Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani leo anafanya kikao na Makatibu Wakuu wa Wizara zenye jukumu la kujenga miundombinu wezeshi

Jemmie

JF-Expert Member
Mar 6, 2018
216
285
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani leo anafanya kikao na Makatibu Wakuu wa Wizara zenye jukumu la kujenga miundombinu wezeshi kwa ajili ya Mradi wa Kufua Umeme wa Megawati 2100 kutokana na maporomoko ya Mto Rufiji pamoja na watendaji wa Taasisi zinazohusika na ujenzi wa miradi hiyo.

Kikao hicho kinachofanyika mjini Morogoro kinalenga katika kujadili hatua za utekelezaji miradi hiyo ambayo inapaswa kukamilika tarehe 10/10/2018 ili kuwezesha kuanza kwa ujenzi wa Mradi huo wa umeme.

Kazi za ujenzi wa miundombinu wezeshi ya Mradi, zinazoendelea kutekelezwa ni pamoja na kuufikisha umeme katika eneo la ujenzi wa Mradi, ujenzi wa barabara zote kuelekea kwenye Mradi ikiwemo inayotoka Ubena Zomozi, yenye umbali wa kilomita 178.4 pamoja na ya Kibiti – Lingungu yenye umbali wa kilomita 210, ujenzi wa mitambo ya maji pamoja na matenki makubwa mawili yenye uwezo wa kuhifadhi lita 22,500 na hivyo kuweza kuhudumia wafanyakazi takribani 11,000.

Kazi nyingine zinazofanyika ni ukarabati wa majengo ya nyumba za wafanyakazi pamoja na ujenzi wa miundombinu ya mawasiliano kwa njia za simu na ujenzi wa Reli.

Kazi nyingine inayotekelezwa ni ujenzi wa Bwawa lenye eneo la kilomita za mraba 914 lenye uwezo wa kuhifadhi maji kiasi cha mita za ujazo takribani bilioni 35.

Katika kikao hicho Waziri wa Nishati amewaagiza watendaji wa Wizara na Taasisi hizo kuhakikisha kuwa wanafanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha kazi ndani ya wakati.
Katika kikao hicho imeelezwa kuwa ujenzi wa miundombinu ya umeme kwa ujumla umefikia asilimia 60 na vijiji vyote vinavyopitiwa na mradi vimepelekewa umeme.

Aidha huduma za mawasiliano katika eneo la mradi zitaanza kupatikana tarehe 10/10/2018 na huduma hiyo itaendelea kusambazwa katika maeneo mengine yanayozunguka mradi.
 
Mkuu shukrani Kwa Habari!
Sasa Mradi unatarajia kuanza Rasmi lini?
Na Lini Utakamilika ili Standard gauge iutumie?
 
Back
Top Bottom