LUS0MYA
JF-Expert Member
- Aug 4, 2011
- 862
- 1,097
Taarifa ya Wizara ya Nishati imetoka kuwa wizara imeingia ubia na kampuni moja ya arabuni kuzalisha umeme megawati 2000.
Kinachoshangaza ni ule uharaka wa kuanzisha mradi mkubwa wa ubia wakati serikali inatekeleza mradi mwingine mkubwa ambao unamilikiwa na umma kwa asilimia 100 na ambao ukikamilika utazalisha utakaozidi mahitaji halisi ya umeme hapa nchini na kubaki na ziada kubwa.
Kuna shida gani serikali isikamilishe huu mradi kwanza wa bwawa la mwalimu halafu ianzishe huo mradi bila ubia na watu wa nje? Kwanini Serikali yenyewe inajitengenezea mazingira ya kujikosesha nguvu ya kusimamia nishati ya umeme ambayo ni nguzo kubwa katika uchumi baada ya mafuta?
Je, hatujifunzi jinsi ubia katika gesi unavyosumbua katika uzalishaji umeme kwa kutumia gesi? Ifike mahali serikali iangalie upya hii wizara ili ifanye mambo yake kwa kuzingatia manufaa ya nchi na watu wake.