Waziri wa Nishati amuumbua Mkono; Asema anamiliki kampuni ya madini Dubai | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri wa Nishati amuumbua Mkono; Asema anamiliki kampuni ya madini Dubai

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jun 23, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  JUMAMOSI, JUNI 23, 2012 10:50

  NA BAKARI KIMWANGA, DODOMA


  *Asema anamiliki kampuni ya madini Dubai
  *Adai anaishambulia Serikali kwa kunyimwa ‘tenda'
  *Mwenyewe, ajibu mapigo, amtaka Waziri afute kauli


  WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amejibu mapigo dhidi ya Mbunge wa Musoma Vijijini Nimrod Mkono (CCM).

  Amesema kuwa, Mkono aliishambulia Serikali bungeni juzi kuhusu Mgodi wa Makaa wa Kiwira, kwa sababu mbunge huyo ni mmoja wa wamiliki wa kampuni moja ya madini iliyopo Dubai, ambayo iliomba kununua mgodi huo na kunyimwa.

  Profesa huyo aliyasema hayo bungeni jana baada ya juzi, Mkono kulitaka Bunge liunde Kamati Teule, ili kuchunguza ufisadi katika mgodi huo.

  "Pamoja na hatua zote, jana (juzi), kuna mbunge alizungumzia Mgodi wa Kiwira, siwezi kulizungumzia hilo kwani uchunguzi umebaini kwamba, naye ni mmoja wa wamiliki wa kampuni mojawapo ambayo ina makao yake Dubai, ambayo ilikuwa imeomba kununua mgodi huo.

  "Na kwa kuwa mbunge huyo naye ni mwekezaji, siwezi kulizungumzia hili na huenda kuna maslahi na mgongano wa kibiashara katika hili," alisema Profesa Muhongo.

  Kauli hiyo ya Profesa Muhongo ilionekana kutomfurahisha Mkono, kwani baada ya waziri huyo kumaliza kuzungumza, aliomba Mwongozo wa Spika na kukiri kuwa anamiliki kampuni ya madini.

  "Mheshimiwa Spika ninaomba muongozo wako, hili suala la mimi kuwa mmiliki wa kampuni mbona ‘nili declare Interest' mapema!.

  "Kati ya watu ninaowaheshimu sana ni pamoja na mheshimiwa waziri, kwa hiyo naomba afute kauli yake humu humu ndani bungeni," alisema Mkono.

  Alipomaliza kusema hayo, Spika wa Bunge Anne Makinda hakumruhusu waziri kuzungumzia alichosema Mkono, kwa kile alichosema kuwa, Profesa Muhongo hakutaja jina la mtu alipokuwa akichangia.

  "Hapa Waziri sikumsikia akitaja jina la mtu na hata kama unasema ulilisema jambo hilo, nahisi hukusema wakati wa kuchangia jana (juzi), sasa naomba tuendelee na shughuli za michango ya bajeti," alisema Spika Makinda.

  Awali Profesa Muhongo akizungumzia mikakati ya Serikali katika kukamilisha miradi mbalimbali ya umeme nchini, waziri huyo wa Nishati na Madini alisema, hivi sasa wako mbioni kuhakikisha wanatekeleza mradi wa megawati 3000 hadi 5000.

  "Nichukue fursa hii kuwataka wananchi wote ambao wamefanya malipo yao kwa jili ya kuunganishiwa umeme, kwamba tayari nimeshatoa agizo kwa TANESCO hadi kufikia Juni 30 mwaka huu, wananchi wote waliofanya malipo wawe wameunganishiwa umeme.

  "Endapo TANESCO hawatafanya hivyo, basi nitapambana nao kwa mujibu wa sheria na nawaomba wateja wote wawasiliane nami kwa hatua zaidi pindi watakaposhindwa kuunganishiwa umeme," alisema Profesa Muhongo.

  Waziri huyo, alisema pamoja na matatizo yanayozikabili nchi za Afrika, nchi hizo lazima zijipange na kuhakikisha zinaandaa bajeti kulingana na mahitaji yao.

  Akizungumza nje ya Bunge jana, Mkono alisema suala hilo si kweli na atahakikisha analiweka sawa, ili kuondoa utata.

  "Si kweli kwamba mimi ni mmoja wa wamiliki wa kampuni iliyoomba mgodi huu na hakuna ukweli wowote katika hili na haijatokea mimi kuomba kumiliki mgodi huu," alisema Mkono.

  Akichangia mjadala wa bajeti juzi, mbunge huyo wa Musoma Vijijini alisema, mgodi huo wenye thamani ya matrilioni ya shilingi, umeuzwa kwa Dola za Marekani 700,000 (Shbilioni 1.1), kwa kampuni ya Intra Energy ya Australia.

  Mgodi huo uliwahi kuzua malalamiko baada ya kumilikishwa kwa Kampuni ya ANBEN Limited, inayomilikiwa na Rais mstaafu Benjamin Mkapa na Waziri wa zamani wa Fedha, Daniel Yona
  .
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Jamani Angalia hawa Mawaziri wa CCM na Rais wao Mstaafu wanavyopeana Machimbo ya Madini kama peremende

  Ndio hao hao wanaohutubia siasa za Ujamaa na Kujitegemea, Bajeti inakuwa na Mapungufu hawajali kwasababu

  Wanajua wao na koo zao hazifi njaa, wataendelea kuwa Matajiri watakopa na kuiacha nchi na Madeni Makubwa

  Na Malipo yake ni kuwapa hao wazungu madini yetu yote; Wanapitisha Bajeti ya CCM na wanashangilia na hakuna

  pesa. Huyu Mkono Amejenga hizo shule angalau anatunyonya azijenge nchi nzima sababu madini ni ya wananchi wote.

  Ni aibu Gazeti la Uhuru linaandika Mambo kwa Ushabiki na pesa hakuna...


  Hawa waandishi Maisha yao Ni Magumu lakini wanaandika kwa Ushabiki hawajui Mbele wataishije badala ya
  Kuandika ya Maana

  [​IMG]
   
 3. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kumbe ukiliona libunge la ccm linafoka bungeni ujui kuna lilichokua linavizia likakosa!
   
 4. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #4
  Jun 23, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  huyu rais wetu wa zamani mkapa atakua billionea aisee...anamiliki migodi? mmhh
   
 5. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #5
  Jun 23, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Huyu Mkono toka alivyokuwa analipwa na Balali, BOT mamilioni ya dola nilimfuta kabisa, lakini siku hizi amekuwa kipenzi cha Pro-Chadema JF.
   
 6. Ng'wamapalala

  Ng'wamapalala JF Gold Member

  #6
  Jun 23, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 6,332
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 145
  Nafikili ungeiboresha vizuri habari hii kwa kutujuza umeinyofoa kutoka gazeti lipi.

  Kwa habari hii pia kama ni kweli, ninapatwa na wasiwasi na wanasiasa wetu, kwa vile inaonekana wapo kwa ajiri ya maslahi yao.

  Nimrod Mkono alikuwa ni kati ya wabunge wa CCM waliotia saini ili waziri mkuu ajihuzuru au Raisi awawajibishe baadhi ya mawaziri na kati ya hao alikuwa waziri wa Nishati na madini.

  Kumbe kampuni yake iliomba tenda ikanyimwa. Kwa hiyo sahihi yake ilikuwa kwa ajiri ya kulipiza kisasi!!!

  Siasa za Tanzania ni kicheko tupu na ndiyo maana tunaambiwa na
  Swiss National Bank (SNB) kama kuna kiasi cha CHF183m ambapo kwa exchange rate 1 swiss francs ni sawa na Tsh 1,654 zimewekwa na wanasiasa, wafanyakazi serikalini na wafanyabiashara ambazo hazieleweki njia zilizotumika kuzipata.
  Kwa siasa hizi, Tutaendelea kuwa masikini mpaka kiama
   
 7. F

  FJM JF-Expert Member

  #7
  Jun 23, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mkono kuwa mmliki wa moja ya kampuni iliyoomba kuuziwa Kiwira haiwezi kuwa sababu kwa waziri wa Nishati na Madini kutoengelea Kiwira. Infact alichokifanya Waziri ni kujaribu kumziba mdomo Mkono ili asiulize chochote kuhusu mgodi wa Kiwira. Huu ni utawala mbaya. Waziri aseme yote anayofahamu kuhusu Kiwira na sio kutumia kujificha kwenye hoja dhaifu kama alizotoa bungeni.
   
 8. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #8
  Jun 23, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Mkono angetulia tu maana kama kula amekula inatosha sasa hapati tena. Ale zile zile zilimtosha sana!!
   
 9. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #9
  Jun 23, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Mwandishi hakutoshi? Unaweza kumgoogle ukapata anafanya kazi gazeti gani; kwanini niweke Mwandishi iwe habari

  Ya kuchonga?
   
 10. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #10
  Jun 23, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,953
  Likes Received: 1,276
  Trophy Points: 280
  dah! Hii inatisha. Nadhani tukipigana vita ndo tutaheshimiana
   
 11. mzalendokweli

  mzalendokweli JF-Expert Member

  #11
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 21, 2012
  Messages: 578
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
   
 12. B

  Bob G JF Bronze Member

  #12
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ni kwa kua watanzania ni wasahaulifu, Nomrod Mkono amehusika na ufisadi BOT alipokua akisimamia kesi za BOT na kulipwa zaidi ya 500m kila mwezi na BOT, na hawa akina Nimrodi wanajua tuwasahaulifu, kesho na kesho kutwa watatokea wengine wengi 2 kama akina maige wakitoka 2 kwenye uongozi wanajifanya ndo wenye uchungu, watarudi akina Rostam na maneno makali kuisema serikali,
   
 13. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #13
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,073
  Likes Received: 4,003
  Trophy Points: 280
  siasa za maji chafu bwana....! Hivi Mkono kutaka kununua Kiwira na kunyimwa ndo kuna-substantiate mgodi wa mabilioni ya US$ kuuzwa kwa US$ 700,000? Au ndio katika kule kum-silence asiongee kitu? huo mgodi kwa jinsi ninavyoisi mmiliki wake si hiyo kampuni ya Australia bali ni gelesha kutakuwa na fisadi mmoja au katika kuuza fisadi kapokea fedha mara kumi ya aliyouzia! Hii ndio Tanzania tuijuayo!
   
 14. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #14
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Mimi nadhani hii ya kusema aliomba kumiliki akanyimwa ni mbinu ya kuwanyima wabunge kuuliza maswali magumu kwa serikali. Tena kwa hali ya Tanzania huyo ambaye ameomba na kunyimwa ndiye mwenye taarifa za kutosha kuujulisha umma ufisadi uliofanyika.
   
 15. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #15
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  This is very cheap for a Prof + minister. Instead of answering the questions he is attacking the questioner!
   
 16. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #16
  Jun 24, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Mkono alikuwa sahihi kuhoji jinsi mgodi wa matrilioni ulivyouzwa kwa bei ya kutupa. Alichofanya Waziri ni kuitetea serikali, huku akimtusi Mkono ili asiendelee kuhoji.
   
 17. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #17
  Jun 24, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Mkuu swali la Mkono halina uhusiano na hilo. Waziri alitakiwa kumjibu Mkono siyo kumshambulia
   
 18. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #18
  Jun 24, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Hata ukimfuta mkono huna la kumfanya yeye ni tycoon Kama Yule mwamba wa kaskazini lowassa tu
   
 19. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #19
  Jun 24, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Umepitia lakini majibu ya Waziri sijui ni wapi kamshambulia Mkono wakati hata jina hajatajwa.
   
 20. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #20
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Cheki hapa: http://www.newhabari.com/mtanzania_habari/
   
Loading...