Waziri Wa Nishati na Madini Kutembelea Mgodi Tanzanite baada ya Kashifa na Kodi na unyanyasaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Wa Nishati na Madini Kutembelea Mgodi Tanzanite baada ya Kashifa na Kodi na unyanyasaji

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KING COBRA, Jul 11, 2012.

 1. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Waziri wa Nishati na Madini amepanga kutembelea Mgodi wa Tanzanite One kabla ya kutoa lesseni ambapo ilizuiliwa baada ya kukwepa kodi ya US$ 2m au Tshs3.5 bils.


  Hata hivyo uongozi wa mgodi huo unafanya maandalizi ya kumupokea Waziri huyo ambaye anatarajiwa kufika kesho huku wakihaha kuficha tuhuma za kumunyanyasa Koplo Raphael ambaye aliumia kazini na kupoteza mkono na Macho!!!
  Koplo Raphael tayari ameandika barua ya kulalamika Ikulu juu ya unyama huo
   
 2. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  [FONT=&quot]RAPHAEL ANDREAS WISSA[/FONT]
  [FONT=&quot]P.O.BOX 30104[/FONT]
  [FONT=&quot]KIBAHA PWANI.[/FONT]
  [FONT=&quot]Mobile : +255 767 007843[/FONT]
  [FONT=&quot]Tarehe: 6/07/2012[/FONT]
  [FONT=&quot]Mhe. Rais ,[/FONT]
  [FONT=&quot]IKULU- DAR ES SALAAM[/FONT]
  [FONT=&quot]P .O.BOX 9120[/FONT]
  [FONT=&quot]DAR ES SALAAM.[/FONT]
  [FONT=&quot]YAH: UKANDAMIZAJI NINAOFANYIWA NA MWAAJIRI [/FONT]
  [FONT=&quot] WANGU BAADA YA KUPATA AJARI KAZINI.[/FONT]
  [FONT=&quot]Mhe. Rais mimi ni askali mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania(JWTZ) mwenye namba MT 62261 na kwamba nimestafu kazi Mwaka 2007 kambi ya kisarawe Mkoani Pwani.[/FONT] [FONT=&quot]Baada ya kupata mafao yangu ya kazi niliamua kujitafutia riziki katika Kampuni iitwayo Tanzanite One ambapo niliajiliwa tarehe 29/11/2009 kama mlinzi wa Mgodi huo ambapo niliwajibika muda wote kulinda madini yanayochimbwa hapo yasiibiwe na wafanyakazi wala kuhakikisha kuwa wafanyakazi wasiowaaminifu hawapati mwanya wa kuiba pia.[/FONT] [FONT=&quot]Mhe Rais , nimefanya kazi hii kwa uaminifu mkubwa hasa nikizingatia maadili ya Jeshi niliyojifunza na kupelekea kuaminiwa na mwaajiri wangu mda wote nilipokuwa kazini.[/FONT] [FONT=&quot]Hatahivyo tarehe 25 /3/2011 ,Mgodi wa Tanzanite One unaofanya shughuli za uchimbaji wa madini Mererani Arusha , ulishambuliwa na Majambazi ambao pamoja na silaha zingine za kivita walitumia BOMU la Kurusha kwa Mkono ambapo lilinijeruhi mimi na kukimbizwa katika Hospitali ya KCMC Moshi na baadaye kutibiwa katika hospitali zingine hapa nchini kama inavyo onyesha katika vyeti vya matibabu.[/FONT] [FONT=&quot]Hata hivyo niweke wazi kuwa matibabu yote haya yaligharimiwa na mwaajiri wangu ikiwa ni pamoja na kuendelea kulipa mshahara wangu hadi sasa.[/FONT] [FONT=&quot]Mhe Rais ajari hiyo imeniletea ulemavu wa macho ambapo madaktari wamesema sitaweza kuona tena maishani na hata barua hii nimeandikiwa na mtoto wangu kwani siwezi kumuona kabisa .[/FONT] [FONT=&quot]Kwa ujumula ajari hiyo imesababisha nipoteze macho, Mkono na ulemavu wa mguu ambao ulivunjika wakati wa ajari hiyo kama inavyo onekana katika picha nilizo ambatanisha sambamba na baurua hii.[/FONT] [FONT=&quot]Tangia nipate nafuu ya ajari hii nimejaribu kufuatilia mafao ya kuumia kazini lakini viongozi wa Tanzanite One ambao ni watanzania wenzangu wameshindwa kunisaidia na wakati mwingine wanasema sina haki katika hilo.[/FONT] [FONT=&quot]Ni kwa sababu hii mimi nimeamua kukuandikia barua hii huku nikiwa sikuoni na wala sitakaa nikuone lakini nina imani kuwa wewe unawaona wahusika akiwemo mwaajiri wangu ambaye mimi nashindwa kumufuatilia kwasababu nimepata ulemavu wa Maisha wakati nalinda mali zake za mabilioni zisiibiwe.[/FONT] [FONT=&quot]Kwa kuwa niliumia kazini nikiwa chini ya Mwaajiri wangu ijapokuwa ni raia wa kigeni lakini ameingia nchini kisheria na anaongozwa na utawala wa sheria na sheria za nchi yetu zinajari mafao ya kuumia kazini ninakuomba unisaidie nipate haki yangu sawa sawa na sheria.[/FONT] [FONT=&quot]Mimi nimefanya kazi Jeshini kwa zaidi ya miaka 22 hadi na staafu sijapata kuona manyanyaso kama haya . Bila shaka Manyanyaso haya yameletwa na Wageni na wapo wengi wanafanyiwa hivi na kwa kutojua Watanzania wengi wanao nyanyaswa na wageni hawa ,wanaweza kukuchukia wewe bure. Mimi nimepata ujasiri wa kukuandikia barua hii baada ya kukusikia unahutubia Taifa juu ya mgomo wa Madaktari.[/FONT] [FONT=&quot]Mhe Rais mimi ni baba wa familia ya Watoto Watano ambapo wote wanasoma shule na mimi ninawajibika kulipa ada . Hata hivyo ninaishi katika nyumba ya kupanga ambapo kwa sasa inadaiwa kodi. Majukumu haya na madai mengine yamenifanya nikose amani kwa kuwa nashindwa kukidhi matakwa haya kwa kuwa nimepata ulemavu wa maisha kazini.[/FONT] [FONT=&quot]Mhe Rais nimeambatanisha picha zangu za Zamani na za sasa ili uweze kujua jinsi Askali wako nilivyo sasa na kunisaidia.[/FONT] [FONT=&quot]Natanguliza shukurani kwa hatua ya msaada wako .[/FONT]
  [FONT=&quot]Ni Mimi katika ulemavu,[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]…………………………………………………[/FONT]
  [FONT=&quot]RAPHAEL ANDREAS WISSA[/FONT]
  [FONT=&quot]TANZANITE ONE REPORT UNYANYASAJI[/FONT]
  [FONT=&quot]Mnamo tarehe 25 March 2011, Majambazi walivamia Mgodi wa Tanzanite One Wakiwa na Bomu la Mkono na Kumushambulia Mlinzi wa Mgodi huo na kumujeruhi COplo RAHAEL ANDREAS WISSA ambapo alikimbizwa kwenye dispensary ya Kampuni na baadaye kupelekwa hospitali ya KCMC kwa matibabu Zaidi .[/FONT]
  [FONT=&quot]Taarifa zinaonyesha kuwa tangia Tarehe 21/06/2011 Bw amekuwa akitibiwa katika hospitali hiyo mpaka tarehe 12/12/2011 ambapo aliruhusiwa kuondoka kwa ajiri ya kuendelea na matibabu nyumbani.[/FONT]
  [FONT=&quot]Utawala wa Tanzania One Ulimuahidi kumupeleka mgonjwa nchini Australia kwa ajiri ya uangalizi maalum wa macho lakini ghafla maamuzi hayo yalibadilika na kufanya uchunguzi huo hapa DSM.[/FONT]
  [FONT=&quot]Hata hivyo tarehe 22/03/2012 CPL Raphael Andreas Wissa alipewa taarifa rasimi na daktari wa The Aga Khan Hospital ,Dar es Salaam kuwa hata ona tena Maishani.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Cpl Raphael alianza kufuatilia haki zake kutokana na kupoteza Mkono, kuto ona tena na kuvunjika mguu lakini ,Mzee MWANI ( 0754 292999) ambaye ni msemaji wa kampuni hiyo alimwambia atapewa Tshs 2,000,000/- .Hata hivyo kampuni hiyo inaendelea kumulipa mshahara lakini hieleweki hatima ya malipo ya fidia kutokana na kuumia kazini.[/FONT]
  [FONT=&quot]Taarifa kutoka ofisi za Malipo zinzonyesha kuwa Cpl Rahael analipwa Tshs 500,000/= lakini pesa halisi inayomfikia kwa mwezi ni Tshs 280,000/=.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Hadi sasa Mgonjwa hawezi kufanya kazi yoyote Maishani na hawezi kuingiza kipato chochote na hivyo kupati kama mlemavu wa maisha. Mpaka naandika waraka huu , Mgonjwa anadaiwa Kodi ya Nyumba, ada za watoto na madeni yanayotokana na majukumu yake kama Mwanaume na baba wa familia.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Sambamba na taarifa hii Wametajwa Wahusika kadhaa ambao wapo upande wa Tanzanite One kama ifuatavyo:[/FONT]
  [FONT=&quot] Mining Manager( Mr Damiani) 0767 600903; Mr Dotto ( 0767 600916, 0755 496717); Mzee MWANI ( 0754 292999) Msemaji wa kampuni; Mr WESSEL MARAI (0754 600994) General Manager; Mr Bernad Oliver (0754 600992) Chief Executive Officer; Balozi Ammy Mpungwe ( 0754 222333) Mweyekiti wa Bodi ya wakurungenzi Tanzanite One ambaye alikuwa balozi wa Tanzania South Africa na ndiye aliyewaleta Wawekezaji hawa kuja kupora mali ya umma; Mr Deogratias( 0767 600996) Afisa Usalama wa Mgodi.[/FONT]
  [FONT=&quot]Mr Maliki (0754 3163030 dereva anayemwendesha Balozi Ammy Mpungwe[/FONT][FONT=&quot][/FONT]
  [FONT=&quot]UHUJUMU UCHUMI NA UKWEPAJI KODI.[/FONT]
  [FONT=&quot]Wakati Serikali ikikosa pesa za kutosha kukidhi bajeti ya 2012/2013 na kushindwa kuwalipa madaktari mishahara wanayotaka ,Kampuni ya Tanzanite One inafanya jitihada kupbadilisha jina na kuitwa RichLand Resources kwa Malengo ya kukwepa kodi. Pia Uchunguzi umebaini kuwa hujuma hiyo ya kuikosesha mapato serikali inaongozwa na Wazawa akiwemo Balozi Ammy Mpungwe na Mzee MWANI ambao wanatumia Uzoefu wao Kubadilisha kampuni na kupora mali ya umma. Hata hivyo tumeweza kubaini kwamba Kampuni ya Tanzanite One inayo jishughulisha na Shughuli hatalishi za Uchimbaji madini haina Insurance inayolingana na hatari inayo wakumba Wafanyakazi kwa malengo ya kukwepa kulipa fidia huku wakipora nchi.[/FONT]
  [FONT=&quot] Kampuni hii imejika zaidi katika Mkoa wa Arusha Mirerani na kwa sasa kutokana na kukwepa kodi inadaiwa na serikali Zaidi ya dola za Marekani Millioni Mbili[/FONT]
  [FONT=&quot] (US$2,000,000 ) sawa na Tshs 3,149,480,000/-kutokana na kutolipa kodi mbalimbali kati ya mwaka 2004 hadi 2008. Taarifa zinaonyesha kuwa wapo wafanyakazi wasiowadilifu kutoka TRA ambao wamekuwa wakipewa rushwa na kuelekeza mbinu za kukwepa Kodi hiyo huku wakiwashauli wahusika kubadili jina la kampuni.[/FONT]
  [FONT=&quot]Baada ya Mpango huo wa siku nyingi kubainika , serikali imezuia kutolewa kwa lesseni mkwa Kampuni ya Tanzanite One hadi deni hilo litakapo lipwa ikiwa ni pamoja na kutekeleza masharti mapya ya sheria ya madini ya mwaka 2010.[/FONT]
  [FONT=&quot]Masharti hayo ni pamoja na kurejesha 50% ya hisa zake serikalini kwa mujibu wa sheria hiyo ili zigawanywe kwa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro na kwa wananchi wazawa.[/FONT]
  [FONT=&quot]Hata hivyo Balozi Ammy anatajwa kuandaa mpango ili wazawa watao chukua hisa hizo wawe ni wale walioko kwenye mtandao wake ili mali hizo zirudi kwa wenyewe.[/FONT]
  [FONT=&quot] Pia inaonyesha kuwa leseni ya kampuni hiyo imeisha muda wake Juni 30,2012 na kwamba hadi sasa imezuiliwa kupewa nyingine hadi mashart yatakapo tekelezwa.[/FONT]
  [FONT=&quot]Sambamba na masharti haya , kampuni hiyo imepewa sharti la uchafuzi wa mazingira ambapo imelazimishwa kuhakikisha uchafu unaotokana na uchimbaji huo hauathiri wananchi wanao zungunguka mgodi huo.[/FONT]
  [FONT=&quot]Aidha wametakiwa kuangalia usalama wa wafanyakazi ikiwa ni pamoja na wale wanaoumia kazini.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]​
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
   
 3. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #3
  Jul 11, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Kwa jina la Mwenyenzi MUNGU kwa hali hii ya makaburu kunyanyapaa ndg zetu Mi binafsi siungi hoja mkono.

  Kwa wahusika! Msiwape hawa wezi wa mali ya umma leseni mpk walipe kodi ya serikali tangu 2004 hadi 2008? Hii haikubaliki!

  Tunashukuru kwa hii news Mkuu!
   
 4. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #4
  Jul 11, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Prof Muhongo, wewe ni mtaalam ukiyebobea katika geology. Tusaidie Watanzania, hali ni mbaya sana migodini.
   
 5. B

  Bob G JF Bronze Member

  #5
  Jul 11, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  yawezekana kapewa zigo lake karuhusu na kutoa leseni,
   
 6. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #6
  Jul 13, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Prof muhogo (0715 555555) yupo mbioni kuwapa makaburu wa tanzanite one lesseni baada ya kutoa rushwa
   
 7. K

  Kiula Senior Member

  #7
  Jul 13, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 114
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hiyo namba uliyoweka hapo ni ya Maswi Katibu mkuu Nishati na Madini siyo ya Waziri
   
 8. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #8
  Jul 14, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Namba ya Ammy Mpangwe mwenyekiti wa Bodi ni0767222333
   
 9. A

  ASKOFU MSAIDIZI JF-Expert Member

  #9
  Jul 17, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unyanyasajitanznite one makaburu kutoka south afrika unatisha wanawaita wafanyakazi wa kiafrika ubwa!!!??
   
Loading...