Waziri wa Nishati afanye zaidi ya kusambaza umeme kwa wanavijiji

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,298
12,600
Kuna vijiji ambayo tangu dunia hii imeumbwa hawajawahi kuona umeme wa TANESCO, Sasa ni mara Yao ya kwanza umeme unafika kwao. Hii Ina maana kuwa pamoja na kupata faida ya umeme lakini watapata pia hasara za kuwa na umeme kama vile kupigwa shoti, kunaswa na umeme, kuunguza nguo kwa pasi na nyumba na mabweni na shule kwa umeme wa TANESCO.

Nguzo za umeme zitaungua kwa moto wakati wanavijiji wakichoma mabiwi na mapori moto wakati wa kilimo na uwindaji.

Wako wanakijiji watatamani vyuma kwa kazi zao na nguzo kwa aajili ya Kuni.

Wako watakaozitobia nguzo kwa misumali kupigilia vibao vya matangazo Yao mbalimbali ya biashara, bidhaa na huduma wanazotoa kama uganga, kuongeza nguvu za kiume, mikutano, kujiunga na freemason, nk.

Hii inamaanisha usambazaji wa umeme vijijini lazima uende sambamba na utoaji elimu kwa wanajamii kuhusu faida na hasara na utunzaji wa miundombinu ya umeme.

Jambo linaloshangaza ni kuona waziri wa Nishati na uongozi wa TANESCO kufumbia macho watu wanaotoboa nguzo kwa misumali kubandika matangazo Yao bila kuchukuliwa hatua.

Tena watu hao huwa wanacha namba zao za simu na majina Yao kwenye hayo matangazo Yao kitu ambacho kingerahisha ukamataji wao. Lakini TANESCO hawajali kama wengine TU kitu kinachopunguza ubora wa nguzo za umeme.

Nani ameturoga?
 
Nilidhani utaongelea kupanda kwa bei za kuunganishiwa umeme vijijini
 
Nilidhani utaongelea kupanda kwa bei za kuunganishiwa umeme vijijini
Bei kubwa za kuunganisha umeme na umeme wenyewe zikiwa kubwa vijijini kutasababisha watu vijijini waendelee kutumia kuni, mkaa, vibatali na tanesco kukosa mapato kutokana na umeme vijijini.
 
Back
Top Bottom