Waziri wa Nishati, January Makamba afanya kikao na mabalozi wa Norway, Sweden na Saudi Arabia

Waziri wa Nishati Mheshimiwa January Makamba amefanya kikao na mabalozi wa nchi za Norway, Sweden na Saudi Arabia nchini Tanzania. Katika kikao hicho amezishukuru nchi hizo kwa mchango mkubwa wanaoipatia Tanzania katika kuendeleza sekta ya nishati.

Waziri Makamba amesema nchi hizo zimeendelea kutoa ushirikiano kwa Tanzania kwa kufadhili miradi mbalimbali katika sekta na kuongeza kuwa Serikali itaendelea kunufaika na fursa mbalimbali zinazotelewa na nchi hizo kwakuwa zipo tayari wakati wowote kufanya kazi na Tanzania.

View attachment 2015132View attachment 2015133View attachment 2015134
Makamba wizara moja imekushinda, sasa unataka uraisi. Utawezaje mudu wizara zote?
 
Watanzania tuna matatizo sana mnapinga kila kitu yule mzee mlimuita kichaa mungu akawaondolea mkaletewa mwenye huruma mnalalamika mnataka raisi wa aina gani ndugu zangu.
 
January anaishi katika dunia yake ya kufikirika kinyume na uhalisia. He has psychiatric disorder called maladaptive daydreams. In his daydreams, he creates fictional characters or idealized versions of himself. ( Labda wa mtu fulani maarufu!)


Hili linaweza kuleta madhara kwa Mama Samia na taifa. Anahitaji usimamizi na uangalizi juu ya uraibu wake hasi, deep inside his mind. Hawa wazungu wanaweza kutumia hii weakness kuingia mikataba ya kilaghai.
 
Tunawaziri kijana lakini katawaliwa na fikra za vijimisaada! Hatuna waziri mwenye ubunifu. Tanzania swala la nishati hivi bado tunalilia misaada na kuongea na mabalozi ofisini tena waziri wa nishati? Waziri ambae anataka sifa toka kwa mabalozi ajioneshe yeye ni yeye! Badala afikirie nje ya box kunamikakati ipi ya ndani kuhakikisha tunakuwa na umeme imara. Tanzania ina kila kitu.

Yeye anapenda zoga ili kujionesha ni mtu wa kimataifa. Nadhani January Makamba, huna ubunifu, umefika mwisho wa kufikiri, huna jipya la kuisaidia Tanzania katika kuondokana na tatizo la nishati. Mawazo yako yanabaki tu kutaka sifa za urais. Nakuhakikishia hutokaa uwe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huna sifa na hufai kabisa.
 
Back
Top Bottom