BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,139
Date::7/31/2008
Waziri wa Nishati na Madini awawashia moto Wakorea kwa kumdharau
Na Habel Chidawali, Mpwapwa
Mwananchi
WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja, juzi aliwajia juu wanunuzi wa madini wakiwamo raia wa Korea akisema wamemdharau kwa kutoka nje katika semina ya madini wilayani hapa.
Ngeleja aliyasema hayo baada ya kutoa hotuba ya ufunguzi wa semina iliyokuwa imeandaliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mpwapwa kwa lengo la kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kujua thamani za madini na namna ya kuondokana na umasikini kwa kutumia rasilimali hiyo.
Waziri huyo alipomaliza kutoa hotuba yake ya ufunguzi juzi katika Ukumbi wa Sinema mjini Mpwapwa, wanunuzi hao walisimama na kutoka ukumbini wakati mada kuhusu madini ikitolewa na Afisa Madini Mkazi na kujikuta akiwa na wanachama wa CCM na wananchi.
Baada ya kuona hivyo, Ngeleja alimtuma Katibu wa CCM wa Wilaya hiyo, Deogratius Rutta, kutoka nje kwenda kuwafuata wanunuzi hao ambao wengi wao ni raia wa Korea na kuwaambia warudi ukumbi.
Walipoingia ukumbini, aliwashambulia kwa maneno na kubadilika ghafla sura yake na kuwa mkali mithili ya mbogo.
Ngeleja aliomba kipaza sauti na kuanza kusema kwa ukali kuwa Wakorea hao, wameshindwa kumheshimu kwa kuonyesha kumdharau hizo mbele yake na kusisitiza kuwa anaamini wageni hao wanawadharau zaidi raia wa kawaida wanaowauzia madini.
Aliendelea kusisitiza kuwa, dharau zao hizo zinaonyesha kuwa huenda zinatokana na kuwanyonya Watanzania wanaowapelekea madini hayo kwa kununua kwa bei ndogo.
Ngeleja alisema anakielewa Kiingereza huenda kuliko wao na kusisitiza kwamba hawezi kukitumia kama wao wanavyotaka kwa sababu katika mkutano huo wengi wao wanazungumza Kiswahili ambacho ni lugha mama ya Tanzania.
''Nimechukizwa sana na kitendo cha ninyi kuondoka katika mjadala huu wakati mkijua kabisa kuwa hili linawahusu na ninyi nawaheshimu na kuwajali, lakini katika hili mmeniudhi sana siwezi kuvumilia ni lazima niseme,'' Ngeleje alisema na kuendelea kutoa dukuduku lake kwa akaongeza kuwa:
''Hamjui kuwa mimi ndie mwenye dhamana ya madini hapa Tanzania kwa niaba ya Watanzania wote, ninaweza kusema hapana au ndio kwani kutokujua sheria isiwe chanzo cha kuvunja sheria, hata katika nchi zenu kuna taratibu na sheria kwani muda wote mliokaa hapa hakuna mtu anayeweza kuwatafsiria Kiswahili ndio maana mkaamua kuondoka, naomba tuheshimiane.''
Aliwaambia wanunuzi hao kuwa ni lazima watafute wakalimani ili wanapokutana na umati katika hafla kama hizo, waweze kutafsiriwa kila kinachozungumzwa kuliko kutaka kulazimisha kiongozi kuzungumza Kiingereza katika nchi yake wakati kuna Kiswahili ambacho kinaeleweka na wananchi wengi wa vijijini.
Mmoja wa wanunuzi hao alisimama na kutuliza mzuka wa Waziri kwa kuomba radhi kwa niaba ya wenzake.
Mnunuzi huyo aliyejulikana kwa jina moja la Omary alimwomba Waziri Ngeleja kuwasamehe na kuahidi kuwa hawatarudia kitendo kama hicho katika mikutano ya aina yoyote.
Omary alisema kwa kuwa amekaa kwa muda mrefu jijini Dar es Salaam anakifahamu Kiswahili vizuri, hivyo atakuwa mstari wa mbele kuwatafsiria wenzake kila neno lililokuwa likizungumzwa katika semina hiyo.
Kutokana na Waziri huyo kuchukizwa na kitendo cha wanunuzi hao, walikaa hadi saa 12:00 jioni juzi semina hiyo ya siku moja ilipofungwa.