachenje

  WAZIRI wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe, amesema serikali inaangalia uwezekano wa kuondoa utaratibu wa kisheria wa walalamikaji wa kesi za madai, kuwagharamia kwa nauli ya kwenda na kurudi mahakamani, watu wanaowashitaki.


  Utaratibu huo pia unamtaka mlalamikaji, kugharimia chakula kwa wafungwa wa kesi za madai.


  Chikawe alisema serikali imeamua kuangalia upya utaratibu huo baada ya kuona kuwa si sahihi.


  Waziri Chikawe alitoa kauli hiyo wiki iliyopita akiwa katika ziara yake ya kukagua Mahakama ya Mwanzo Machame, mkoani Kilimanjaro.


  Alikuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari, kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu wizara yake.


  Waziri huyo wa sheria na katiba, alisema utaratibu huo unaotumika zaidi vijijini, ambako washitaki wa kesi za madai, wanalazimika kugharimiwa nauli za kuwafikisha mahakamani na kurejea makwao kesi zinapositishwa.


  Alisema jambo hilo ni mzigo na kero kwa wananchi wanaolalamika na kutafuta haki zao mahakamani.


  " Katika kesi hizi za madai toafauti na zile za jinai, anayeshtaki ni mtu binafsi, inakuwa jukumu lake kugharamia nauli, huo ni ukweli, lakini kwa kweli si sahihi. Sasa tunatafuta njia sahihi ya kuondoa tatizo hilo," alisema Chikawe.


  Alisema katika kesi za jinai, ni jukumu la serikali kugharamia kesi hizo na kwamba hiyo inatokana na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwa ndiye inashtaki.


  "Kimsingi serikali inatambua tatizo lililoko katika kesi za madai, lililo mbele yake sasa ni kutafuta utaratibu mwingine, ili kuwaondolea wananchi kero hiyo," alisisitiza.


  Alisema serikali iko mstari wa mbele kuboresha huduma za mahakama na sheria ili kuwawezesha wananchi kupata huduma bora.
   
 2. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #2
  Jun 4, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Mr Impossible pamoja na makala ya kupaste , mchanganuo wako haujaonekana hivyo kulifanya swali lako kuwa redundant
   
Loading...