Waziri wa Nishati January Makamba, fedha za miradi mipya ya Tanesco bajeti 2022/2023 hadi sept 2022 hazijapekwa kanda ya ziwa

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,802
21,398
BARUA YA WAZI KWA Mh.JANUARY MAKAMBA WAZIRI WA NISHATI .

Ninakusalimu kwa jina la jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Pamoja na salam hizi , ninaomba tukufikishie ujumbe wa barua hii uupate ili uifanyie kazi kuilinda na kuiheshimu heshima ya Rais wetu Samia na kuenzi kauli yake ya kaxi iendelee.

Nije kwenye mada, ulipitia mikoa yote ya kanda ya ziwa ukigawa gas ya kupikia kwa wakinamama kanda ya xiwa hilo tunakupongeza na asante sana .

Sasa changamoto iliyopo mikoa yote ya kanda ya ziwa tanesco uliitengea fedha kupitia bajeti ya wizara yako 2022/2023 fedha kwa ajili ya miradi mipya kupeleka umeme maeneo yasiyo na umeme.

Hadi sept 2,2022 hakuna mkoa hata mmoja umetumiwa fedha za ujenzi wa mirafi hiyo na haijulikani ni lini miradi hiyo itaanza kutekelezwa kupitia muda wa bajeti hiyo ya serikali.

Wananchi wa kanda ya ziwa wanakwenda mbali wakilalakika kutokuwa na umeme kitu kinacho ashiria wananchi na wanaccm kanda ya ziwa, kutokuwa na imani na kauli ya Rais samia ya kupeleka huduma muhimu na kwa wakati ili kupunguza ukali wa maisha.

Tunakuomba mh makamba ujitahidi fedha ulizozitengea bajeti kwa miradi hiyo mipya uzitume ili miradi hiyo iweze kufanyika kwa wakati na wananchi waendelee kuitetea na kukilinda chama tawala kama mboni ya jicho.

Ni matumsini yetu tanesco mikoa ya kanda ya ziwa itapokea fedha hizo kabla ta tarehe 10.9.2022, kwani tulijaribu kumpigia simu Katibu mkuu wa wizara ya Nishati Eng. Mramba alijibu yeye sio msemaji wa wizara ya Nishati.

Pamoja na salam za chama tawala peleka salam zetu kwa mh Rais samia suluhu, tunampenda na aliko mama kanda ya ziwa tupo.
 
Wapeleke umeme haraka machimboni. Gharama za matumizi ya Diesel ziko juu sana. Kanda ya ziwa Ina migodi kibao ya wachimbaji wadogo. Mheshimiwa Waziri liangalie hili
 
Wapeleke umeme haraka machimboni. Gharama za matumizi ya Diesel ziko juu sana. Kanda ya ziwa Ina migodi kibao ya wachimbaji wadogo. Mheshimiwa Waziri liangalie hili
Pamoja na hilo ili huko kuna vijiji mamia na maelfu havina umeme na wananchi wanataabika sana.
 
Wapeleke umeme haraka machimboni. Gharama za matumizi ya Diesel ziko juu sana. Kanda ya ziwa Ina migodi kibao ya wachimbaji wadogo. Mheshimiwa Waziri liangalie hili
Wafanyabiasha wa mafuta wakisikia iyo kauli wanakulaani maana wao wanataka waendelee kuuza mafuta. Kufa kufaana alafu jua biashara ya mafuta ni ya wanaotakiwa kutoa Fedha ili umeme uende. Akili ku mkichwa. Kazi kwako kuzika au kusafirisha
 
BARUA YA WAZI KWA Mh.JANUARY MAKAMBA WAZIRI WA NISHATI .

Ninakusalimu kwa jina la jamhuri ya muungano wa Tanzania...
Ndugu mteja!

Tunashukuru kwa taarifa yako,tunaomba kukupatia ufafanuzi kuwa hakuna uhaba wa bajeti kwa miradi inayoendelea maeneo ya Kanda ya Ziwa kama ulivyodai, kinachofanyika ni kutangaza zabuni (tender) kwa maeneo ambayo miradi ya kusogeza miundombinu ya umeme inapaswa kufanyika jambo ambalo lipo hatua za mwisho kutekelezwa.

Tunaomba kuwatoa hofu wateja wetu wa Kanda ya Ziwa na maeneo mengine nchini kuwa TANESCO imejizatiti kuhakikisha kasi ya utekelezaji wa miradi ya usambazaji umeme inaenda kwa kasi nzuri ili kuwahakikishia wateja wetu upatikanaji na ubora wa umeme.

Hitimisho
Kama unatatizo la moja kwa moja au eneo fulani tafadhali onesha namba yako ya simu, tatizo na eneo husika kwa ufafanuzi au hatua zaidi au wasilisha taarifa zaidi kwa barua pepe zifuatazo customer.service@tanesco.co.tz na seniorzm.lake@tanesco.co.tz kwa hatua zaidi au huduma kwa wateja kwa namba 0748550000

TANESCO Kanda ya Ziwa
 
Ndugu mteja!

Tunashukuru kwa taarifa yako,tunaomba kukupatia ufafanuzi kuwa hakuna uhaba wa bajeti kwa miradi inayoendelea maeneo ya Kanda ya Ziwa kama ulivyodai, kinachofanyika ni kutangaza zabuni ( tender) kwa maeneo ambayo miradi ya kusogeza miundombinu ya umeme inapaswa kufanyika jambo ambalo lipo hatua za mwisho kutekelezwa.

Tunaomba kuwatoa hofu wateja wetu wa Kanda ya Ziwa na maeneo mengine nchini kuwa TANESCO imejizatiti kuhakikisha kasi ya utekelezaji wa miradi ya usambazaji umeme inaenda kwa kasi nzuri ili kuwahakikishia wateja wetu upatikanaji na ubora wa umeme.

Hitimisho
Kama unatatizo la moja kwa moja au eneo fulani tafadhali onesha namba yako ya simu, tatizo na eneo husika kwa ufafanuzi au hatua zaidi au wasilisha taarifa zaidi kwa barua pepe zifuatazo customer.service@tanesco.co.tz na seniorzm.lake@tanesco.co.tz kwa hatua zaidi au huduma kwa wateja kwa namba 0748550000

TANESCO Kanda ya Ziwa
Ninashukuru kwa majibu mazuri kutoka tanesco .

Sasa ni lini au mwezi gani kazi ya ujenzi wa hiyo miradi itaanza baada ya tender kukamilika?

Je kipindi hiki wakisubiri miradi hiyo kutangazwa wananchi wa kanda ya ziwa wajiandaeje kupokea miradi hiyo?

Mwisho ni mikoa ipi inayotarajia kufaidika na miradi hiyo?

Je miradi hiyo ikitanzwa wananchi watajuaje tender zimetangazwa wa maeneo husika ili waanza kufanya wiring kwenye makazi yao na kujiandaa kufungua viwanda?
 
Wafanyabiasha wa mafuta wakisikia iyo kauli wanakulaani maana wao wanataka waendelee kuuza mafuta. Kufa kufaana alafu jua biashara ya mafuta ni ya wanaotakiwa kutoa Fedha ili umeme uende. Akili ku mkichwa. Kazi kwako kuzika au kusafirisha
Waziri wetu ni msikivu sana huyu jamaa atatimiza ombi langu. Hayo ya kwako yanakufaa wewe tu bwanakaka
 
Tulieni kwanza,
Someni alama za Nyakati,
Nchi now iko Zanzibar, Pwani na Mbeya, (Kusini)

Nyie kanda ya Ziwa nakanda ya kati na Kaskazini MTULIE KWANZA tutakuja kuchukua Kura zetu 2025
Pia kaskazi shukuruni UFADHILI WA WAFANYA BIASHARA royal tour na Kuruhusu Tanzanite,

Wengine Lipeni Tozo kwanza
 
Back
Top Bottom